Je, Rais Samia anaelekea kuipata tuzo ya Mo Ibrahim?

mzeempili

JF-Expert Member
Aug 16, 2021
327
531
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kujipambanua kwa hatua mbalimbali nyingi zikikinzana na za mtangulizi wake.

Ninaamini atakuwa alijiwekea lengo la kuibuka mshindi siku zijazo za hii tuzo "lucrative" ya Mo Ibrahim. Endapo atashinda tuzo hii, Tanzania itaingia kwenye nafasi nzuri sana kidemokrasia na hali za maisha ya watu.

Ni jukumu letu sote kuendelea kumkumbusha pale atakapoonekana kukengeuka na kuacha roadmap ya kumpa tuzo hii. Mama anaweza
 
Hiyo tuzo itamsaidia nini Mtanzania wa kawaida?

Au hiyo "tuzo" ndiyo itaondoa tozo za hovyo hovyo zilizoanzishwa na Serikali yake?
 
Tuzo ya Mo Ibrahim hata siku moja haiwezi kunyakuliwa na Rais wa Tz kutoka Ccm. Take it from me.
 
Siku kutakapokuwa na tuzo ya kiongozi mwongo na mnafiki, lazima kiongozi wa Tanzania toka CCM ainyakue.
 
Kwani MO Ibrahim huwa anatoa tuzo kwa magaidi na madikteta?🤡🤡🤡
UHPIp.jpg
 
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kujipambanua kwa hatua mbalimbali nyingi zikikinzana na za mtangulizi wake.

Ninaamini atakuwa alijiwekea lengo la kuibuka mshindi siku zijazo za hii tuzo "lucrative" ya Mo Ibrahim. Endapo atashinda tuzo hii, Tanzania itaingia kwenye nafasi nzuri sana kidemokrasia na hali za maisha ya watu.

Ni jukumu letu sote kuendelea kumkumbusha pale atakapoonekana kukengeuka na kuacha roadmap ya kumpa tuzo hii. Mama anaweza
Sawa mzee Mpili tuombe kheri,ila katika eneo la ubambikiaji kesi,uonevu kwa wapinzani na democrasia ongeza juhudi kumkumbusha,vinginevyo Hadi sasa tayari nje ya hiyo road map.
 
Tuzo kwa mtu aliyeingia madarakani kwa kura za wizi?
 
Sawa mzee Mpili tuombe kheri,ila katika eneo la ubambikiaji kesi,uonevu kwa wapinzani na democrasia ongeza juhudi kumkumbusha,vinginevyo Hadi sasa tayari nje ya hiyo road map.
Tusaidiane kumpigia kelele pale penye mapungufu. Akikaa kwenye roadmap ni kwa faida yetu sote. Nchi ikiendelea ni furaha ya kila mtanzania.
 
Kwani MO Ibrahim huwa anatoa tuzo kwa magaidi na madikteta?
View attachment 1902638
Huyu Gado kazidisha chumvi.

Rais wetu tangu aingie madarakani sijasikia mtu katekwa au kauwawa na wasiojulikana au kaporwa pesa kwenye account kwa njia ya kubambikiza.

Kilichobaki tumkumbushe kuwa demokrasia nayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi. Huwezi kuzima sauti halali za wananchi halafu ukatarajia kupata ushirikiano wao katika kuleta maendeleo.

Pia tumkumbushe kuwa yeye ni rais wa watanzania wote. Siyo Rais wa CCM. CCM ni platform tu. Na ilipaswa anapokabidhiwa nchi, ajue anawajibika kufanyia kazi mahitaji ya wananchi wote. Hata wale wasiomkubali.

Mambo ya kukipigania chama awaachie wanaolipwa Lumumba. Rais analipwa kwa kodi ya watanxania wote. Siyo haki akakifanyia kazi chama kimoja badala ya nchi yote. Akiona ni vigumu aache makazi ya Ikulu ya wananchi wote, aache magari yetu, aache vyote ahamie Lumumba, akalipwe na CCM.
 
Kilichobaki tumkumbushe kuwa demokrasia nayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi. Huwezi kuzima sauti halali za wananchi halafu ukatarajia kupata ushirikiano wao katika kuleta maendeleo.
Kiongozi anaezima demokrasia ndiye dikteta mwenyewe huyo.Kuzima demokrasia ndiyo definition yenyewe ya udikteta.
 
Back
Top Bottom