Je, shetani/ibilisi anatoka koo zipi miongoni mwa koo za majini? Wazazi waliomzaa ni akina nani?

Hiyo ni according to your faith. ... ukienda kwa wa Buddha . Hindu. Wayahudi. .na,wao wana masimulizi yao tofauti yanayo husu imani zao
Kwani wewe unavyojua ibilisi historia yake ikoje?? Au unabisha bisha hovyo vitu usivyovijua?

Ibilisi ni jini ambaye alikuwa akiishi na malaika

sasa maswali yangu ndio nikayapanga kama ifuatavyo

1)Wazazi wake ni nani na nani?

2)Ndugu zake ni akina nani?

3)Anatokea katika aina/koo ipi ya majini?

4)Uzao wake ulianzaje anzaje?

5)Kama ikiwa binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adamu, je jini wa kwanza kuumbwa ni nani?
 
Kwanza ufahamu si majini wote ni waovu kipindi bado binadamu hajakuja duniani kulikuwa na majini wanaomuabudu mungu na majini ambao walikuwa wakimuasi mungu.

Soma hizi aya mbili
“ ‘I am better than him (Adam), You created me from fire, and him You created from clay’”

[al-A’raaf 7:12]

Hii aya inaonesha iblis ametengenezwa na mungu kutokana na moto (hajazaliwa)

“Will you then take him (Iblees) and his offspring as protectors and helpers rather than Me while they are enemies to you?”

[al-Kahf 18:50]

Hapa inaonesha Iblis ana watoto kama nimetafsiri vizuri,

Kama nilivyokuambia hapo juu kuna majini wema na wabaya hivyo iblis alikuwa kundi la majini mema na aliungana na malaika kupigana vita na majini wabaya (battle of good and evil) na malaika pamoja na iblis wakashinda na majini wabaya wakatokomezwa, baada ya vita iblis akitegemea ushindi wake atapata zawadi fulani amazing kama kupewa awe kiongozi wa dunia hivi ila Mwenyezi Mungu alikuwa na plan nyengine akamuumba adam, na kumpa uongozi wa dunia, hope stori inavyoendelea unaijua.
Hapa sijaelewa
Adam kaumbwa na udongo
Jini kaumbwa na moto
Malaika wameumbwa kwa nuru

Sasa naomba kueleweshwa
kabla hajaumbwa adam,majini yalikuwa yakiishi hapa duniani,walipomuasi Mungu,walitumiwa jeshi la malaika kuja kuwaangamiza na sifa za malaika tunaambiwa kuwa hawamuasi Mungu,sasa ilikuwaje wakamuasi Mungu kwa kutomuua ibilisi ? Je Ibilisi ndiye alikuwa pekee anayemuabudu mungu kuliko majini wengine na kama walikuwepo majini wengine waliuliwa au ilikuwaje mpaka akachukuliwa ibilisi tu.
Nalog off
 
Mkuu at that time ibilisi alikuwa Ni mchamungu, na alipokuja duniani alikuja as part ya jeshi la Mwenyezi mungu, Ibilisi hakuwa katika list ya majini waliotakiwa kuuliwa, Ila alishiriki kuwaua majini wengine, Na akili yake yote alijua kuwa akifanya vizuri kwa status yake atapewa yeye uongozi wa Dunia, hivyo mwenyezi mungu Alipomuumba Adam na kusema binadamu ndio wanapewa usimamizi wa Dunia, na akaambiwa amsujudie Adam ndio akaasi.
 
Ahsante mkuu
Nalog off
 
Kwa mujibu wa maandiko shetani alikuwa ni malaika mkuu uko mbinguni na alipewa nguvu nyingi sana na uwezo kiasi kwamba akatamani kuupindua ufalme wa Mungu na na yeye ndiye awe mfalme.

Baada ya shetani kulianzisha maandiko yanatueleza kwamba ilitokea vita kubwa sana uko mbinguni kati ya majeshi ya shetani na majeshi ya Mungu.

Baada ya vita Mungu alimshinda shetani hivyo akamtupa kuja duniani yeye pamoja na malaika wake waasi ambao ilikua ni theluthi nzima na alimuahidi hukumu yake itakuwa ni moto wa jehanamu.

Hivyo shetani anacho kifanya hivi sasa ni kuwadanganya watu watende maovu ili ule moto wa jehanamu asiungue mwenyewe.

Na ukumbuke kipindi shetani anatupwa uku duniani alitupwa akiwa na nguvu zake zile zile na ndio maana unaona ananguvu za kumshawishi binadamu kufuata matendo yake.

Note:shetani kipindi akiwa mbinguni alitambulika kwa jina la LUSIFA. jina la shetani limekuja baada ya kuhasi mbinguni.
 
Umejitaid
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom