Nicas Mtei
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 11,556
- 7,113
Hali zenu ndugu zangu wa humu MMU? Natumaini kuwa wote mu wazima wa afya,Tumshukuru Mungu kwa ajili ya uzima na afya aliyotujalia.
Siku ya leo napenda tuongelee suala zima la uvunjikaji wa mahusiano na nini cha kufanya baada ya kuachana.. Napenda kukushauri kuwa usiwe mpweke na usiwe mnyonge.
Badala ya kujuta, kusaga meno kwa imani kwamba unaonewa, ni vizuri kutuliza kichwa, upate majibu ya mzizi wa tatizo. Inawezekana ukawa ni wewe mwenyewe, kwa hiyo hutakiwi kulia, badala yake futa machozi utazame mbele. Maisha yanaendelea.
Siku zote weka akilini kuwa jawabu la kila changamoto inayoweza kukukabili, ipo ndani ya uwezo wako mwenyewe. Kama mapenzi ni magumu kwa upande wako, ni jukumu lako kuhakikisha yanakuwa mepesi ama kwa kujirekebisha wewe mwenyewe au kuachana na mpenzi msumbufu.
Machozi yako yana thamani kubwa, hutakiwi kuyatoa kwa mtu ambaye hathamini upendo wako kwake. Amekuacha, hupaswi kujiinamia muda wote na kushindwa kufanya shughuli zako. Hebu piga moyo konde, tazama mbele kwa matumaini kwamba kila kitu kizuri kinakuja.
Makosa yako yarekebisha. Kama ulikosea na ukajirekebisha, ukaomba msamaha lakini bado hujasamehewa, vilevile usijute, tazama mbele. Hupaswi kumlimlia mpenzi aliyepita bali jenga picha tamu juu ya mwenzi wako anayekuja. Zingatia kwamba kuna waliolia Farao alipozama Bahari ya Shamu bila kujua kuwa kifo chake ndiyo ukombozi wa wana wa Israel.
Nakutakia kila heri kwenye maisha yako ya kimapenzi.

Nina mtazamo huu katika kuacha ama kuachwa kimapenzi... Na nazungumzia from my Personal experience.
Kwanza siwezi kabisa ingia katika mahusiano ya Mapenzi na mtu ambaye simpendi... Siwezi for the simple reason kuwa I can not imagine kufanya tendo la 6/6 na mtu ambaye sim'feel. Na ninapokuwa katika mahusiano naingia kwa miguu miwili yote, siwezi simamia mguu mmoja sababu sipendi kujiyumbisha ama kuyumbishwa. Hiyo inanifanya kuwa makini, mvumilivu, mstahimilivu na pengine hata ku apply hekima niwapo katika mahusiano ya Kimapenzi. Na namshukuru Mungu I have been lucky to have had Great men.
Pamoja na kuwa yule ambaye nilianza naye siyo ambaye nipo nae sasa na simpendi wala siwezi imagine yeye kunigusa kwa namna yoyote ile... Bado namuheshimu na nampa nafasi yake ya yeye kunikaribisha katika ulimwengu wa kupenda kama kichaa, kunikuzo toka kuwa binti na kukomaa kuwa mwanamke, na kunikomaza kwa kunivunja moyo wangu na kunifanya nitambue kuwa wanaume ni watamu kama walivyo wachungu hivyo kuniandaa kuwa nisishangae ikitokea tena.
Wito wangu kwa Broken hearts...
Kama you feel like crying... Cry all you can but iwe na kikomo. Kama mpenzi wako huyo alikupa furaha, mapenzi na amani kwa wakati fulani, shukuru kwa hilo lakini hakikisha kuwa unapoa na kumuona wa kawaida asitawale maisha yako kwa kufanya maamuzi kwa vigezo vyake.
Ni muhimu sana kuthamini kitu bila kujalisha kimekuumiza kiasi gani. Tena mwisho wa siku unaweza shangaa na kukuta wewe ndiyo source ya hayo mahusiano kuvunjika kama alivyo huyo mtu wako. Kauli za alikuwa hanifai kitu, hana maana, hatapata kama mimi... Kwangu huwa naona ni za kujifariji tu sababu mapenzi ni matokeo. Inaweza tokea wewe ama mwenzio akapata mtu bora ama bomu zaidi.
Umuhimu wa kuthamini penzi lililovunjika huja katika kukujenga inakuja pale mbapo unatathimini mtu wa kuwa nae tena. Muhimu tu kuwa mvumilivu na kutokuwa na haraka ya kuingia katika mahusiano tena... Ikiwezekana hata mwaka kama you can pull it off..