Je, 'Uhalifu' nchini Tanzania 'umepungua' kama si 'kumalizika' kabisa hadi hawa 'Jamaa' wageukie huku ghafla?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
39,925
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa litaanza kuchukua hatua kwa wagombea wote ambao hawafuati ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jambo ambalo ni kosa kulingana na kanuni za maadili ya vyama vya siasa na uchaguzi.

Nipashe

Laiti Jeshi la Polisi nchini Tanzania lingekuwa na Umakini huu kwa 'Wanasiasa' dhidi ya 'Uhalifu' nchini huenda Tanzania yetu ingeshakuwa Salama.
 
Ed Kawiche

JF-Expert Member
May 28, 2020
497
1,000
sijakuelewa!
Tanzania ingekuwa salama kivipi?
inamaana Tanzania si nchi salama?
 
Cliffhanger

JF-Expert Member
May 22, 2018
640
1,000
Polisi wa nchi hii wanatia hasira. Juzi juzi vibaka wamefunga mtaa maeneo ya Mabibo Polisi wamejificha. Polisi wetu wame specialize kupambana na wanasiasa wa upinzani tu!!!
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,226
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa litaanza kuchukua hatua kwa wagombea wote ambao hawafuati ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jambo ambalo ni kosa kulingana na kanuni za maadili ya vyama vya siasa na uchaguzi.

Nipashe

Laiti Jeshi la Polisi nchini Tanzania lingekuwa na Umakini huu kwa 'Wanasiasa' dhidi ya 'Uhalifu' nchini huenda Tanzania yetu ingeshakuwa Salama.
😂😂😂😂😂😂

Mie nimemuuliza sabas anapanga kuchukua hatua gani dhidi ya mjumbe wa NEC Kassim Majaliwa ambaye anafanya kampeni za uraisi maeneo mbalimbali bila kuwepo kwenye ratiba ya Tume???

Nimeumia Sabas hajanijibu hadi saivi 😂😂
 
usinisogeze

Senior Member
May 6, 2017
191
250
Una uhakika kabisa tena wa 100% kuwa Tanzania ni Salama? Je, unaelewa kuwa neno 'Salama' na 'Usalama' ni 'Mtambuka' mno tu? Usinichoshe!!!
Brother fafanua usalama upi, maana sasa hivi wafanyabiashara wanafanya biashara zao hadi usiku wa Saa 3 na hatijasikia kuvamiwa. Labda utueleze wewe Tanzania sio salama kivipi, maana umeleta hoja isiyo na mashiko brother, au wewe inawezekana haupo Tanzania nini?
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
10,577
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa litaanza kuchukua hatua kwa wagombea wote ambao hawafuati ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jambo ambalo ni kosa kulingana na kanuni za maadili ya vyama vya siasa na uchaguzi.

Nipashe

Laiti Jeshi la Polisi nchini Tanzania lingekuwa na Umakini huu kwa 'Wanasiasa' dhidi ya 'Uhalifu' nchini huenda Tanzania yetu ingeshakuwa Salama.
Sasa hivi tunaelekeza nguvu zetu kuwapukutisha wahalifu wa kisiasa ambao ni maccm
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom