Je! Uko tayari kuoa au kuolewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je! Uko tayari kuoa au kuolewa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 13, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wana JF habari za Jumapili!natumain walio wengi wamekwenda kumwabudu Mungu(wakristo kanisani!) Basi sina Budi kushare maneno machache kutoka kwa mtumishi Christopher Mwakasege!


  Ni swali muhimu, uko tayari, maana yake umefika mahali hali yako ya ndani na nje, inakuruhusu kuoa au kuolewa? Uko tayari kuoa au kuolewa? Umefika mahali pa namna hiyo?. Wengine wanasema huyu ni mtoto, lakini unajua pamoja na kwamba ni mtoto, ni vizuri kujua kama uko tayari kiumri. Lakini ninapozungumzia hapa juu ya utayari wa kuoa au kuolewa, sizungumzii tu habari za miaka, bali ninazungumzia habari za hali yako ya ndani.
  Nimeona kuna mtu mwingine ana miaka arobaini, lakini kwa kweli hayuko tayari kukaa na mwanamke, ndani yake, mawazo yake na kufikiri kwake, hayuko tayari kukaa na mwanamke, hawajibiki hata yeye mwenyewe juu yake mwenyewe. Wengine hata wana miaka hamsini, lakini ana hali kama hii. Nimeona akinadada hata wana miaka arobaini na tano, hayuko tayari kuolewa, maana akiolewa ni shida tu.

  Nilienda mahali fulani, nikakuta dada ana umri mkubwa tu, lakini wakati wa maombi hakusema kama anataka tuombe ili aolewe. Nikaona ngoja nimuulize labda anaona aibu kusema hitaji hili kwa sababu umri umesogea, nikamwambia “hutaki tuombe uolewe”? Akasema, “hapana, sitaki kuolewa” (Na alikuwa ana umri wa miaka kama arobaini na zaidi). Nikamuuliza, “kwa nini”. Akasema, “kwa sababu sitaki kuomba ruhusa kwa mwanaume ninapotaka kutumika”. Nikamuuliza unafanya kazi, akasema, “ndio”.

  Nikamwambia, “unapokwenda kumtumikia Mungu huwa unafanyaje, - unaomba ruhusa au unatoroka huko kazini?” Akasema, “ninaomba ruhusa”. Nikwamwambia, “kwa nini unaona ni rahisi kuomba ruhusa kwa mwajiri wako na unaona taabu kuomba ruhusa kwa mume wako?” Alishindwa kujibu hilo swali. Nikamwambia tatizo lako ni kubwa kuliko unavyo fikiri.
  Unaweza ukaona kabisa ya kwamba, huyu mtu hayuko tayari kuolewa, wala msijaribu kumlazimisha aoelewe – pamoja na kwamba umri wake ni mkubwa. Usijaribu kumsukuma kwenye maamuzi ya kuolewa maana hayuko tayari kuolewa, akiingia kwenye ndoa atakwenda kuleta shida tu!
  Ndio maana ninakuuliza swali, je uko tayari kuoa au kuolewa? Lina vipengele vingi vya kulitazama, na linabadilisha vitu vingi sana.

  Mwingine unakuta ni msichana, wazazi wake ndio wanamtegemea karibu katika kila kitu. Mimi ninakuambia kabla hujafikiria kuoa au kuolewa, fikiria hilo swali. Kwa sababu ukiishaolewa tu biblia inakuambia wasahau watu wa nyumbani mwa wazazi wako (Zaburi 45:10). Sasa haimaanishi usiwasaidie, ila maana yake ni kwamba huwezi ukawasaidia tena ‘moja kwa moja’ kama ulivyokuwa unawasaidia zamani. Ni vitu lazima ujadiliane na mume wako juu ya kuwasaidia wazazi wenu wa pande zote mbili – maana mna mipango yenu sasa.

  Na inawezekana labda umeoa au umeolewa kwa kijana ambaye hana mzigo na wazazi wake kabisa, kila mtu anaishi kivyake vyake kama simba porini, suala la kusaidia wazazi hana ndani ya moyo wake. Wewe umekuwa na huo mzigo, wazazi wako wamekulea, umefika mahali umeanza kazi, sasa na wewe unawatunza hatua kwa hatua, siku unaolewa yule baba anasema basi usiwatunze tena, - fikiri hilo.

  Litakuwa linakuumiza kila siku jinsi wazazi wako wanavyopata shida. Utafika mahali utakuwa unachukua vitu kisiri siri unapeleka kwa wazazi, na hiyo ina shida yake pia. Kwa hiyo kabla hujakubali kusema mimi nataka kuolewa, fikiri kwanza na kuomba, maana ndoa inakwenda kukubadilishia mambo yako mengi.
   
 2. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa
   
 3. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja 50/
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,579
  Trophy Points: 280
  Mimi kama mwanangu Feisbuku.
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Umeniacha hewani ninaposoma habari hii nahisi kuna vitu sivipati sawasawa.
  Kwahiyo tusioe au kuolewa kama kuna vitu nyuma yetu.?
  Je basi mwanamuke asiyetaka kuolewa haoe na mwanaume asiyetaka kuoa haolewe kama inawezekana.?
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Thankx for sharing
   
 7. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  sina hakika kama nimeielewa barua yako
   
 8. S

  STEPHENMFUMYA Member

  #8
  Jun 12, 2013
  Joined: May 9, 2013
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AM FINDING GIRLFRIEND FROM ARUSHA, MOSHI, MANYARA OR TANGA, TEXT ME ON mfumyas@yahoo.co
   
Loading...