Je, tutumie Msiba wa Malkia kama darasa somo la Organization, Simplicity, Humility na Humbleness au tukomae na misafara yetu na ubosi wetu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Huku kwenye mitandao ya kijamii mjadala wa viongozi wetu kupandishwa basi moja ugenini jijini London, kwenye mazishi ya Malkia Elizabeth, imeendelea kushika kasi, hivyo hili ni bandiko la swali.

Je, tuutumie somo tulilolipata kwenye Msiba wa Queen Elizabeth kama Shamba Darasa la somo la Simplicity, Humility na Humbleness hivyo sasa viongozi wetu tubadilike kweli, tuwa simple, humble na humility ya kiukweli ukweli, au kwavile ile humbleness ya UK, Kupandishwa basi moja ni just a forced humility due to logistics issues and time management, lakini huku back home ambapo hatuna any logistical issues and we have all the time kufanya mambo yetu, sisi tuendelee kuvimba kwa u big boss na ma misafara mirefu kama kawa?

Nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kufuatia mchango wa member huyu kwenye bandiko hili Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden
nafikiri wengi hawajaelewa kinachofanya wabongo,Waafrika kushangazwa na kufurahi viongozi wao walivyolazimishwa kuwa "humble ndani ya kimbinyiko" Ipo hv,kama watu wale wale,wapo ulaya wamepandishwa basi,ishu ya usalama haikuwepo,inakuwaje huku bongo,Afrika,waziri,naibu waziri,mkurugenzi hawawezi kupanda gari moja hata kama wnatoka ofc moja kwenda eneo moja kufanya uzinduzi!?kila mtu anataka avimbe kwenye vieite yake!!!sasa ukija huku juu,PM,makamu,na Raisi misafsra yao huwa na magari zaidi ya 50!!hata kama wanaenda kuzindua choo!!
Sasa kitendo Cha wazungu kuwalazimisha hawa wajuba kukwea basi moja,bila kujali kuvimba kwao,kimetuthibitishia,kumbe ni wakawaida tu,hawana maajabu,ile misafara ya V8 100,huwa ni mbwembwe tu!!hakuna Cha usalama Wala nini,
Mnaosema kupanda mabasi ni kawaida,mbona bongo hawapandi mabasi?,badala ya kuwaita wananchi washamba,waulizeni hao vongozi wa Afrika
Naomba kuanza na kutoa angalia, kwanza sio kweli viongozi wa Africa wamedhalilishwa, na pili sio kweli viongozi wa Africa wamejifeel small!. Kuna baadhi ya viongozi wa Africa kiukweli wako very humble, na humbleness yao na humility yao ni natural nature yao, mmoja wa viongozi hao ni huyu mshuhudie HAPA

Huyu mtu yuko humble hata kabla hajaukwaa uongozi wa mkuu wa nchi, mshuhudie hapa na uangalie ni lini hili lilisemwa HAPA! hivyo kwa yeye kupanda basi la pamoja haimsumbui popote, tena mimi naamini ile window sit sio kwamba alijiwahia siti ya dirishani bali ilitokea tuu ameingia kwenye basi akajikalia tuu kumbe siti ikawa ni siti ya dirishani ambako kwa sisi akina kakamb.nani siti za dirishani ni za kugombania, hivyo mlipo muona mama pale mkadhani amegombea kuwahi siti ya dirishani!.

Kiukweli kuna events nyingi, watu wa ofisi moja wana attend event moja mahala pamoja na wote wakitoka ofisi moja na baada ya event wote wanarudi kazini mahali pamoja, lakini kwa vile kila mmoja ni boss, na kila mmoja ana Vieite lake na dereva wake na mafuta yake, kwanini kila mmoja asipande gari lake? Why share watu kubanana kwenye magari wakati magari magari yapo, mafuta yapo, madereva wapo?

