Je tunaamini kuwa Elimu ni ya bure Tz.

Sep 19, 2015
64
9
Ndugu zangu lazima tukubali kuwa elimu hii wapayo watoto wetu tunailipia kwa kodi zetu japo wengi hawajui hivyo,tulize mwanafunzi mmoja analipiwa na serikali shilingi ngapi kwa mwaka halafu piga hesabu je kwa mazao uliopeleka sokoni bidhaa ulizonunua ambazo zinatozwa kodi je hujalipia tusibweteke Elimu bure unakuta walimu wawili madasa saba wanafundishaje kazi kwetu.
 
Kwa hili ni sawa na kuhamisha fedha za kwenye kibubu na kuziweka kwenye Sox. Hakuna elimu bure duniani kote kwani fedha wanazopeleka mashuleni ini kodi zenu na ni fedha zenu. Serikali haina fedha zake yenyewe Bali fedha zetu walizozikata ndio wanazigawa. Waziri, watoto wetu hawana walimu wa sayansi hebu rudisha michango ya taaluma mashuleni itusaidie kukodisha ealimu. Au ndio mnataka watoto wafeli?
 
"Elimu bure" huu ni msemo ila katika utekelezaji ni ngumu mnoo. Ukiangalia ule mgawanyo wa hela zilizopokelewa mashulen unagundua huwez kuendesha shule kwa stail hiyo.
 
Katikat ya mwez wa kwanza nliomba ka leave kidgo nkaenda uchagani kuhesabiwa...sasa kuna shule ya msingi apo kijijin kwetu,sku iyo kukawa na kikao cha wazazi kujadili mapato na matumiz ya shule kwa mwaka huu....Cha kushangaza serikali ilikuwa imeleta TSH 82,000 ili zitumike kuendesha shule..hapo hapo ikikataza michango yyte,iwe ya mlinzi au ya chakula...mimi nlifkir HM anatania,nkajisogeza kwe ubao wa matangazo,asee nlishangaa sana kuona kweli ile ndo pesa iliyoletwa na imesainiwa na Afisa elimu na muhuri juu....nkabaki mdomo waz..
Sasa turudi kwe reaction ya wazazi sasa..Baada ya ilo tangazo wazazi walikuja juu kama mbogo,wakasepa huu ni ushenzi na hatuwezi kuuvumilia..sasa wakaamua ivi;,
Kila mzazi atachangia Debe moja la mahindi yaan kilo 20/25..na maharage kilo 5,pamoja na sh 4000,kwa ajili ya kulipia bili ya maji,mlinzi na mpishi ili watoto wao wale shule na wapate kusoma vizuri...
Wakamalizia kwamba,huyo magufuli akija,mwambie akutane na sisi wazazi ndo tumeamua hivyo na atupe sabab za kutuletea sh elf 82...kama so dharau ni kitu gani?
Shule tumeijenga siai na huu ndo utaratibu wetu wa kusomesha watoto wetu na huwa wanapata matokeo mazuri na hakuna mzazi anayelalamika kwa hili..
Kiukweli ukienda mkoa wa kilimanjaro kila shule wanafunzi wanakula shuleni na wanalishwa na wazazi sio serikali..
So huu mpango wa elimu bure ni kiuhalisia hautekelezeki,just kujitaftia sifa tu bas..
 
Ndugu zangu lazima tukubali kuwa elimu hii wapayo watoto wetu tunailipia kwa kodi zetu japo wengi hawajui hivyo,tulize mwanafunzi mmoja analipiwa na serikali shilingi ngapi kwa mwaka halafu piga hesabu je kwa mazao uliopeleka sokoni bidhaa ulizonunua ambazo zinatozwa kodi je hujalipia tusibweteke Elimu bure unakuta walimu wawili madasa saba wanafundishaje kazi kwetu.
"Elimu ya Tanzania sio bure, sema wamefuta Ada tu.. mbona watoto vifaa vyote vya mashuleni Tunanunua kwani haviko kwenye elimu?-Uongo wenye ukweli ni mtamu kuliko ukweli wenyewe.
 
Back
Top Bottom