Ground Zero
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 342
- 95
Wewe na taifa lako mnadhani mnanufaika vipi na kuwa na vazi la taifa, manufaa ambayo mngeyakosa kama msingalikuwa nayo?Angalia Avatar yangu utajuwa mimi ni kutoka Taifa gani.
Ni utambulisho wa Uraia wako. Kama mimi hilo ni vazi la taifa letu la Oman.
Angalia Avatar yangu utajuwa mimi ni kutoka Taifa gani.
u
Ni utambulisho wa Uraia wako. Kama mimi hilo ni vazi la taifa letu la Oman.
katika kitu ambayo naona serikali inapoteza nayo muda ni swala la vazi la kitaifa,kwanza ni swala ambalo hata hilo vazi likipatikana itakuwa ni kazi bure,leo hii na matatizo yote haya bado mtu eti ujivalishe vazi la taifa?likusaide nni?
umezani = umedhani
bule = bure
Watazame viongozi wa dini zote kuu Tanzania uone wanavaa nini. Halafu niambie hakuna wamasai humo?
Kama hujui namna ya Khanga zinavyoweza kuwa ushungi, tafuta avatar ya Mwali, umuone anavyopendeza.
chukua herufi za kwanza za makabila yote - tengeneza maumbo/maumbile! ama ngao mbalimbali za makabila! kitambaa murua kabisa!
halafu waachie ndugu wananchi waamue watafanyia nini vitambaa hivyo -- toa miaka mitatu. Ule mtindo utakaokuwa umebebwa na wengi - ndio vazi lenyewe hilo! Usasa/Ukale vyote vitachanganika humo! Ndio itakuwa hali halisi! halafu, hivyo vizazi vijavyo ndio vitakuwa vinaangalia historia yake.
tupe uzoefu wako kuhusu India n.k, wao mavazi yao yanatofautiana kulingana na hadhi? Pia kuhusu hayo magome ya miti kutoka bukoba hasahasa kiziba bado wana elimu hii..yatakubalika kwa hawa vijana wa mjini na hawa wawakilishi wetu(viongozi wapenda suti)? Pia hawa wadau watatumia mria mfumo wa kutuma meseji bure kupendekeza vazi/kitambaa..sasa mimi nina shaka kama waTanzania wa vijijini watashiriki kikamilifu..
kukubalika kwa vazi la taifa na kwenyewe ni shughuli tofauti na kuchagua! nadhani kwa sasa tukubali uhalisia wa mchakato huu - maana ulikuwa wazi kwa kitambolakini mkuu hadi sasa mchakato unaonekana kuanza na hauna uelekeo huo ulioutaja..labda utume meseji nyingi kadri utakavyoweza kuwabadilisha wahusika wakuu wa mchakato.
Mi ndio maana napendekeza Tanzania iingie kwenye maajabu saba mapya kabisa ya dunia.
Wewe pamoja na matatizo yote tuliyo nayo, watu kitu wanachoona cha maana ni kuunda kamati kutafuta vazi la taifa!
Halafu? Ina maana tukishapata hilo vazi ndio matatizo yetu ya elimu duni, uhaba wa madawa, miundombinu mibovu, ufisadi, umeme n.k yatakuwa yamekwisha? Hebu msinitie hasira..