Nilipoajiriwa na FCO ya UK na kupostiwa Dar es Salaam kama Mshauri wa Siasa wa Balozi wa UK pale Umoja House, Ubalozi una gari moja tuu CDM-1 kwa ajili ya balozi na ndilo lenye dereva maalum, magari mengine yote ni pool and shared. Wakati wa ziara za Bungeni Dodoma,. Ile CDM 1 inatangulia na dereva, mimi na balozi tuna fly, inakuja kutupokea Airport, tunapanda gari moja!. Mimi ndio nakaa siti ya mbele, balozi anakaa siti ya nyuma, vioo vya nyuma ni tinted, hivyo anayeonekana kutinga Bungeni na union jack ni mimi!. Hivyo baadhi ya wale waheshimiwa wetu wa vile vitu maalum kunidhania mimi ndio mnene!, na hivi nao ni binadamu tuu wana mahitaji ya kibinaadamu kama binaadamu wengine wowote, na sisi watu wa Kanda ile tulivyojaaliwa roho nzuri...

Kwenye saikolojia ya utajiri, ukoo wa kifalme wa Uingereza, ndio unaoongoza duniani kwa kuwa na hazina kubwa ya vito vya thamani, lakini huwezi kumuona malikia amevaa mi cheni, mi pate, na kutoboa matundu kibao ya masikio na kuvaa mihereni ya gold!, amekuwa akivaa simple!. Lakini nenda Uswazi, wana wanawake wa Uswazi, ambao walizaliwa masikini kisha wakapata uwezo, hivyo atavaa micheni, vidoleni mipete, masikioni matundu kibao ya hereni, ili kuonyeshea utajiri.

Vivyo hivyo, mtu aliyezaliwa kwenye familia tajiri yenye magari, kwake kutumia hata VW Beetle is not an issue, lakini wale masikini wenzangu na mimi, waliokwenda shule peku, na kutumia TZ 11, "akipata ma..ko hulia mbwata", mtu kama huyu akipata!, hufanya mambo ili watu waone!.

Sipingi misafara ya viongozi, lakini sometimes misafara hii inakuwa ni mirefu mno bila sababu za msingi!. Hili la misafara ya viongozi niliwahi kuizungumzia hapa Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Rais wa Marekani kila anaposafiri kwenye ziara za nje, anatumia ndege yake maalum iitwayo Air Force-1, japo inatajwa kama ni ndege moja, sio ndege moja, Air Force - ni set ya ndege 3 za Boeing 747 Jumbo Jet, moja ndio inambeba rais na waserekali, nyingine inawabeba waandishi na other people na ya tatu ni cargo ikibeba magari na vifaa!.

Sisi sasa tunayo ndege yetu ya Airbus, rais wetu akisafiri, asafiri na ujumbe mzito wa wafanyabiashara na sisi waandishi, ushauri huu niliusema ile siku Rais Samia amehutubia UNGA Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York alipozindua Royal Tour US, nikashauri tena Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Viongozi wetu, wanapopata ukubwa, wasijisikie sana na kuvimba vichwa, kupandisha mabega na kuanza kunata, hata simu zetu hawapokei wala sms hawajibu!, shuhudieni JPM alivyokuwa simple "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa! mfano mzuri ni baadhi ya wana jf wenzetu, walikuwa active humu when they were nobody!, walipopata uongozi na kuteuliwa uwaziri, humu jf wametuhama!, kisa madaraka!.

Kinachowafanya baadhi ya viongozi kufurahia ukubwa ni kitu kinachoitwa kujisikia, superiority complex! Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex! Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Hili la misafara ya viongozi, ikitokea viongozi wako ofisi moja, wanakwenda kwenye tukio moja, na wakimaliza wanarejea mahali pamoja, hakuna ubaya ma boss waki share usafiri.

Hitimisho:

Nimalizie kwa lile swali la msingi la mada hii.

Jee Tuutumie Msiba wa Queen kama Shamba Darasa la Somo la Organization, Simplicity, Humility na Humbleness?, Au Tukomae na Misafara Yetu na U-Boss? Nashauri tuutumie simplicity ya msiba huu utufundishe organization, humility kuwa simple na humble!

