Je, Serikali inaweza Kubinafsishwa? Kwanini Serikali yetu isibinafsishwe ili kuleta ufanisi kiutendaji?

Matangwa

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
641
1,061
Kuna wimbi kubwa la kubinafisishwa kwa Taasisi za serikali na mashirika ya umma ili kuleta ufanisi katika taasisi hizo. Mfano wa hivi karibuni ni Bandari yetu ya Dar es Salaam.

Hoja inayotolewa na wenye mamlaka ni kuongeza ufanisi wa bandari yetu ama kwa lugha rahisi ni kwamba serikali haiwez kusimamia na kuleta ufanisi wa kiwango bora kwa Taifa. Kwenye taasisi au mashirika ya umma

Hoja yangu ni kwamba uduni wa huduma hapa nchini upo kila wizara na sekta zote kuanzia huduma mbovu za Elimu kwenye shule za serikali, huduma duni kabisa kwenye Afya, huduma mbovu kwenye maji, umeme na mengine mengi kila huduma inayotolewa na serikali yetu ama ni ya kiwango duni au inatolewa kwa kuchelewa sana.

Kwa kifupi Serikali imeshindwa kuleta ufanisi sehemu yoyote inaposimamia au kutoa huduma. Swali ni Je, kama tunaami katika sekta binafsi na mambo ya ubia kwa nini serikali isibinafisishwe ili kuleta tija kwa taifa? Au isiwe ya ubia na sekta binafsi ili kuleta ufanisi wa huduma mbovu zinazotolewa na kusimamia na serikali?

Mfano wizara nzima ya habari na mawasiliana ibinafisishwe kwa Elon Musk, na wizara ya nishati tuwape Total Energies ya Ufaransa, wizara ya Ulinzi wapewe Wagner group ya urusi, m michezo na utamaduni tuwape Sport Pesa na wizara ya ujenz wakapewa CHICO ya China?

Tusijifiche kwenye masuala ya sera za nchi hilo tunawapa KPMJ company kutunga na kuendeleza sera za nchi.

johnthebaptist Pascal Mayalla
 
Mkuu agiza gongo baridiiiiiiiii nakuja kulipa 😂 umepiga kwenye mfupa kabisa hapo
 
Natamani tuibinafsishe kwa wananchi lakini siyo hawa wachukuaji waitwao wawekezaji au magabacholi. Natamani niwe rais wake ili nisweke ndani na kunyongelea mbali. Natamani niwe Magu mwingine hata wakinikolimba poa tu
 

Na tutabinafsisha kila kitu, kwasababu ya uzembe na kupeana kazi kwa kujuana.

Kama tunawaambia watu wale kadri ya urefu wa kamba zao, wale wasivimbiwe, utategemea kuona ufanisi na nidhamu kwenye utumishi wa Umma?

Mtu anaiba pesa hapa, ikigundulika anatolewa anapelekwa pale, utategemea nidhamu?

CAG anahaha kukagua na kuonesha uozo na wizi, hakuna hatua zozote zaidi ya kusemwa.

Tutashindwa hata kuongoza vyuo vikuu vyetu na tutavibinafsisha,
 
Tuwape waarabu kila kitu bhanaa, waja wa mtukufu mnyaazi, huku kwenye mikeka ya uteuzi dini ya mnyaazi nayo imezingatiwa......haya twende kazi.
 
Back
Top Bottom