Je Uhalisia ni you?

Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,036
592
Mwewe anapokuwa umbali juu, huweza kumwona panya chini.Inamaana panya huonekana mkubwa kwa macho ya mwewe, maana kwa macho ya binadamu asingeonekana.kama vipimo vya mwewe vingekuwa si kweli angemkosa huyo panya,kwa maana angesomba hewa.Swali ni kwamba kipimo halisi ni kipi?cha mwewe au cha binadamu?msaada please.
 
Mantiki ya swali lako sijaielewa. Fafanua zaidi ili nikumwagie nondo za kufa mtu.
 
Samahani Heading nimekosea,autocorrection imeweka neno you badala ya kipimo halisi au kwa maneno mengine,kipimo cha huyo panya cha kweli ni kipi?ni ninachokiona Mimi binadamu au anachokiona mwewe.futi ninayoiona Mimi je inaukubwa sawa na futi anayoiona mwewe?
 
Kabla ya yote kwanza ujue kuna tofauti ya muonekano wa picha kwa kiumbe kimoja mpaka kingine,

Hivyo inawezekana mwewe akawa anamuona panya(mnyama mwingine) kwa namna tofauti na wewe ndio maana anamditect kirahisi.mfano kinyonga anabadiri rangi kwa kufanana na eneo alilopo kujificha, lakini kuna wanyama wanamuona bila shida.

Hivyo si kipimo cha ukubwa ndio kinasababisha hili ila ni hivyo hapo juu.
 
Back
Top Bottom