Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,519
- 30,218
Kwa nchi yoyote yenye utawala Bora, inavitumia vyombo vya habari kama mhimili wao wa 4, usio rasmi, baada ya mihimili rasmi ya Serikali, Mahakama na Bunge, katika kuendesha nchi.
Huwa wanavitumia vyombo vya habari kama "watchdogs" vyao Kwa kuwa huwa wanakosoa, Ili serikali Ione mapungufu yake Ili ijirekebishe, katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Hali ni tofauti Sana hapa nchini kwetu, Kwa kuwa mihimili yote 3, yaani Serikali, Mahakama na Bunge, yote ni kama "imemezwa" na Mhimili wa Serikali, ambao ndiyo unaoelekea kuwa "umejichimbia" zaidi chini, hivyo kufanya mihimili mingine ya Bunge na Mahakama kutoweza kufurukuta!
Hata hivyo pamoja na mihimili hiyo 2 "kumezwa" na Mhimili mmoja, ambao ni Serikali, Bado hufanya Mhimili mwingine, usio rasmi, wa vyombo vya habari, kufanya kazi yake ya kukosoa Kwa weledi mkubwa, hivyo kuufanya Mhimili wa Serikali, kufanya kazi yake ikijirekebisha pale ilipokosolewa.
Hapa nchini kwetu, Mhimili wa Serikali, unachukua nafasi ya u-mungu-mtu, ambao hautaki kabisa kukosolewa na hivyo kufanya utawala Bora, kuwa kama hadithi tuuu ya alifu lela ulela!
Serikali inaweza kusema inatoa uhuru Kwa vyombo vya habari, pamoja na vile vya binafsi, kuwa huru, lakini "indirectly" uhuru huo wanauminya!
Kwa kuwa vyombo vya habari, hususani magazeti, hujiendesha Kwa kutumia matangazo ya biashara, na Serikali ikiwa ndiyo mtoaji mkubwa wa matangazo hayo, huweza "kuvipendelea" vyombo vya habari vinavyosifu sifu utawala huu wa CCM, Kwa kutumia lugha yao kuwa "Rais Samia anaupiga mwingi"na hivyo kutotoa matangazo hayo Kwa vyombo vya habari, ambavyo vinatekeleza wajibu wao kikamilifu wa kukosoa na hivyo kuvinyima matangazo hayo na hivyo kuvifanya vyombo hivyo vya habari binafsi, kutoweza ku-survive katika soko hilo.
Kwa Serikali kujifanya Iko 100 percent perfect, ndiko kunakoifanya ifanye figisu figisu hizo za kuvinyima fursa hiyo ya matangazo vyombo hivyo vya habari ambavyo viko "serious"
Hivi katika nchi kama yetu, ambayo imeweka mfumo wa kumfanya Rais wetu, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chake, kuwa kama mungu- mtu, ambaye ni binadamu, kutotoa nafasi ya kukosolewa, kunadhoofisha Sana mfumo wa utawala Bora.
Kwani vitabu vyote vya dini vinaamini kuwa ni Mungu pekee, ambaye yuko 💯 percent perfect, ambaye hapaswi kukosolewa.
Lakini sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na hivyo kutufanya kutumia njia ya kukosolewa kama njia ya kujirekebisha na hivyo kurudi kwenye msitari.
Ukiviacha vyombo vya habari vya mtandaoni kama Jamii forum, ambavyo uhuru wao wa kukosoa uko juu, vyombo vingine vya habari, kama vile magazeti, Televisheni na Radio, uhuru wao wa kutoa habari unathibitiwa na Serikali na upo chini Sana hapa nchini kwetu.
Dawa pekee na ya kudumu ni kupata Katiba mpya, ambayo itaweka mifumo imara ya kiuongozi wa nchi