Nina mtazamo huu katika kuacha ama kuachwa kimapenzi... Na nazungumzia from my Personal experience.
Kwanza siwezi kabisa ingia katika mahusiano ya Mapenzi na mtu ambaye simpendi... Siwezi for the simple reason kuwa I can not imagine kufanya tendo la 6/6 na mtu ambaye sim'feel. Na ninapokuwa katika mahusiano naingia kwa miguu miwili yote, siwezi simamia mguu mmoja sababu sipendi kujiyumbisha ama kuyumbishwa. Hiyo inanifanya kuwa makini, mvumilivu, mstahimilivu na pengine hata ku apply hekima niwapo katika mahusiano ya Kimapenzi. Na namshukuru Mungu I have been lucky to have had Great men.
Pamoja na kuwa yule ambaye nilianza naye siyo ambaye nipo nae sasa na simpendi wala siwezi imagine yeye kunigusa kwa namna yoyote ile... Bado namuheshimu na nampa nafasi yake ya yeye kunikaribisha katika ulimwengu wa kupenda kama kichaa, kunikuzo toka kuwa binti na kukomaa kuwa mwanamke, na kunikomaza kwa kunivunja moyo wangu na kunifanya nitambue kuwa wanaume ni watamu kama walivyo wachungu hivyo kuniandaa kuwa nisishangae ikitokea tena.
Wito wangu kwa Broken hearts...
Kama you feel like crying... Cry all you can but iwe na kikomo. Kama mpenzi wako huyo alikupa furaha, mapenzi na amani kwa wakati fulani, shukuru kwa hilo lakini hakikisha kuwa unapoa na kumuona wa kawaida asitawale maisha yako kwa kufanya maamuzi kwa vigezo vyake.
Ni muhimu sana kuthamini kitu bila kujalisha kimekuumiza kiasi gani. Tena mwisho wa siku unaweza shangaa na kukuta wewe ndiyo source ya hayo mahusiano kuvunjika kama alivyo huyo mtu wako. Kauli za alikuwa hanifai kitu, hana maana, hatapata kama mimi... Kwangu huwa naona ni za kujifariji tu sababu mapenzi ni matokeo. Inaweza tokea wewe ama mwenzio akapata mtu bora ama bomu zaidi.
Umuhimu wa kuthamini penzi lililovunjika huja katika kukujenga inakuja pale mbapo unatathimini mtu wa kuwa nae tena. Muhimu tu kuwa mvumilivu na kutokuwa na haraka ya kuingia katika mahusiano tena... Ikiwezekana hata mwaka kama you can pull it off..