Je, tabia iliyoibuka kipindi cha kubalehe, ndio upo nayo hadi sasa?

Je, tabia iliyoibuka kipindi cha kubalehe, ndio upo nayo hadi sasa?

Smile Digital Stationery

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2024
Posts
202
Reaction score
317
Muhali gani Wadau;

Kiukweli kila mmoja wetu humu na nje ya humu JF alishaipitia hii hatua ktk ukuaji wake, ndio kama ukaribisho wa kuingia kwenye utu uzima.

Kila mmoja ana style yake ambayo alibadilika kitabia, Wapo ambao balehe yao iliwatuma Ujeuri, Kiburi, Kujiamini kuliko kawaida, Ubabe, na wengine iliwatuma ngono, hapa nazungumzia kwa WANAUME.
***
Binafsi nakumbuka nlikuwa Darasa la 7 wakati hali hiyo inanikuta, Mimi haiba yangu ni mkimya/mpole. Ila nilijishangaa Nakuwa jeuri na mwenye kujiamini kuliko kawaida, nlikuwa nikitumwa jambo kama sijisikii kulifanya nasema kabisa SITAKI/SIENDI kauli ambazo awali sikuwa nathubutu kusema kwa wakubwa zangu. Nlikuwa naweza kuwakoromea ma broo na sister angu na nikiwatazama naona kama nawamudu jambo ambalo kiuhalisia sio kweli.

Nao nadhan kwakuwa walishapitia ile stage wakawa wananiona kama kituko tuu wananipuuza kunipa ushindi, nadhan walikuwa wanajua sio mimi yule ila ni Balehe😄.
Na nikweli, nilikuwa out of my mind!

Kwa upande wa ngono sikuwepo kabisaa wala kufikiria, yaani Waschana nlikuwa sipatani nao kabisaa, yaan ilikuwa ikiisha siku shuleni sijapelekwa Staff kuadhibiwa kwa kumpiga mschana ni bahati sana, ila cha ajabu ni kwamba nilikuwa na kismart cha kupendwa na Waschana mnoo ila wakati wanavutiwa na mimi wakinisogelea wanachezea mbata hadi wakawa wananiogopa.
***
Baada ya kuvuka ile hatua (Balehe) kuna baadhi ya mambo nilokuwa nayafanya najisemea "Hivi nilikutwa na nini?"

Binafsi baada ya kile kipindi kupita nilirudi katika asili yangu kitabia hadi sasa.

Nauliza, Wewe uliipita hatua ya kubalehe na tabia gani, na je hiyo tabia bado upo nayo hadi sasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom