Hakuna Rais wa Tanzania anayeweza kushinda Tuzo ya Mo Ibrahim

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Habari wana jamvi,

Nimetafakari mambo mengi kisiasa, mwisho nimeridhika kuwa hakuna Rais wa Tanzania awezaye kushinda Tuzo ya Mo Ibrahim.

Nimefikiria mambo anayo fanya Rais Samia, utadhani ameshahakikishiwa kwamba 2025 hatoboi. Anauza rasilimali za Nchi kwa bei chee, lakini za chini chini ni kwamba kajiwekea kibindoni mkwanja wa maana sana. Hii ni roho ya kikatili sana kwa Nchi yetu. Hana sifa hata moja ya kupata Tuzo ya Mo Ibrahim.

Mtazame Kikwete, hata kuliingiza jina lake miongoni mwa washindanishwaji hata shetani anasema "Huyu hapana".

Kwa tamaa ya fedha ndiye aliye haribu mradi wa gesi ya Mtwara. Undani wa jambo hili yeye anajua.

Ndio maana Magufuli alipojua baadhi ya machafu yake alichukia sana.

Itoshe tu kusema kwa hii kinga ambayo Rais amewekewa ya kutokushitakiwa, hawa viongozi wanaona ni fursa kwao ya kujilimbikizia mali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom