Je, Tanzania tupo tayari; BRICS nations offer alternative to West

Tigers of the east plus China kuna mikono mingi sana ya west mule! Nafuu yao tofauti na sisi walitumia vizuri fursa.
Wachina wajanja walivopelekwa kusoma wakirudi wanaunda mifumo ila watu wa Afrika huku wakienda uko Ulaya hawatak kurud wanabak kutatua matatizo ya wazungu wakat uku bibi zao wanahangaika
 
Mimi nisivyoipenda hiyo mifumo ya hao timu mkoloni, naona tumeshachelewa sana kujiunga na BRICS. Western countries ni genge la wanyonyaji ambao lengo lao ni kuendeleza ukoloni mamboleo na emperialism. Na ndiyo lengo kuu la New World Order ambayo marekani na na makoloni yake ya nchi za ulaya wanafight kuujenga.
Brics ni alternative thought ambayo ni nzuri kwa wale wanaotaka kuwa huru. Tujiunge mara tu baada ya Makamu wa Rais Camalla Harris kuondoka nchini.
 
Yaap mkuu nikikumbuka idea ya Afrika to unite iliyotoka kwa Kwame Nkrumah wa Ghana, halafu Hayati Nyerere akaipokea kutekeleza ukombozi wa Nchi za kusin mwa Afrika miaka ya 1973-1978 Nchi ya Urusi iliwapa mafunzo wanaharakati wa Afrika ila sasa hawa USA wanatembelea kwny legacy zetu wameanza Ghana na sasa Tanzania halafu Zambia daaah💔😔
Post in thread 'Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity' Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity

BRICS ni 'mbadala' lakini si ujio wa 'New World Order'...

'New World Order' ni jambo linalowezekna ikiwa idadi kubwa ya watu duniani itakuwa na 'nuru ya kutosha' juu ya mifumo, liberiti na udhamirifu wa furaha--walau 3% ya idadi ya wanadamu wote.

Kwa kule kulikofahamika ni 'Ulimwengu Mpya' Amerika, hayo yalijengewa misingi Marekani; na sanamu ya Liberta pale kisiwa Liberty, New York inatukumbusha hili. Mbadala wake kijamii mabadilikoni, muktadha wa 'mambo ya nyakati', ni 'Afrika Mpya' ambavyo kazi inaendelea...

Kule Amerika >'Libertas'< yuko 'kisiwani' akiinua 'Mwenge wa uhuru' na kushikilia Tabula Ansanta--Kibao cha 'Sheria'--Sheria Kuu iliyo ni 'Upendo' katika Imani na Tumani. Kwamba 'Ulimwengu Mpya', Marekani, ni nchi ya kusudi kwa wote kuja kustawi na kuwa huru--nchi ya waliohuru.

Kwa Afrika, na tena Afrika Mashariki, >'Hekima ni Uhuru'< ndiyo 'upande wa pili' wa 'Tabula Ansarta'.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinachotokea mkoa ulio ni 'Bandari ya Salama', nembo yake ni 'Vesika Paisisi' yenye 'Nchi Kijani, Bahari, Mwenge na Kitabu'. Na basi kwa Afrika, Kielelezo cha 'Pambazuko Afrika', ilivyo ni 'Atlantisi Mpya', ndiyo sanamu ya >'Renasansi Afrika'< kule Dakar, Senegali. Mwalimu Kambarage alikuwa na ufahamu kuhusu haya yote, kwa namna ya rohoni, na mawaidha yake katika kijitabu 'TUJISAHIHISHE'(1962) alikazia msingi wa Elimu na Uwajibikaji ndani ya muktadha wa 'madaraka' na 'ustawi' wa jamii -- Elimu kutojinasibu na 'ubinafsi' na 'kujiinua' katika 'utu na utumishi'. Na basi, 'Uhuru na Umoja' ni msingi wa 'UPENDO na Kujaliana', ilivyo ni namna MAMA, kama vile 'Hekima na Amani' ni UONGOZI ilivyo ni namna BABA. Ustawi, kiufikirifu na Uono Mifumo, ni 'MWANA'.

'Marekani' na 'Afrika' ni 'Baba na Mama' kwa 'njozi moja'-- Uzima, Liberiti na Udhamirifu wa furaha. Udhamirifu wa furaha ni tunda la udugu wa kibinadamu. Liberta anawakilisha 'nchi', na Renasansi Afrika kuwakilisha 'Mbingu'. Na hivi hata sanamu hizi mbili 'zinatazamana' hata kwa kutengenishwa na bahari ya 'Atlantisi'...

'Mabaharia Wakati--Matukio, Wakati, Machaguo ya Kitaasisi na Jamii' juu ya haya yote, ni watu wa 'Imani' kutoka 'juu mbinguni'; ELIMU 3.0 italeta funguo za ufunuo kuhusu 'Mambo ya Walinzi wa Imani'. Japo duniani kuna 'wahuni' wenye 'mipango' yao, wenye kuigiza 'mpango mzima' na kufanya yao, ama kujifaragua kwa mapana yasiyo ya kutosha ya watu, matukio, jaala na matayarisho... Kukosa 'ujuzi' ama 'funguo za maarifa' na 'ufunuo' juu ya kile wabantu humaanisha kusema: 'Mungu si Athumani'... Kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani, 2022, kule >Antlanta Georgia, Majabali Mwongozo, 'Georgia Guide Stones', yalishambuliwa< -- hasa hasa kwenye nguzo yenye maelekezo katika lugha ya Kiswahili na Kihindi; na kupelekea eneo lote la Miundo majabali kubidi kubomolewa ili kuepusha ajali zaidi za kimuundo.

