Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
Je, vipaombele vyetu kama taifa viko wapi? Kwa nchi kama Tanzania je, ni muhimu kuwa na vazi la Taifa leo?
1. Badala ya kuunda tume ya kusaidia wakulima wa Pamba ili pamba yao iwe katika kiwango bora tunaunda tume ya kutafuta vazi la Taifa?
2. Wakati hadi sasa tunashindwa kuongeza thamani ya pamba yetu ili tuiuze kama mali ghafi nje leo tunaunda tume ya kutafuta vazi la taifa?
3. Badala ya kufufua viwanda vyetu vya nguo vilivyokufa, leo tunaunda tume ya kutafuta vazi la Taifa?
Hivi kama vazi hilo likipatikana ni kiwanda gani hapa nchini kitashona nguo hizo za vazi la Taifa, au tutaanza tena mchakato wa kutafuta mzabuni wa kutushonea vazi la Taifa, nchini China, India na Pakistani.
Halafu njoo kwenye wajumbe wa hiyo tume, tunajifunza nini kutoka kwao juu ya vazi hili la taifa, mbona tume imejaa wanahabari ni vigezo vipi vilivyo tumika?
Kweli kuna umuhimu wa kutafuta vazi la Taifa sasa?
===
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi ameitaka Kamati Maalum ya Kupendekeza Vazi la Taifa kutimiza wajibu wake ipasavyo ili kukamilisha mchakato huo kwa muda uliokusudiwa.
Akizungumza ofisi kwake jana wakati akizindua kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga, Waziri Nchimbi alisema hakukurupuka katika uteuzi wake wa wana kamati kwani alipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali.
"Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali, wajumbe mnayo kazi kubwa kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watanzania kile ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu,"alisema Nchimbi.
Alisema,"Vazi hilo likishapatikana mtasaidia kulitangaza ili wananchi walijue na lianze kutambulika rasmi kama nembo mbalimbali za Taifa,"alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Kusaga pamoja na kushukuru kwa kuteuliwa huko alisema kamati yake itafanya kazi hiyo kwa nguvu zote kuhakikisha vazi hilo linapatikana.
Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahsusi linalotambulisha utaifa wa Watanzania.
Mbali na Kusaga kamati hiyo inaundwa pia na Angela Ngowi (Katibu), Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absaloom Kibanda, Makwaiya Kuhenga na Ndesambuka Merinyo ambao ni wajumbe.
Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilianzisha mchakato wa kupata vazi la Taifa mwaka 2004 na mwaka huu wazo hilo limerudishwa tena.
Mwananchi