Je, una mtazamo gani juu ya hili?

Khalu

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
525
565
Wakuu salaam.

Wakuu nimeona nishee na nyinyi hili tukio.

Kuna siku moja nikiwa maeneo ya Mbagala nikitembea pembezoni mwa barabara kuelekea stendi kwa ajili ya kupanda gari, nilitupia macho upande wa barabara kubwa (kilwa road) kwa mbali kidogo nikamuona baba mmoja mtu mzima akivuka barabara kutokea upande niliokuwepo.

Yule baba alikuwa akivuka barabara huku akitoa kitambaa -cha kufutia jasho- katika mfuko wa nyuma wa suruwali yake kwa ajili ya kujifuta jasho, alikitoa kwa kukivuta hivi kidogo, kile kitambaa kilichomoka pamoja na noti tatu, zile noti zikaangukia barabarani pasi na yeye kujua, kwa rangi ya zile noti bila shaka zilikuwa ni noti ya shingi elfu tano, elfu mbili na elfu moja.

Sekunde chache baada ya tukio hilo kutokea, walitoka vijana watatu wa bodaboda, kutokea upande aliotokea yule baba, wakizikimbilia zile noti na kuziokota, kisha wakarejea walipo kuwa.

Yule baba hakuwa na habari ya kilichotokea nyuma yake, yeye aliendelea kujifuta jasho, huku akiangalia magari ili amalizie kuvuka barabara kuelekea upande wa pili.

Binafsi nilishindwa kushangaa, na kubaki nikijiuliza maswali.

Je, ni uungwana kweli mtu kuokota kitu huku anamuona aliye kiangusha na asimrudishie?

Jaribu kuvuta picha ungelikuwa ni wewe umeangusha ni sahihi usirudishiwe?

NB; Huenda nikawa sio mwandishi mzuri lakini nadhani nimeeleweka.
 
Hahahaha nusu nipigane na kijana wa Boda boda Kahama kwenye kijiwe chao, alipita Binti akiwa na kijana, akadondosha buku mbili, boda boda akaifuata faster, nikaomuona!
Nikajitahidi kumwambia yule binti akaniletea shobo nikamsisitiza kuwa umeangusha peda na muda huo nimemshika boda mkono dah.

Kiichotokea basi but binti alichukua buku mbili yake akatokomea akaniachia msala, nadhani sijui walikua wanawahi Guest washenzi wale
 
Sijaelewa...kwahyo ulitaka bint abaki na wewe au? Si umemshtua akaja ichukua?, 😆😆😆! Chadema hamtaki uonevu popote pale😆😆!hongera
 
Huo ni wizi kama wizi mwingine.

Mioyo ya watu imeharibika kwa mambo mengi. Kwa mtu ambaye sio mcha Mungu ataona kama ni bahati yake ila huo ni wizi.

Kwani ukimstua aliyezidondosha hizo pesa utapungukiwa na nini. Kwani utapoziokota na kuzifanya zako zitakutoa kwenye umasikini ulio nao?

JESUS IS LORD!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wamekosa ubinadamu.
 
Naweza kusema ni tamaa tu hakuna jipya hapo

Lakini kiukweli kabisa hao watu walichokifanya wala sio sahihi hata kidogo maana kama umemuona mtu aliyedondosha ni vyema ukamtaarifu kuwa hiki kimetendeka kutoka kwako kuliko hicho walicho Fanya hao boda boda

Ila kuna msemo unasema ukitenda wema umejitendea na ukitenda ubaya umejitendea huo ubaya walioitenda hao watu utawarudia tu Hiyo ni nature
 
Hahahaha nusu nipigane na kijana wa Boda boda Kahama kwenye kijiwe chao, alipita Binti akiwa na kijana, akadondosha buku mbili, boda boda akaifuata faster, nikaomuona!
Nikajitahidi kumwambia yule binti akaniletea shobo nikamsisitiza kuwa umeangusha peda na muda huo nimemshika boda mkono dah.

Kiichotokea basi but binti alichukua buku mbili yake akatokomea akaniachia msala, nadhani sijui walikua wanawahi Guest washenzi wale
Pole sana, mkuu

Hata mimi nilibaki tu nikiwatazama, maana sikuwa na lakufanya, hata kama ningesema nimkimbilie yule mzee nimwabie, ningerudi huku hawa jamaa wangeniruka futi 100.

Sasa si ndio msala unapoanzia
 
Naweza kusema ni tamaa tu hakuna jipya hapo

Lakini kiukweli kabisa hao watu walichokifanya wala sio sahihi hata kidogo maana kama umemuona mtu aliyedondosha ni vyema ukamtaarifu kuwa hiki kimetendeka kutoka kwako kuliko hicho walicho Fanya hao boda boda

Ila kuna msemo unasema ukitenda wema umejitendea na ukitenda ubaya umejitendea huo ubaya walioitenda hao watu utawarudia tu Hiyo ni nature
Umesema kweli.

Ni wachache sana wenye moyo wa kumrudishia mtu kitu chake pale anapokianguasha.
 
Back
Top Bottom