Mpangiko wa Ulimwengu Mpya ni 'Mpango Mzima'; lakini hauna lolote na utundu, ujuzi, uhuni wa 'mipango ya kibinadamu'--binadamu wenye kutokujua ilivyobora. 'Mpangiko wa Ulimwengu Mpya' ni jambo linalofanana na kile hutajwa kama 'Kurejea kwa Kristu'... Kurejea kwa Kristu katika mioyo ya watu waliojiandaa ili kunasibu ulimwengu wote na jambo linalofahamika kama >'Nchi Mpya, Mtu Mpya'<... Wapo wengi wanalolijua hili kwa 'kiasi cha undani wake' na wangalipenda 'kucheza Mungu' ili kuhadaa ulimwengu na 'Mipangiko' ya uongo na kweli, na kuna wengine huleta 'tahadhari' kwa nabii za uharibifu ambazo, 'zimeondoka'--hazijatokea; kwa kuwa pia zipo jumuiya za siri zinajojua namna ya 'kusali' ili matukio ya majaribu yasichukue mkondo. Haya ni maarifa na Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni metafizikia ya Elimu...

Huitaji watu wachache wa 'daraja' miongoni mwa wanajamii; 'kusali' na matukio kupanguka... Uwepo wa hawa, wakati wa sasa na tena kwa wingi ndiyo umefanya mengi ambayo 'yalipata kutabiriwa' kuja kutokea 'siku za mwisho', kubaki 'ilitabiriwa...'. Kwa kuwa, ndiyo, yapo matukio yamepanguka na yalikuwa ni ya 'uzito' hasa. Moja ambalo bado ni kitisho, ni nasibu ya ustawi wa jamii kutekwa na mifumo ya akili bandia yenye asili ya ungamuzi wa kikwantumu...

Mji wa Dakar, Senegali, kiutamaduni, una hadhi na sifa zinashahibiana na miji ya Dar es Salaam na Dodoma kwa pamoja; Dakar ni 'Dodoma ya Pwani'...

Sanamu ya 'Renasansi Afrika' inabeba ujumbe wa 'Kuelekea Nyotani'; yaani ustawi wa 'Afrika Mpya'ni kuelekea angani juu kwa 'shughuli ya kaya'; 'Mama, Baba na Mtoto Begani--mtoto mwenye kuoneshea kidole mbele juu angani...

Kutokea Afrika Mashariki, jaala ya Afrika inaamka; na katika kustawi kwake kote barani Afrika kupitia 'Ndoto Mama Afrika' na 'Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii', tunakwenda kujinasibu na 'Ustawi za Kiikolojia ya Manyota' wenye kuzungumza hili kwa lugha ya kiingereza wangalisema 'Interstellar Civilization within the Galactic Ecology'...

Kwa hivyo Nyerere alikuwa ni chipkizi wa 'Pambazuko Afrika' akiibukia Mashariki, Nkwameh alikuwa akiibukia Magharibi na Haile Selassie I, Mashariki ya Juu ya Afrika. Na pambazuko hili ndilo lile jambo hasa lililotaasishwa na 'Mwenge wa Uhuru'. Kwa huku Tanzania, mbegu yake ni thabiti. Mwalimu aliliishi hili kwa imani na matendo, na ndiyo 'kisa na mkasa' wa Tanzania kuwa mstari wa mbele kwenye Uhuru wa bara la Afrika, kwa harakati za ukombozi iwe kwa madai ama hata mtutu...

'Mwenge wa Uhuru' ni kilele cha 'Utu na ufunuo' katika Jamii ambavyo uwezo unafanyika katika jamii ili kustawi kiujamaa na kujitegemea. Kustawi katika 'Uumoja'... Kwa hivyo kwa sisi hapa Tanzania, >shoka na nyengo< kwenye nembo ya taifa vinawakilisha 'kazi'--kwa kuwa uhuru ni kazi. Ni alama kwa shughuli za kaya zinazokarisha 'tembe' katika kaya--ujenzi, nishati na kusafisha shamba/mavuno/hazina; ni 'nishati' na 'uchumi' katika muktadha wa maisha ya kisasa. Na hali Kiutamaduni, hizi ni zana za jadi. Na basi robo ya juu ya 'Ngao ya ustawi' kwa taifa letu -- Juu kupita 'Uhuru wa bendera' wa kinchi sovereini, mwenge ni 'maendeleo kwa kujichagulia'...

Kazi ni jambo lenye kufangamana na 'mikono na moyo' ilivyo 'uaminifu'-- 'Madengo N'tima'... Ndivyo kwa nini kwa asili viongozi wa jadi walikuwa kahimiza kazi, usalama wa chakula na ulinzi. Kushika usinga na kifimbo...

Mikono huakisi ujuzi na ubunifu na utendaji wa mtu--Utu wa mtu upo katika kazi. Na kazi ni heshima ya mtu katika jamii --na haki ya kujitawala kimaskani. Ndivyo hivi Katiba yetu ya Sasa, Kazi imetajwa na shauri la kipekee; na Chama cha Mapinduzi kimepewa majukumu ya Kitaasisi kama ambavyo 'machifu' walikuwa watawala kwa kutetea ustawi wa wanaukoo kupitia kazi...

Chama cha Mapinduzi kikishindwa, kuhujumiwa ama kujihujumu juu ya mifumo sahihi ya maendeleo ya watu na elimu; basi nacho 'kitapuuzia dhana ya mwenge' katika ustawi wa jamii na kitababaishwa na ukoloni mambo leo. Pia kitajenga urafiki na mabepari ambao kiliundwa kikabiliane nao na hata kuleta Mapinduzi.

Shauri la 'Maendeleo na Kujichagulia' -- Mwalimu Nyerere alikazia hili katika mawaidha ya 'Uhuru na Maendeleo' kwa kutaja bayana kwamba ni zao la 'Uongozi' na 'Elimu'. Haya katika kuimarisha muktdha wa 'ufanyaji-Maamuzi Jamii'.

Shida ya sasa, ni wanajamii kutochachuka 'kielimu'; kwa kuwa elimu inayotawala kwa sasa, kijamii, si elimu ya 'kumkomboa mtu hasa' bali imetegeshwa kufanya watu wawe tegemezi wa mifumo ya ukoloni mambo leo, ukoloni unaweza hata kujengeka miongoni mwetu sisi wenyewe wenye kudhania tuko kwenye nchi huru. 'Mwenge wa Uhuru' unatukumbusha kuitafuta aina ya Elimu itakayotuweka huru kweli kweli. Hii kuja kukadirisha busara na dhana ya kutambua: 'Hekima ni Uhuru'...