Paskali
 
Ndio na matumizi ya mavieite yaondoshwe, na misafara yenye kuhitaji tozo Ili iende barabarani, mbona UK imewezekana kwetu kunani🤔,Au siye matajiri kuliko hao mabeberu wasiona shida kuchoma pesa Kwa kununulia silaha Kwa ajili ya ukraine 🏃
 
Anko pasi umejipiindaa kuandika bandiko lakini lets be realistic.
1. Hawa jamaa wa siri-kali wengi wao hawajawahi kuwa humble EXCEPT wakiwa wanaomba kura. Charity begins at home, lakini kwa kias kikubwa wengi wao ni waongo.

2. Njaa njaa njaaa! Asilimia kubwa ya viojgozi wametoka kwenye njaa kali na huku serikalini walipaona kama sehem ya kupoza machungu na kujikusanyia mali. Hivyo ndo maana matumizi yao ni makubwa.

3. Inferiority complex n kubwa, wengi wa hawa wanaojiita watoto wa wakulima n kweli hawakuwahi kuona magari kwao so kuyapanda serikalini ni mojawapo ya njia zao za kuyazoea na kujimwambafy.

4. Watangulizi wao waliamini katika kuflaunt wealth na matumizi mabaya. So waliopo wanaiga tu. Waliopo nna uhakika walikua wanatamani sana kufuja hizi mali sasa walipopata nafas usitegemee wawe wazalendo. Waswahili wanasema, ukila nyama ya mtu huachi. Usitegemee watabadilika.

Mwisho: hakuna somo watakalojifunza, sasa hv ishu ni hot kwaio tutataftiwa kazengwe flani tusahau ili wao waendelee.

NB: Watu wanaosema usalama n.k, lets b real nchi ambayo threat ni panyarodi anaetumia silaha za jadi kama panga u think atakua sniper?
 
Hapo hakuna darasa, ilitokea tu kama ajali.

Nina mwanaume mwenzio nataka nimburuze mahakamani.

Nafanya je, ongea hapa hapa siyo siri, acha mjifunze
 
Ulimbukeni ndio tatizo letu kubwa, viongozi wetu wanaona sifa kuwa na misafara mirefu ya magari ya gharama yanayotumia mafuta mengi, na sioni kama wataweza kubadilisha tabia zao kwa urahisi, kwasababu hiyo kwao ni kama namna fulani ya kujitofautisha nasi watawaliwa.

Hawa washamba wetu, wameiga ile tabia ya mkoloni wakati akitutawala, ajabu mkoloni baada ya kurudi kwao hafanyi kama alivyokuwa akitufanyia sisi, lakini hawa jamaa zetu akili zao zimelala, wamekosa maarifa, wao ndio wanafanya yale aliyokuwa akitufanyia mkoloni, kwa maana nyingine wanatuambia wao ndio watawala wetu wa sasa, tunatakiwa tupate uhuru mwingine.
 
Brah Paskal huoni kama kuna baadhi ya watumishi posho zitakauka misafara ikipungua.Mpaka garage zile zinazojaza gesi za Air condition kama Makofia pale Ilala watakosa riziki.

Kuna mwanaharakati mmoja wa mazingira kule twitter alikuwa anauliza wale waheshimiwa wanaokimbiaga jogging huku gari la mkuu likitembea pale London walikuwa wapi.

Kutokana na uchumi wa dunia ulivyo hatuna budi kupunguza matumizi ikiwemo hilo la misafara na kufunga mabarabara hata Mwigulu kaongea bungeni.
 
  • Kiongozi anakuwa na msafara wa magari kama matone ya mvua, juu kuna chopa moja au mbili ILI KUWATISHA WANANCHI!
  • Kutukamua TOZO na wao kuishi kama wako peponi ni kujichumia laana. Ile habari ya tajiri na masikini kwenye Biblia itakuwa juu Yao.
 
Hivyo baadhi ya wale waheshimiwa wetu wa vile vitu maalum kunidhania mimi ndio mnene!, na hivi nao ni binadamu tuu wana mahitaji ya kibinaadamu kama binaadamu wengine wowote, na sisi watu wa Kanda ile tulivyojaaliwa roho nzuri...
Mzee wa kujipakulia minofu
 
Back
Top Bottom