Je, Ukiwa upo vizuri kiuchumi na wanawake wengi wanazipenda hela zako, unaweza kupata mke Loyal kwa kujifanya masikini kama kwenye muvi za wanaijeria?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Ni kazi sana mwanamke kujuia na pesa za mwanaume labda awe ni mtoo wa kishua au ana kazi yake inamlipa fresh,

Hali hii imepelekea vijana wengi wenye pesa kutembea ama kuoa wanawake wanaojali pesa zao tu, na endapo kukawa kuna mtu mwenye pesa zaidi basi hawajiulizi mara mbili kukuacha ama kuchanganya wanaume bila wao kujua.... ni kama paka unaemlisha samaki kila siku ila ghafla pakawa hapaeleweki unamwekea ugali anaususa, kesho kutwa unamkuta yupo kwa jirani mwenye uwezo wa kumpa samaki na maziwa.

hali hii imefanya wengine wajaribu kuishi maisha ya kimaskini (huku biashara zao zikiendelea kuwaingizia vipato ama mishahara yao ikiendelea kuingia) ili wapate wanawake wanaowapenda kama walivyo na kuna muvi huwa zinatengenezwa kabisa... wengine hujifanya walinzi, wengine hujifanya wauza karanga mtaani, wengine hujifanya ma waiter, wengine hujifanya wafagiaji, n.k.

1659890630483.png

1659890658152.png

1659890699152.png
 
Dunia ya sasa stay inline kweny kipato chako mambo ya kuigiza kuwatafuta watu ubaya tu uje uachwe wakati una pesa usipende kupima imani utaumia.
Siku hizo pesa zikipotea ama apate mwengine anaekuzidi hela utafuahi 😂 😂
 
Ni kazi sana mwanamke kujuia na pesa za mwanaume labda awe ni mtoo wa kishua au ana kazi yake inamlipa fresh,

Hali hii imepelekea vijana wengi wenye pesa kutembea ama kuoa wanawake wanaojali pesa zao tu, na endapo kukawa kuna mtu mwenye pesa zaidi basi hawajiulizi mara mbili kukuacha ama kuchanganya wanaume bila wao kujua.... ni kama paka unaemlisha samaki kila siku ila ghafla pakawa hapaeleweki unamwekea ugali anaususa, kesho kutwa unamkuta yupo kwa jirani mwenye uwezo wa kumpa samaki na maziwa.

hali hii imefanya wengine wajaribu kuishi maisha ya kimaskini (huku biashara zao zikiendelea kuwaingizia vipato ama mishahara yao ikiendelea kuingia) ili wapate wanawake wanaowapenda kama walivyo na kuna muvi huwa zinatengenezwa kabisa... wengine hujifanya walinzi, wengine hujifanya wauza karanga mtaani, wengine hujifanya ma waiter, wengine hujifanya wafagiaji, n.k.

View attachment 2317294

View attachment 2317295

View attachment 2317296
FANYENI KAZI
 
Boss... weeeh cheza kama wewe. Kikubwa wanao. Mtoto wako hatakuacha kwa sababu kuna baba au mama tajiri zaidi. Iyo ingine, wachana nayo.
 
Kiukweli ukiwa na pesa kupata mapenzi ya kweli si rahisi, mara nyingi ni pesa ndio huwa inaongea, kule kujaliwa, kuthaminiwa, marafiki, ndugu weengi hujileta kwa ajili ya pesa.

Money talks wala si uongo
 
Tafta pesa mkeo ashindwe kuzimaliza
Afu sasa pesa ikiwa sio shida atakuambia humkazi vizuri...maaanake we kazi ni kutafta pesa tu. Kifuatacho pesa yako anapelekewa kijana kiungo mkabaji almaarufu kwa jina la Ngono Kante anayekufungulia geti kila ukitoka na kuingia home kwako. Kumbe ye umemfungulia maisha kila akitoka na kuingia chumbani kwako.
Hii maisha form ni wewe....tafuta pesa kwa ajili yako, sio ili upendwe. Pata dem kwa ajili yako, sio uonekane una dem.
 
Utasumbuka na kujitesa bure,akiamua kubadilika hawagi na sababu maalumu anabadilika tu.
 
Back
Top Bottom