Habari wadau.
Juzi kati nimepata simu ya Samsung E2222 au Samsung ch@t222 au Samsung ch@t222 GT-E2222 lakini kinachoniboa kila nikizama youtube kitu kinagoma au kinaniambia "Sorry,the file is unssuported"
Msaada wa ushauri wadau.
Hiyo simu ni 2G, (Edge) kwa spidi iliyonayo katika inaternet kamwe haiwezi kufungua video youtube ama popote, hata internet surfing yake ni POOOOR..
YouTube inakubali na 2g ymollel sema ni ile quality ya mwisho 144p
Cha muhimu awe na edge yenye speed kama ya Voda.
Ila Samsung haziruhusu kuplay video online hivyo utabidi uzidownload kwanza.
Download browser inaitwa ucbrowser then install kwenye simu halafu tumia website hizi kudownload video za YouTube.
Vuclip | Videos | Video Clips |
Tubidy Mobile Video Search Engine
Shukrani mkuu Chief-Mkwawa.
Hii simu imeniboa,kunikera na kuniudhi sana.Ilivyokaa kaa ki-high classic tena Samsung kampuni kubwa namba moja duniani nikajua yes,hobby yangu ya ku-stream itafika mahala pake,kumbe uzuri wa bure tu.
Hii simu imenikera sana.
Pumbavu Samsung ch@t222 GT-E2222.
hiyo simu nilishakuwa nayo na ninatumia voda tena nipo maeneo ya mjini kati. lakini hata surfing ilikuwa poor, kamera very poor, display poor . kwa kweli sikuwahi kufanikiwa kuplay video online. Lakini ni simu inayotunza charge vyema, ina mziki mzuri ukitumia headphones.
kama ulivyoshauriwa fanya kuuza ununue hata samsung trend lite. naona bei zinakaribiana