Je, umeshawahi kukutana na mtu aliekuwa hajui habari za Tanzania nae akiwa mtanzania anae ishi nje?

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,645
11,153
Hivi ndugu zanguni Nyerere bado Rais wa Tanzania? Nikiwa laundromat street ya pili tu na Bowling green university na rafiki yangu mmoja Mtanzania na mmoja Msenegal. Tukicheza game za ndani ya hio laundromat akatokea mzee around 55y to 60y. Mimi na huyu mtanzania mwenzangu tukiongea Kiswahili alituangalia na kutusalimu How are you doing guys? Na kuweka nguo kwenye washing machine na kutoka nje. Baada ya dakika 5 akarudi tena na kuweka na nguo nyengine na kuwasha mashine huku akiwa amesimama na mikono yake kiunoni. Akiwa kama mtu mwenye kufikiria kitu na mara kugeuka na kutuuliza kwa kiswahili:- Kiswahili chetu cha Pwani mnatokea Tanzania? Tulimjibu ndio akasema kwanza hongereni ni watu wastaarabu sana nilikuwa nakusikilizeni tu kama mna tabia za kuwasema watu ila nakuoneni mnaongea mambo yenu tu.

Huyu mwenzenu nae anaongea Kiswahili? Nilimjibu hapa huyu ni Msenegal. Akasema hivi Nyerere bado Rais wa Tanzania? Tulibaki kuangaliana machoni mimi na rafiki yangu na kucheka. Ndipo aliposema yeye anaitwa Jumbe anatokea Mwanza yupo amefika USA tokea 1970 mkaazi wa Michigan. Tokea aingie nchini Marekani hakuwahi kwenda wala kujua habari zozote za Tanzania. Hapo na sisi kwa wakati huo tukamjibu kuwa Rais wa Tanzania ni Mh Jakaya Mrisho Kikwete.

Akasema simjui huyo ila ninafikiria kutembelea Tanzania manake sijui hata kama wazee wangu wapo hai. Kwakweli tulibaki kushangaa na alitupatia business card yake bahati mbaya tulipokwenda Cider points ilipotea. Je, umeshawahi kukutana na mtu aliekuwa hajui habari za Tanzania nae akiwa mtanzania anae ishi nje ya Tanzania?
 
JamiiForums-1982044373.gif
 
Mkuu mambo ya laundromat huku hatuyajui, hayo ungeacha hukohuko na ungesimulia tu kwa kifupi au ungesema kwenye maduka makubwa ya kufua na kukausha nguo kwa kutumia mashine kwa malipo, hasa jijini New York ambako mabeberu wameweka mfumo wa watu kutoweza kufua nguo zao kwenye hizo''NHC'' zao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom