Je, Sumatra imeshinikizwa na vigogo ili kuruhusu mabehewa mtumba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Sumatra imeshinikizwa na vigogo ili kuruhusu mabehewa mtumba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 22, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,481
  Trophy Points: 280
  Date::12/22/2008
  TRL ruksa kutumia mabehewa ya mtumba
  Jackson Odoyo
  Mwananchi

  HATIMAYE Kampuni ya MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeiruhusu Kampuni ya Reli (TRL) kuanza kutumia mabehewa yake 23 ya mitumba yaliyokodishwa kutoka Kampuni ya Reli ya India. Awali Sumatra waliizuia TRL kutumia mahehewa hayo kwa madai kwamba hayakuwa na obora unaotakiwa.

  Hata hivyo, meneja uhusiano wa TRL, Midrahji Meiz alisema jana kuwa Sumatra sasa imewaruhusu kuendelea kutumia mabehewa hayo baada ya vigezo vilivyokuwa vinahitajika kukamilika.

  “Tumesharuhusiwa na Sumatra kuanza kutumia mahehewa hayo na hivi sasa utaratibu unafanyika ili yanze kusafirisha abiria... baada ya utaratibu huo kukamilika tutatoa taarifa rasmi,” alisema Meiz na kuongeza: “Suala la usafiri wa treni ni suala la msingi kabisa na ndiyo maana tunajitahidi kuboresha usafiri huo kila wakati ili abiria wasafiri katika mazingira mazuri.”

  Mkurugenzi na mdhibiti wa reli wa Sumatra, Alfred Nalitolela alikiri kuwepo kwa suala hilo na kusema kuwa wameamua kuiruhusu TRL indelee kutumia mabehewa hayo kwa kuwa wamekamilisha marekebisho yaliyokuwa yanahitajika.

  “Tulibaini kwamba mabehewa hayo hayana ubora unaostahili kwa matumizi ya reli yetu, na moja ya vitu hivyo ni kiungio kati ya behewa moja na jingine, usambazi wa umeme ndani ya mabehewa, belling, spring, breki ya mkononi na magurudumu,” alisema Nalitolela na kuongeza:

  “Tulipokwenda India kukagua mabehewa hayo, tuliwaeleza wafanye vitu hivyo lakini wakaleta mabehewa kabla ya kukamilika kwake ndipo ikabidi tuwakataze kuyatumia mpaka wamalize kuyafanyia marekebisho hayo.”

  Alifafanua kwamba baada ya hapo walichukuwa moja ya kiungio cha mabehewa na kuyapeleka katika maabara ya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuyafanyia utafiti kama ni vifaa vipya na kuomba maelezo ya kina.

  “Unafahamu katika suala hili lile jumba la behewa ndilo linalotakiwa kuwa mtumba, lakini vifaa vyote vinavyofanya mabehewa hayo yafanye kazi vinatakiwa kuwa vipya, ikiwemo usambaji wa nyaya za umeme ndani ya behewa. Na hicho ndicho tunachokikagua na kukiangalia na kuhakikisha kwamba viko salama kila wakati,” alifafanua Nalitolela.
   
Loading...