ELIMU 1, ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0 ndizo zitakazokadirisha 'Mpangiko Mpya wa Ulimwengu'; huu ni ulimwengu wa watu kuwa 'Nuru' na 'Chumvi' ya Dunia...

Hata kwa utawala wa 'sarafu ya dola', kwa sasa, ni 'New World Order'... Mpangiko Mpya wa Kiulimwengu lakini 'uliyodukuliwa'...

Isikushangaze kusikia, Chama cha Mapinduzi kilisanifiwa ili kuleta uhuru wa kiuchumi wa umma wa Watanzania; pia kuwa kwamba, uongozi wake kimadaraka ya namna zijazo kwa siasa za uwakilishi uje kuwa ni 'nuru ya mataifa' juu ya haki, utu na usawa.

Hata bila kuifikiria BRICS, Chama cha Mapinduzi kinaweza kuleta 'mapinduzi' kwa kukata shauri juu ya namna mpya na tofauti ya Uchumi na Ustawi wa wanajamii--#UCHUMI-MAMA. Jambo hili ndilo suluhu ya ustawi mbovu unaoponza watu kuishi kwa ujanja ujanja, uwizi, ukwapuaji, rushwa, dhulma, kujilimbikizia, ufisadi n.k

Tunachokihitaji ni tu jitihada mpya za muktadha wa 'Studio Maendeleo' na 'Umodelishi' kwa kazi na huduma kuhakikisha kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi, anafanyakazi--HILI LINAWEZEKANA, ni suala la utashi kwa upande wa umma, utawala na mifumo. Mapinduzi ya kitekinolojia, yanatubariki kuweza 'kujiongeza' na hata kujinasibu na maendeleo makubwa siku za mbele. Hili 'litawapita kushoto' wale wote wanaodanganyika na mifumo ya kana 'biashara ni ushindani'... Hata sarafu ya dola inatawala kwa kuwa hatua za makusudi zinatumika kuendesha agenda za 'biashara za kimataifa' kwa faida ya 'Wakubwa'... Na misingi ya biashara hizi 'si usawa' ila 'kuzidiana kete'... Hili linafanya 'uhuni' kuweza kuonekana kuonekana eti ndiyo ujanja....

Pasipo uwezo na kubaini 'mzizi wa fitina' hata watu wa madaraka daima wataishi kulalamika na kutupiana lawama juu ya 'ukosefu wa maadili' na 'tabia mbovu' juu ya utendaji na utumishi wa umma--kama iwavyo hivi kila siku, kila pahala; pale panapokosekana mifumo thabiti ya utawala, ustawi na ulinzi. Mfumo mzima wa fedha na ustawi hauna budi kupitia metamofosia ya 'miundo, sifa na utendaji'--yenye kukidhi ukweli wa kubaini 'Hekima ni Uhuru'... Hivi ndivyo tunavyodhamiria hata katika kuimba 'Hekima, Umoja na Amani' ndizo ngao zetu--Afrika, viongozi na watu wake; kwenye Wimbo wa Taifa.

'Umoja na Amani' havipo kwenye kuishi katika maisha yenye unyonge, umasikini, dharau, ukosefu wa tumaini na chuki. Na vivyo hivyo, jamii nzima haina budi 'kuamka na kuzinduka': hakuna mtu aliye mkombozi kwa mwingine ila yeye mwenyewe... Kama vile alivyosema Mwalimu Kambarage Nyerere katika uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi(1977), ikiwa anayepewa nafasi ya uwakilishi ataonekana kutowafaa wananchi na taifa, tena wale wenyekujua ilivyobora, huyo atanyimwa nafasi hiyo ya utumishi ili kupisha wengine wenye wito, kusudi na utashi katika yaliyobora. Na kwamba, kazi ya kujenga uhuru wa mtu ilivyo ni 'utu' ni ngumu kuliko ilivyokuwa katika kuutafuta 'uhuru wa bendera'...

Hatuna budi kuwatia moyo viongozi wetu kuwa na ujasiri katika kujaribu njia tofauti za ustawi badala ya kuwaacha 'wachukulie poa' mambo ambayo tangia awali 'hayajapata kuwa poa'... Tusimame nao watakapokuwa na kifua katika kuyapa nafasi mabadiliko makubwa ya kijamii. 'Fedha, fedha, fedha' si 'mpango mzima' katika kuleta haki, utu na usawa katika nasibu ya 'maendeleo ya watu na vitu'. Ingawaje kutingwa kupo kiasi cha kudhani ama kuona hakuna nafasi ya kujaribu lililotofauti. Tuwe na uwazi na ujasiri kukumbushana: kusifiwa sana ni 'mtego kwa kiongozi' kwa kuwa sifa za kinafiki ni 'mkakati' na 'mtaji' wa mafundi wa kutafuta kula na vipofu... Ingalikuwa kheri kujihadhari na hadaa za michezo ya 'siasa za tawala'. Wala hakuna haja ya kutengeneza njia ya 'utawala wa muda mrefu' kwa kuendekeza 'siasa za kuuza kwa umma' kwa ku-fosi kingi. Nia thabiti ya kuonesha ujasiri dhidi ya mifumo, hata ikikiriwa hivyo mbele za watu wachache wenye namna, inatosha. Katika Ustawi, yote ni matokeo--hauwezi kupanda pilipili ukaja kuvuna parachichi...

Nafasi ya mabadiliko makubwa, kwa mwaka huu na kusonga, ni kama 'goli la wazi'; yote yanawezekana--'kukomaa na shughuli tete ili kudumu sana na kuacha alama' ama 'wakati uamue kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0'. Kwa kuwa 'mabadiliko makubwa yatachukua muda kukadirishwa na kudhihiri'--na hali hata safari ndefu huanza na hatua moja. Shauri hili ni sawa na kuwa kwenye njia panda ilivyo ni >Kisebusebu na roho kipapo<-- kama alivyopata kuandika William Shakespear: 'Kuwa' au 'Kutokuwa' hilo ndilo swali...

Baraka, Imani na Tumaini daima vipo na mtu mwenye kujua ilivyo bora, na basi kuchagua ilivyobora.

Msaada upo popote penye nia, kadri vile penye nia pana njia...
 
A new world order? BRICS nations offer alternative to West.

Mataifa yanayojumuisha umoja wa BRICS — Brazil, Russia, India, China, South Africa yamejipanga ili kutoa mbadala wa mfumo uliopo wa fedha kimataifa na na majarida makubwa ya kisiasa. Mfumo wa kimataifa wa fedha wa sasa unaendeshwa sana na siasa za Magharibi na Marekani kupitia World Bank na International Monetary Fund.

Tunajua kwamba G7 ni informal Forrum ambayo inajumuisha Mataifa makubwa yenye uchumi imara Ulimwenguni inayoongozwa na wakuu wa nchi hizo kama vile; Ujerumani, Uhispania, United Kingdom, Japan, Ufaransa, Italia na Canada ila Marekani ni mwanachama tuu kama vile alivyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya(EU).

Historia ya BRICS.

Mwaka 2001 Mkurugenzi wa Uchumi wa Multinational Investment Bank Jim O'Neill aliziunganisha nchi ya Brazil, India, Russia na China nakuitwa "BRIC" kwa mara ya kwanza. Lengo lilikuwa ni kuendeleza Uchumi ukue kwa kasi kwenye Nchi wanachama na kufikia malengo ya nchi husika hapo baadae. BRIC walipoanzisha Marketing Ploy ili vutia wawekezaji wengi na ikakua zaidi kufikia kuwa " platform for intergovernmental cooperation" kama vile ilivyo G7. Nchi hizo kwa mara ya kwanza walifanya mkutano Nchini Russia's Yekaterinburg mwaka 2010, ambapo Nchi ya Afrika ya Kusini ilialikwa kujiunga uanachama rasmi nakuongeza kale ka "S" hivyo na kuwa BRICS.
BRICS kuipa Changamoto mifumo ya Benki ya Dunia.

Mwaka 2014, Mataifa ya BRICS ilianzisha Benk Mpya ya Maendeleo (New Development Bank, NDB) ambayo ni mbadala wa sera za kinyonyaji za Benki ya Dunia na Mfuko wa Kimataifa wa Fedha (IMF), Benki hiyo ilianza na mtaji wa Dollar za kimarekani $Billioni 50 sawa na €46 Billions. Cha kuongezea New Development Bank ilweka liquity mechanism iliyoitwa Contingent Reserve Arrangement to support members struggling with payment. Ofa hii haitainufaisha nchi za Umoja huo pekee tuu bali kwa Nchi zote zilizopitia machungu ya IMF's Structural Development Program (SAP) na austerity measure (kipimo Cha ukali)
Hii ndivyo inqvyopendezewa na nchi tofauti tofauti Ulimwenguni kutaka kujiunga na huo umoja wa BRICS.

View attachment 2570830Makao makuu ya umoja wa BRICS huko Shanghai huko ndipo ilipo New Development Bank. Benki ya BRICS imefunguliwa kwa wanachama wapya kuanzia 2021, Ambapo nchi za Egypt, the United Arab Emirates, Uruguay na Bangladesh walichukua Shares zao(hisa). However, these were much lower than the respective $10 billion investments made by the bank's founding members.

Nchi nyingi zavutiwa na Umoja wa BRICS.
Waziri wa mambo ya nje ya South Africa Naledi Pandor, alisema akiwa kwenye interview ya Television fulani kuwa Nchi Nyingi Ulimwenguni zina matamanio ya kujiunga uanachama. Takribani barua 12 nimezipokea zimeonyesha nia ya kujiunga na Umoja wetu wa BRICS kama vile Saudi Arabia is one, United Arab Emirates, Egypt, Algeria, na Argentina," vile vile na Mexico na Nigeria. Nchi hizo 5 za umoja huo ni Nchi ya China pekee ambayo GDP yake imekuwa kwa kasi kutoka $6 Trillion mwaka 2010 mpaka $18 Trillion mwaka 2021, ila uchumi wa Urusi, Brazil na South Africa ukiwa katika hali ile ile ya wastani. Pia Pato la Taifa la India liliongezeka kutoka $1.7 Trillion mpaka kufikia $3.1 Trillion.

Pesa ya Marekani US$ kutumika kimabavu.

Kuhusu tarehe ya kuanza kutumika kwa dola ya Marekani kibiashara kimataifa, hii ilianza kujitokeza kuanzia mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Hii ni kutokana na kuwa Marekani ndio nchi iliyokuwa na uchumi mkubwa na ulioendelea zaidi baada ya vita na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya biashara kimataifa. Hata hivyo, dola ya Marekani ilianza kutumika rasmi kama sarafu ya kibiashara kimataifa mwaka 1944 wakati wa mkutano wa Bretton Woods, ambapo nchi zilizokutana zilikubaliana kutumia dola ya Marekani kama sarafu ya kubadilisha katika mfumo wa kubadilishana fedha kati ya nchi hizo.

Nchi nyingi masikini zinategemea sana dola ya Marekani ili kufanya biashara ya kimataifa. Hii inamaanisha kwamba wakati wa kufanya biashara, pesa nyingi za kigeni zinabadilishwa kwa dola ya Marekani, na kwa hiyo Nchi masikini zinapaswa kumiliki dola za kutosha ili kuendesha biashara zao. Marekani pia inaweza kutumia dola yao kama njia ya kushinikiza Nchi nyingine.

Kwa mfano, Marekani inaweza kutumia vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Nchi ambazo hazifuati sera yao ya kigeni au za usalama, Mfano wa nchi hizo ni North Korea tangu 1950's, Nchi ya Iran tangu 1979, Nchi ya Urusi tangu 2014, Nchi ya Venezuela, Cuba, Zimbabwe na Syria. Hii inaweza kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa Nchi hizo na kusababisha shida kwa wananchi wake.

