Nimemsikiliza speeches zake hasa kwa polisi akiwaambiwa ukweli juu ya waliyotaka kumfanyia baadae wakagundua ni nani wanaomba msamaha na kutubu ,ni miaka hiyo akiwa anafanya kazi katika asasi za kibinafsi huko alikotokea.
Niliwahi kuhakikishiwa kuwa pure civilian hawezi kuwa CIC na ndio sababu Samia ameweza na ndio sababu ya zile top 5 za wakati wote za CCM inamaanisha kuwa lazima wale jamaa wakukubali sana .
Kama umekuwa potential hata ukiwa na miaka 30+ watakupa mafunzo ya muda ili uendane na kasi ya kuchambua data kisawasawa sio kiraia.
Je huku jamiiforumu kuna wadau walau wanamfahamu mama akiwa kitenge kama field officer au agent wa TISS akiwa foreign affairs au kokote
Raisi Samia si zao la TISS ila ni zao la CCM tangu ngazi za chini kwa malengo maalum.
Ni mmoja wa watu ambao wamepaliliwa kwa malengo maalum ndani ya CCM na humu JF ipo picha yake akiwa ndani ya kikao cha CC miaka ya zamani.
Hata huko nje ni katika ile twasema "nenda upate "exposure" na wakufahamu" unanielewa hapa? Kamala Harris ni mfano wa watu ambao amefurahishwa na raisi Samia kiasi cha kutaka kuja Tanzania "for a chart" na kutaka more investimate opportunities.
Hivyo hapo polisi kama kawaida hata ukivaa uzuri tu hukuogopa kwamba labda weye ni walewale lakini kwa raisi Samia pengine aliwaambia na kuwaonyesha kuwa yeye ni nani nchi hii kwa upande wa CCM na pengine ilibidi afanye hivyo kulingana na aina ya "issue" ilokuwepo.
Yawezekana pia simu ilipigwa kwa (jina kapuni) na akasema "nyie vijana ebu mwachieni huyo ni dada yangu" na vijana walipoona ni sauti ya yule au hata ya wasaidizi wake (jina kapuni ) wakatahayari na kuomba radhi.
Hivyo ndani ya CCM ukiwaweka raisi Samia na hayati JPM , raisi Samia ni "insider" na hayati JPM alikuwa ni "outsider" na hapo utaona nani ana "backup" kubwa ya "support" ya wenye chama na kubwa zaidi kutoka kwa JK na ndo maana anamwamini kwa ushauri.
Kuna kitu watu wengi washindwa kukielewa ni uhusiano wa raisi Samia na JK. Uhusiano huu ni kwa sababu JK alimteua raisi Samia kuwa waziri katika serikali ya Muungano mwaka 2010 aliposhinda uchaguzi na kumuona kuwa huyu afaa zaidi hata kwa huko mbele.
Serikali ya mzee Karume ilikuwa na mawaziri wengi wanaume na raisi Samia wakati huo alikuwa ni mwanamke pekee na hiyo kwa wale tuangaliao kwa undani twaona kwamba ilikuwa ni aina fulani ya kubinya nafasi kwa wanawake na raisi Samia alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na ndilo alolibeba leo.
Kwa Tanzania TISS ipo nusunusu yaani nusu kazikazi (kwa maana ya kuhakikisha usalama wa nchi upo sawa) na nusu ni kufungwa mikono kwa nyuma (hands tide behind on their back) kwa yale mambo ya ajabu ambayo twayasikia sasa hivi yakiendelea yaani kuangalia tu nchi ikiharibiwa na wasiwe na uwezo wa kufanya chochote.