Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,513
- 113,638
Wanabodi,
Jumatatu ya leo, nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu, za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya leo nikihoji kuu umasikini wa Tanzania yetu na kupokea mikopo na misaada yenye masharti.
Naomba nianze kwa nukuu ya Mwalimu Nyerere kuwa "Umasikini mkubwa kabisa na mbaya kabisa, ni umasikini wa fikra" "poverty mentality"
Mwalimu akimaanisha kuwa umasikini mkubwa zaidi na mbaya zaidi, ni ukiwa na mawazo ya kimasikini.
Hivyo hoja kuwa Tanzania ni nchi masikini ni hoja muflisi kwa watu waliofilisika kimawazo, hivyo kitendo cha kuita nchi yetu kuwa nchi masikini, kunapalekea sisi kujisikia wanyonge.
Ukweli halisi kuhusu Tanzania, sio nchi masikini and has never been a poor county kwa sababu Tanzania ni nchi tajiri kwa utajiri mkubwa wa rasilimali za asili, madini, maliasli, mifugo, samaki, udongo wenye rutuba, vyanzo vya maji, vivutio vya utalii etc.
Kama Tanzania tuna utajiri wote huu, kwa nini nchi yetu bado ni masikini?. Naomba mimi nisilijibu swali hili, japo nakijua chanzo cha umasikini huu wa taifa letu, nisije nikachafua hali ya hewa ya bandiko hili.
Ndio maana, Rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli alipoingia tuu madarakani aliposema Tanzania sio masikini, Tanzania ni nchi tajiri na soon tutakuwa a Donner country wengi wetu tulimuunga mkono na kumpongeza.
Ila pamoja na utajiri wote huu tulionao ambao ndio unaotufanya Tanzania tuwe ni nchi tajiri, lakini Watanzania ni watu masikini wa kutupwa, wanaoishi kwenye umasikini uliotopea, wa kipato cha chini ya Dola kwa siku, na bajeti yetu a taifa, bado ni bajeti tegemezi inayowategemea wafadhili, misaada na mikopo, ya Mashirika yao ya misaada na mikopo, likiwemo Shirika la IMF na World Bank, kwa hiyo mwisho wa siku hutuamulia mambo yetu kupitia masharti ya mikopo na misaada yao.
CNN walipotangaza uongo huu,
CNN: Tanzania loses $300m World Bank loan amid crackdown concerns - JamiiForums
mimi ni miongoni mwa watu tulipinga na kushauri
Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tz tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu - JamiiForums
Hivi kweli Tanzania ni masikini ki hivi hadi tupokee mikopo ya masherti hivi, na masherti mengine ni ya udhalilishaji wa uhuru wetu na viongozi wetu?.
Namalizia kwa hili swali,
Jee Tanzania ni Masikini Hivi Hadi Tuendelee Kupokea Mikopo na Misaada Yenye Masharti Kwa Ajili Tuu ya Umasikini Wetu, Au Tufike Mahali Tuwe Masikini Jeuri, Tukatae?
Wasalaam
Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali

Kama hili ni kweli, pamoja na ukali wote ule rais Magufuli aliounyesha kwenye suala hili la mimba za mashuleni, halafu ni rais Magufuli yule yule aliyekuwa anafurahia msaada huu na masharti haya, hii inaonyesha, kumbe Tanzania pamoja na kuwa ni nchi huru, na tuna misimamo yetu, lakini mwamuzi wa mwisho kumbe sio sisi bali ni wenye kisu kikali kama ilivyo kwa mpiga zumari, kumbe nyimbo nyingine, hatuchagui sisi bali huchagua aliyemlipa mpiga zumari. Hivyo wanasiasa wa upinzani mliozuiliwa mikutano ya siasa, wakubwa wakiamua, mtashangaa mikutano inaruhusiwa.Sasa nimesikia juu huu kuwa huu mkopo wa WB, ambao mwanzo ulizuiliwa kwa hoja za kauli ya Rais Magufuli kuhusu kutosomesha watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, hatimaye sasa mkopo huu utatolewa kwa masharti ya kulazimisha mtoto wa kike atakaeshika ujauzito akiwa shule lazima aendelezwe baada ya kujifungua.
Kama shurti hili ni kweli ni miongoni mwa masharti ya ukopo huu, jee tuupokee tuu kumaanisha tumekubali masherti?.
Kama rais wetu aliishatoa msimamo kuwa "hatusomeshi kwa fedha za serikali, wasichana wanaopata mimba shuleni".
Na kwa vile nchi yetu ni masikini, tunakwenda kuomba mkopo wa WB kuboresha elimu, mtoa mkopo anatuwekea shurti la kusomesha mtoto wa kike anayepata ujauzito, jee tupokee tuu kwa vile ni masikini na hizo fedha tunashida nazo, au tuwagomee kwa kunyesha kuwa Tanzania japo kweli ni masikini, lakini, kwenye kutuingilia mambo yetu ya ndani, sisi ni masikini jeuri, jee tuupokee tuu na kujidhalilisha uhuru wetu mbele ya matajiri hawa, au tuwagomee na kulinda heshima yetu, pamoja na umasikini wetu wote, lakini tulinde uhuru wetu, na hata ikibidi nchi yetu, kujifanya kuwa kama "Kozi Mwana Mandanda, Kulala Njaa Kupenda".
Wakati wa Nyerere, baada ya Vita ya Kagera, mwaka 1879, Mwalimu Nyerere alitutangazia taifa "miezi 18 ya kukaza mikanda" hii ni miezi 18 ya shida na hali ngumu.
Tukaomba mikopo WB na IMF, wakatupa masherti magumu, Mwalimu alikataa kata kata, hivyo ile miezi 18 ya shida , badala ya kuwa miezi 18, ili extend kwa miaka 6, hadi 1985, Mwalimu Nyerere alipoamua kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, akaamua kuachia usukani, akaachia ngazi, akaghatuka na kumpisha rais Mwinyi, aliyekuja kuruhusu kila kitu, hivyo kuitwa Mzee wa Rukhsa".
Enzi hizo, kiukweli hali ilikuwa mbaya, hivyo kuilazimu kukubali kila kitu yakiwemo masherti hayo magumu.
Lakini kwa Tanzania ya leo, nchi ya uchumi wa gesi, tunaelekea Tanzania ya viwanda, tunaweza kujenga miradi mikubwa ya SGR, Stigler Gorge kwa fedha zetu wenyewe za ndani, tunaweza kununua ndege Dreamliner kwa cash money, jee tuna umasikini gani hadi tupokee mkopo wenye masharti yanayokwenda kinyume cha kauli ya kiongozi wetu?.
Hakafu kamkopo kwenyewe tunako nyanyasiwa na kudhalilishwa ni ka tu dola Milioni 300 tuu!. Hii ni pesa gani ya kuinyenyekea wakati juzi kati tuu, yule mzungu wa Canada, katuahidi kutupa bure bila masherti yoyote!.