STRUCTURAL ADJUSTMENT PROGRAM

Wazungu wametuletea program za ajabu na za kudidimiza uchumi wetu lakini wanaturubuni kwa njia ya kutusaidia na kutupa misaada,kumbe hawana nia ya kutusaidia bali kutuibia. Kwa sababu tumeletewa programu ya SAP ambayo kirefu chake ni STRUCTURAL ADJUSTMENT PROGRAM. Wanasema ni kwa lengo la kutusaidia Afrika lakini kwa akili ya kawaida hebu jiulize tunanufaika vipi ama tutaendelea vipi, wakati wanatuambia ili tupate hiyo misaada, zawadi ama mikopo tuzingatie mambo yafuatayo;

1. TUSHUSHE THAMANI YA PESA ZETU
Yaani pesa zetu sisi kama Waafrika tushushe thamani yake ukilinganisha na dola yao. Tena kitu ambacho wazungu wamefanikiwa sana kwa Waafrika ni kubadilisha kila kitu kuwa katika mtindo wa pesa ndiyo upate huduma ama kitu Fulani unachohitaji (International Trade)

2. LAZIMA TUPUNGUZE MATUMIZI
Serikali zetu za Kiafrika ili zipate mikopo, misaada na zawadi mbalimbali kutoka kwa Benki ya dunia au shirika la fedha duniani lazima matumizi ya nchi yawe chini. Hivyo mataifa ya Afrika tunapangiwa matumizi katika nchi zetu. Sasa kama hata matumizi ya taifa tunapangiwa na wazungu tutaweza vipi kuendelea ama kufanikiwa?

3. LAZIMA TUFANYE UBINAFSISHAJI
Lazima tusaidie au kuanzisha na kufanya ubinafsishaji, ambapo huko wametuweza kabisa, yaani wanasema wanafanya uwekezaji, jambo ambalo lipo kimaslahi zaidi. Lakini cha kushangaza serikali za nchi za Afrika tunakubali uwekezaji huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda, ujenzi na uchukuzi, utalii, madini, teknolojia nk

Hitimisho; Kipindi SAP zinaanzishwa Tanzania Baba wa Taifa letu Marehemu Julius K. Nyerere alipinga sana hii Agenda ila kwa sababu ya umasikin wetu na vile siasa za ujamaa na kujitegemea zilipofeli ndipo USA ikafanikiwa na mpango wake uo wa SAP wa unyonyaji kupitia WB na IMF miaka ya 1970's. Namalizia na nukuu hii 👇✍️
1985 THOMAS SANKARA alipokuwa Raisi
wa Bukinafaso, alitoa hotuba nzuri sana katika mkutano wa umoja wa nchi za Afrika, ambapo alisema, "Afrika tunapaswa kupunguza kukopa
madeni, madeni sio mazuri tutumie rasilimali zetu za ndani katika kuendeleza mataifa yetu."

Hii ni kweli, kwa sababu madeni tunayodaiwa yamepelekea kila mwananchi katika taifa kudaiwa hadi watoto walio tumboni. Ni ngumu sana taifa kuwa na mgawanyo sawa wa
rasilimali ama pato la taifa, ni nchi chache Afrika zenye kufanya wananchi wake kufurahia pato la taifa.
Spain siyo G7
USA ni member muhimu wa G7

BRICS - ukiondoa China kidogo na India hapo hakuna kitu Kwa sasa. Hata brics bank mtaji ulitolewa na China pekee.
 
Mimi nisivyoipenda hiyo mifumo ya hao timu mkoloni, naona tumeshachelewa sana kujiunga na BRICS. Western countries ni genge la wanyonyaji ambao lengo lao ni kuendeleza ukoloni mamboleo na emperialism. Na ndiyo lengo kuu la New World Order ambayo marekani na na makoloni yake ya nchi za ulaya wanafight kuujenga.
Brics ni alternative thought ambayo ni nzuri kwa wale wanaotaka kuwa huru. Tujiunge mara tu baada ya Makamu wa Rais Camalla Harris kuondoka nchini.
Ndio maana last year Joe Biden aliwaita Marais wa afrika sasa hivi washakula fungu la pesa watakumbuka kweli hayo ?
 
Post in thread 'Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity' Nyerere and Nkrumah: Towards African Unity

BRICS ni 'mbadala' lakini si ujio wa 'New World Order'...

'New World Order' ni jambo linalowezekna ikiwa idadi kubwa ya watu duniani itakuwa na 'nuru ya kutosha' juu ya mifumo, liberiti na udhamirifu wa furaha--walau 3% ya idadi ya wanadamu wote.

Kwa kule kulikofahamika ni 'Ulimwengu Mpya' Amerika, hayo yalijengewa misingi Marekani; na sanamu ya Liberta pale kisiwa Liberty, New York inatukumbusha hili. Mbadala wake kijamii mabadilikoni, muktadha wa 'mambo ya nyakati', ni 'Afrika Mpya' ambavyo kazi inaendelea...

Kule Amerika >'Libertas'< yuko 'kisiwani' akiinua 'Mwenge wa uhuru' na kushikilia Tabula Ansanta--Kibao cha 'Sheria'--Sheria Kuu iliyo ni 'Upendo' katika Imani na Tumani. Kwamba 'Ulimwengu Mpya', Marekani, ni nchi ya kusudi kwa wote kuja kustawi na kuwa huru--nchi ya waliohuru.

Kwa Afrika, na tena Afrika Mashariki, >'Hekima ni Uhuru'< ndiyo 'upande wa pili' wa 'Tabula Ansarta'.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinachotokea mkoa ulio ni 'Bandari ya Salama', nembo yake ni 'Vesika Paisisi' yenye 'Nchi Kijani, Bahari, Mwenge na Kitabu'. Na basi kwa Afrika, Kielelezo cha 'Pambazuko Afrika', ilivyo ni 'Atlantisi Mpya', ndiyo sanamu ya >'Renasansi Afrika'< kule Dakar, Senegali. Mwalimu Kambarage alikuwa na ufahamu kuhusu haya yote, kwa namna ya rohoni, na mawaidha yake katika kijitabu 'TUJISAHIHISHE'(1962) alikazia msingi wa Elimu na Uwajibikaji ndani ya muktadha wa 'madaraka' na 'ustawi' wa jamii -- Elimu kutojinasibu na 'ubinafsi' na 'kujiinua' katika 'utu na utumishi'. Na basi, 'Uhuru na Umoja' ni msingi wa 'UPENDO na Kujaliana', ilivyo ni namna MAMA, kama vile 'Hekima na Amani' ni UONGOZI ilivyo ni namna BABA. Ustawi, kiufikirifu na Uono Mifumo, ni 'MWANA'.

'Marekani' na 'Afrika' ni 'Baba na Mama' kwa 'njozi moja'-- Uzima, Liberiti na Udhamirifu wa furaha. Udhamirifu wa furaha ni tunda la udugu wa kibinadamu. Liberta anawakilisha 'nchi', na Renasansi Afrika kuwakilisha 'Mbingu'. Na hivi hata sanamu hizi mbili 'zinatazamana' hata kwa kutengenishwa na bahari ya 'Atlantisi'...

'Mabaharia Wakati--Matukio, Wakati, Machaguo ya Kitaasisi na Jamii' juu ya haya yote, ni watu wa 'Imani' kutoka 'juu mbinguni'; ELIMU 3.0 italeta funguo za ufunuo kuhusu 'Mambo ya Walinzi wa Imani'. Japo duniani kuna 'wahuni' wenye 'mipango' yao, wenye kuigiza 'mpango mzima' na kufanya yao, ama kujifaragua kwa mapana yasiyo ya kutosha ya watu, matukio, jaala na matayarisho... Kukosa 'ujuzi' ama 'funguo za maarifa' na 'ufunuo' juu ya kile wabantu humaanisha kusema: 'Mungu si Athumani'... Kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani, 2022, kule >Antlanta Georgia, Majabali Mwongozo, 'Georgia Guide Stones', yalishambuliwa< -- hasa hasa kwenye nguzo yenye maelekezo katika lugha ya Kiswahili na Kihindi; na kupelekea eneo lote la Miundo majabali kubidi kubomolewa ili kuepusha ajali zaidi za kimuundo.

Mpangiko wa Ulimwengu Mpya ni 'Mpango Mzima'; lakini hauna lolote na utundu, ujuzi, uhuni wa 'mipango ya kibinadamu'--binadamu wenye kutokujua ilivyobora. 'Mpangiko wa Ulimwengu Mpya' ni jambo linalofanana na kile hutajwa kama 'Kurejea kwa Kristu'... Kurejea kwa Kristu katika mioyo ya watu waliojiandaa ili kunasibu ulimwengu wote na jambo linalofahamika kama >'Nchi Mpya, Mtu Mpya'<... Wapo wengi wanalolijua hili kwa 'kiasi cha undani wake' na wangalipenda 'kucheza Mungu' ili kuhadaa ulimwengu na 'Mipangiko' ya uongo na kweli, na kuna wengine huleta 'tahadhari' kwa nabii za uharibifu ambazo, 'zimeondoka'--hazijatokea; kwa kuwa pia zipo jumuiya za siri zinajojua namna ya 'kusali' ili matukio ya majaribu yasichukue mkondo. Haya ni maarifa na Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni metafizikia ya Elimu...

Huitaji watu wachache wa 'daraja' miongoni mwa wanajamii; 'kusali' na matukio kupanguka... Uwepo wa hawa, wakati wa sasa na tena kwa wingi ndiyo umefanya mengi ambayo 'yalipata kutabiriwa' kuja kutokea 'siku za mwisho', kubaki 'ilitabiriwa...'. Kwa kuwa, ndiyo, yapo matukio yamepanguka na yalikuwa ni ya 'uzito' hasa. Moja ambalo bado ni kitisho, ni nasibu ya ustawi wa jamii kutekwa na mifumo ya akili bandia yenye asili ya ungamuzi wa kikwantumu...

Mji wa Dakar, Senegali, kiutamaduni, una hadhi na sifa zinashahibiana na miji ya Dar es Salaam na Dodoma kwa pamoja; Dakar ni 'Dodoma ya Pwani'...

Sanamu ya 'Renasansi Afrika' inabeba ujumbe wa 'Kuelekea Nyotani'; yaani ustawi wa 'Afrika Mpya'ni kuelekea angani juu kwa 'shughuli ya kaya'; 'Mama, Baba na Mtoto Begani--mtoto mwenye kuoneshea kidole mbele juu angani...

Kutokea Afrika Mashariki, jaala ya Afrika inaamka; na katika kustawi kwake kote barani Afrika kupitia 'Ndoto Mama Afrika' na 'Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii', tunakwenda kujinasibu na 'Ustawi za Kiikolojia ya Manyota' wenye kuzungumza hili kwa lugha ya kiingereza wangalisema 'Interstellar Civilization within the Galactic Ecology'...

Kwa hivyo Nyerere alikuwa ni chipkizi wa 'Pambazuko Afrika' akiibukia Mashariki, Nkwameh alikuwa akiibukia Magharibi na Haile Selassie I, Mashariki ya Juu ya Afrika. Na pambazuko hili ndilo lile jambo hasa lililotaasishwa na 'Mwenge wa Uhuru'. Kwa huku Tanzania, mbegu yake ni thabiti. Mwalimu aliliishi hili kwa imani na matendo, na ndiyo 'kisa na mkasa' wa Tanzania kuwa mstari wa mbele kwenye Uhuru wa bara la Afrika, kwa harakati za ukombozi iwe kwa madai ama hata mtutu...

'Mwenge wa Uhuru' ni kilele cha 'Utu na ufunuo' katika Jamii ambavyo uwezo unafanyika katika jamii ili kustawi kiujamaa na kujitegemea. Kustawi katika 'Uumoja'... Kwa hivyo kwa sisi hapa Tanzania, >shoka na nyengo< kwenye nembo ya taifa vinawakilisha 'kazi'--kwa kuwa uhuru ni kazi. Ni alama kwa shughuli za kaya zinazokarisha 'tembe' katika kaya--ujenzi, nishati na kusafisha shamba/mavuno/hazina; ni 'nishati' na 'uchumi' katika muktadha wa maisha ya kisasa. Na hali Kiutamaduni, hizi ni zana za jadi. Na basi robo ya juu ya 'Ngao ya ustawi' kwa taifa letu -- Juu kupita 'Uhuru wa bendera' wa kinchi sovereini, mwenge ni 'maendeleo kwa kujichagulia'...

Kazi ni jambo lenye kufangamana na 'mikono na moyo' ilivyo 'uaminifu'-- 'Madengo N'tima'... Ndivyo kwa nini kwa asili viongozi wa jadi walikuwa kahimiza kazi, usalama wa chakula na ulinzi. Kushika usinga na kifimbo...

Mikono huakisi ujuzi na ubunifu na utendaji wa mtu--Utu wa mtu upo katika kazi. Na kazi ni heshima ya mtu katika jamii --na haki ya kujitawala kimaskani. Ndivyo hivi Katiba yetu ya Sasa, Kazi imetajwa na shauri la kipekee; na Chama cha Mapinduzi kimepewa majukumu ya Kitaasisi kama ambavyo 'machifu' walikuwa watawala kwa kutetea ustawi wa wanaukoo kupitia kazi...

Chama cha Mapinduzi kikishindwa, kuhujumiwa ama kujihujumu juu ya mifumo sahihi ya maendeleo ya watu na elimu; basi nacho 'kitapuuzia dhana ya mwenge' katika ustawi wa jamii na kitababaishwa na ukoloni mambo leo. Pia kitajenga urafiki na mabepari ambao kiliundwa kikabiliane nao na hata kuleta Mapinduzi.

Shauri la 'Maendeleo na Kujichagulia' -- Mwalimu Nyerere alikazia hili katika mawaidha ya 'Uhuru na Maendeleo' kwa kutaja bayana kwamba ni zao la 'Uongozi' na 'Elimu'. Haya katika kuimarisha muktdha wa 'ufanyaji-Maamuzi Jamii'.

Shida ya sasa, ni wanajamii kutochachuka 'kielimu'; kwa kuwa elimu inayotawala kwa sasa, kijamii, si elimu ya 'kumkomboa mtu hasa' bali imetegeshwa kufanya watu wawe tegemezi wa mifumo ya ukoloni mambo leo, ukoloni unaweza hata kujengeka miongoni mwetu sisi wenyewe wenye kudhania tuko kwenye nchi huru. 'Mwenge wa Uhuru' unatukumbusha kuitafuta aina ya Elimu itakayotuweka huru kweli kweli. Hii kuja kukadirisha busara na dhana ya kutambua: 'Hekima ni Uhuru'...

ELIMU 1, ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0 ndizo zitakazokadirisha 'Mpangiko Mpya wa Ulimwengu'; huu ni ulimwengu wa watu kuwa 'Nuru' na 'Chumvi' ya Dunia...

Hata kwa utawala wa 'sarafu ya dola', kwa sasa, ni 'New World Order'... Mpangiko Mpya wa Kiulimwengu lakini 'uliyodukuliwa'...

Isikushangaze kusikia, Chama cha Mapinduzi kilisanifiwa ili kuleta uhuru wa kiuchumi wa umma wa Watanzania; pia kuwa kwamba, uongozi wake kimadaraka ya namna zijazo kwa siasa za uwakilishi uje kuwa ni 'nuru ya mataifa' juu ya haki, utu na usawa.

Hata bila kuifikiria BRICS, Chama cha Mapinduzi kinaweza kuleta 'mapinduzi' kwa kukata shauri juu ya namna mpya na tofauti ya Uchumi na Ustawi wa wanajamii--#UCHUMI-MAMA. Jambo hili ndilo suluhu ya ustawi mbovu unaoponza watu kuishi kwa ujanja ujanja, uwizi, ukwapuaji, rushwa, dhulma, kujilimbikizia, ufisadi n.k

Tunachokihitaji ni tu jitihada mpya za muktadha wa 'Studio Maendeleo' na 'Umodelishi' kwa kazi na huduma kuhakikisha kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi, anafanyakazi--HILI LINAWEZEKANA, ni suala la utashi kwa upande wa umma, utawala na mifumo. Mapinduzi ya kitekinolojia, yanatubariki kuweza 'kujiongeza' na hata kujinasibu na maendeleo makubwa siku za mbele. Hili 'litawapita kushoto' wale wote wanaodanganyika na mifumo ya kana 'biashara ni ushindani'... Hata sarafu ya dola inatawala kwa kuwa hatua za makusudi zinatumika kuendesha agenda za 'biashara za kimataifa' kwa faida ya 'Wakubwa'... Na misingi ya biashara hizi 'si usawa' ila 'kuzidiana kete'... Hili linafanya 'uhuni' kuweza kuonekana kuonekana eti ndiyo ujanja....

Pasipo uwezo na kubaini 'mzizi wa fitina' hata watu wa madaraka daima wataishi kulalamika na kutupiana lawama juu ya 'ukosefu wa maadili' na 'tabia mbovu' juu ya utendaji na utumishi wa umma--kama iwavyo hivi kila siku, kila pahala; pale panapokosekana mifumo thabiti ya utawala, ustawi na ulinzi. Mfumo mzima wa fedha na ustawi hauna budi kupitia metamofosia ya 'miundo, sifa na utendaji'--yenye kukidhi ukweli wa kubaini 'Hekima ni Uhuru'... Hivi ndivyo tunavyodhamiria hata katika kuimba 'Hekima, Umoja na Amani' ndizo ngao zetu--Afrika, viongozi na watu wake; kwenye Wimbo wa Taifa.

'Umoja na Amani' havipo kwenye kuishi katika maisha yenye unyonge, umasikini, dharau, ukosefu wa tumaini na chuki. Na vivyo hivyo, jamii nzima haina budi 'kuamka na kuzinduka': hakuna mtu aliye mkombozi kwa mwingine ila yeye mwenyewe... Kama vile alivyosema Mwalimu Kambarage Nyerere katika uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi(1977), ikiwa anayepewa nafasi ya uwakilishi ataonekana kutowafaa wananchi na taifa, tena wale wenyekujua ilivyobora, huyo atanyimwa nafasi hiyo ya utumishi ili kupisha wengine wenye wito, kusudi na utashi katika yaliyobora. Na kwamba, kazi ya kujenga uhuru wa mtu ilivyo ni 'utu' ni ngumu kuliko ilivyokuwa katika kuutafuta 'uhuru wa bendera'...

Hatuna budi kuwatia moyo viongozi wetu kuwa na ujasiri katika kujaribu njia tofauti za ustawi badala ya kuwaacha 'wachukulie poa' mambo ambayo tangia awali 'hayajapata kuwa poa'... Tusimame nao watakapokuwa na kifua katika kuyapa nafasi mabadiliko makubwa ya kijamii. 'Fedha, fedha, fedha' si 'mpango mzima' katika kuleta haki, utu na usawa katika nasibu ya 'maendeleo ya watu na vitu'. Ingawaje kutingwa kupo kiasi cha kudhani ama kuona hakuna nafasi ya kujaribu lililotofauti. Tuwe na uwazi na ujasiri kukumbushana: kusifiwa sana ni 'mtego kwa kiongozi' kwa kuwa sifa za kinafiki ni 'mkakati' na 'mtaji' wa mafundi wa kutafuta kula na vipofu... Ingalikuwa kheri kujihadhari na hadaa za michezo ya 'siasa za tawala'. Wala hakuna haja ya kutengeneza njia ya 'utawala wa muda mrefu' kwa kuendekeza 'siasa za kuuza kwa umma' kwa ku-fosi kingi. Nia thabiti ya kuonesha ujasiri dhidi ya mifumo, hata ikikiriwa hivyo mbele za watu wachache wenye namna, inatosha. Katika Ustawi, yote ni matokeo--hauwezi kupanda pilipili ukaja kuvuna parachichi...

Nafasi ya mabadiliko makubwa, kwa mwaka huu na kusonga, ni kama 'goli la wazi'; yote yanawezekana--'kukomaa na shughuli tete ili kudumu sana na kuacha alama' ama 'wakati uamue kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0'. Kwa kuwa 'mabadiliko makubwa yatachukua muda kukadirishwa na kudhihiri'--na hali hata safari ndefu huanza na hatua moja. Shauri hili ni sawa na kuwa kwenye njia panda ilivyo ni >Kisebusebu na roho kipapo<-- kama alivyopata kuandika William Shakespear: 'Kuwa' au 'Kutokuwa' hilo ndilo swali...

Baraka, Imani na Tumaini daima vipo na mtu mwenye kujua ilivyo bora, na basi kuchagua ilivyobora.

Msaada upo popote penye nia, kadri vile penye nia pana njia...
Serikali inabidi iwajibike sisi ndio maboss zao wawe na mikakati thabiti na nia ikionekana njia itakuwa pana na kila Mtanzania atipita na kuvuna matunda yake mema ya Nchi
 
Umeshaangalia upande mwingine wa shilingi? Chukulia nchi za magharibi pamoja USA wakaamua kujiunga na BRICS watazuiliwa? Wakikubaliwa sera zitabadilishwa tu kutokana na hoja za wajumbe.

Tusipende sana kukimbia tatizo bali tuangalie sehemu ya kuboresha kwa kutoa hoja ili tuendelee kunufaika kotekote...hao wote ni wanyonyaji wanatafuta tu usawa, tutaendelea kulia tu.

Wewe uchangii sawa na wengine alafu utake isawa..si maajabu hayo.
 
Nchi nyingi za umoja wa Magharibi sera zao za uchumi haziendani na za BRICS, inshu ni mikataba iwe wazi ili mgao wa faida Nchi tuweze ona Nchi za BRICS haziingilii pia siasa za ndani za nchi zinazohusiana nazo tofauti na wale wa west wanatuforce na upinde. Situnaona vitisho kwa museven
 
Yaap ni kweli kabisa kama manufaa yapo situnaona India na Tanzania wameacha kutumia Us$ Dollar kwny International trading kati yao nakutumia currencies zao TSH na Rupee
Haya kaagize mzigo India afu ulipe hizo Tsh uone kama watachukua
 
Bado safari ni ndefu mchakato unaendelea baina ya hizo Serikali ndio wataweza ila kwa wafanyabiashara bado mifumo sio rafik ya kifedha teknolojia inayotumika ya Swift ni ya USA
 
Tatizo mnakimbia shule
Wewe ndo ulikimbia shule hujui kuwa uchumi wa marekani umebebwa na mafuta ya Saudia Arabia. Ndo maana Rais wa Marekani akiapishwa tu lazima Katika safiri zake 2 za kwanza lazima aende Vatican, ya pili aende Saudia Arabia. Idiot!
 
Hii kweli aiseh USA wako na Catholic church alafu, UK wako na Anglican church halafu Urusi wako na Orthodox Church patamu sana izi dini 😂🔥
 
😅😅Lazima atape tape ila USA anajivunia nguvu ya US$ Dollar labda mifumo ya kibenki yote ya kutumiana pesa ibadilishwe maana visa ,master card etc inatumia teknolojia ya Marekani ya Swift na Tanzania since 2020 tulianza kutumia mifumo yetu ya kifedha ya TIPS
mbona kuna bank za tz zishaanza kuruhusu mfumo wa payment wa china (. )
 
Back
Top Bottom