Je, Rais Magufuli hakuyaona haya alipokuwa mbunge/waziri?

Nimekuelewa sana tu, uko katika kuwafunda walio katika nafasi za maamuzi. Lakini kuna ukweli ambao hutaki kukiri nao ni JPM asinge weza kufanya haya anayofanya sasa kama Rais wakati akiwa Mbunge na waziri. Sanasana angejiuzulu pengine akarudi kwao kulima ngombe na hata asingekuwa Rais leo hii. Na asinge fanya haya afanyao kama Rais maana si Rais.

Na washawasha!

Umeelewa nnachisema mkuu?? Nani kasema sipendi hatua zinazokuliwa?

Point yangu waache unafiki na wanapoona ujinga wasikae kimya na kupiga makofi tu bungeni! Thats my point mkuu!!
 
Mkuu naomba nikupe elimu kidogo. Position ya mtu katika eneo fulan ndio inayomuwezesha kufanya maamuzi na siyo yeye. Nikupe mfano mdogo tu. Upinzani wameanza zaman kushinikiza kuwekwa wazi kwa mikataba ya wawekezaji na siyo ya madini tu, ya uwekezaji wowote. Ila mpaka kesho hakuna kitu kama hiko kilichofanyika na wanaendelea kuonge. Kwanini ? Hawana total jurisdiction ya kufanya hivyo. Hawapo katika position ya kufanya hivyo either kwa mmoja mmoja au upinzani wote kwa ujumla. Magufuli naye alikuwa mbunge na waziri, haimaanishi alikuwa anapenda yanayotokea na tisimsemee hilo ni swala binafsi ila tu alikua hana nguvu na hakua katika nafasi ya kuifanya sauti yake au maoni yake yawe vitendo. Raisi ni nafasi ya juu zaidi ulimwenguni pote na ana mamlaka makubwa mno. Ana uwezo wa kuyabadili maneno yake kuwa vitendo pasipo na kuzuiwa. JPM akiwa waziri na JPM akiwa mbunge ni tofauti kabisa na JPM akiwa raisi. Ukishayaelewa hayo ndo utajua kwamba hata angeongea mpaka apasuke katika nafasi yake ya ubunge au uwaziri asingebadili chochote as long as aliyekuwa amekalia kiti alikuwa na mipango mingine. Tambueni Uraisi ni nafasi ya Juu zaidi duniani... Marekani na demokrasia yake, pamoja na wananchi wengi kumpnga trump... trump ndo raisi wao .. na anafata misingi na sera zake.. ana nguvu kubwa
....anadiriki kupga chin program zilizoanzishwa na raisi aliyepta na anafanikiwa . Yupo katika position ya kuyafanya hayo. ASILAUMIWE JPM HATA KIDOGO. AUNGWE MKONO NA AOMBEWE KAMA ANAVYODAI.

Kuyaelewa haya uliyoyaandika....anatakiwa ajivue joho la mahaba....
 
Ndugu Magufuli aliruhusu vipi....!??
Akiwa kama waziri wa nishati na madini au kama mbunge au akiwa kama mwanasheria mkuu wa serikali....!!??

Una maanisha Magufuli ndio alikuwa mtu wa mwisho kusaini hiyo mikataba...!!?
Tunajua akina zito na mnyika walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii mikataba! Je uliwahi kumuona magufuli akiipinga bungeni?

Kama hukuwahi je huu sio undumilakuwili??
 
North Korea kamtunishia US na mambo shwari kabisa. Hivi unadhani mboga inahitaji chumvi kiasi gani mkuu!
Tatizo watu wanaona mambo yanatokea kama ambavyo hawajazoea na hawadhani kama ingekuwa hivyo. Thats is too bad. Fear is an Evil.
 
Sintanyamaza kuona huu usanii wenu wa kujidai mnauchungu wa nchi wakati matatizo mmeleta nyie wenyewe!!
Sawa kamanda, ingia ulingoni sio uko bize kwenye mitandao humu, unakuwa hauna impact! Nimependa "uzalendo" wako ila unachemka kusema kwa nini JPM hakuzuia wasisaini.
 
Mkuu, kwa maelezo ya mashabiki wa CCM ni kuwa huyo "fisadi" aliyeko CHADEMA (Lowasa) na Magufuli ni dugu moja. Kumbuka ile siku Magufuli alipodai kutokewa na muujiza wa kushikana mkono na Lowasa! Wewe vuta subira tu; utauona ukweli kuwa CCM ni ileile.
Ni ndugu moja? Je naye magufuli unataka sema ni fisadi??

Unaposema lowassa ni fisadi kwanini asichukuliwe hatua jibu swali!!
 
Tunajua akina zito na mnyika walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii mikataba! Je uliwahi kumuona magufuli akiipinga bungeni?

Kama hukuwahi je huu sio undumilakuwili??

Kama hiyo ndiyo tafsiri ya undumilakuwili basi wanasiasa wote hapa nchini ni mandumilakuwili......
 
Sawa kamanda, ingia ulingoni sio uko bize kwenye mitandao humu, unakuwa hauna impact! Nimependa "uzalendo" wako ila unachemka kusema kwa nini JPM hakuzuia wasisaini.
Mkuu hata kama watu 100 wangesema yes yeye akasema no tungemuelewa...huu ni usanii
 
Hili jibu nililitarajia sana!! Kwahiyo unamaanisha magufuli ni muoga??? Hata kama aliogopa kwanini hakusema ukweli ili aokoe nchi kama kweli alikua na nia hiyo??

Okey kama aliogopa ina maana ni muoga...so akija trump akamwambia nataka nchi then atampa kwasababu anaogopa wakubwa??
Point yako ni nini sasa? Mbona unarukaruka kama chura?
 
Kwahiyo unakubali kwamba alikubali mikataba mibovu isainiwe??

Unajua mkataba ukisainiwa kuvunja ni gharama?? Na kama alijua hili kwanin aliruhusu?
Yes, kwa mantiki ya collective responsibility alikubali.Ila naamini kwamba hata huo mkataba hauku-mention kwamba migodi i-export michanga bila ya the other party kujua kuna nini, otherwise itakuwa mikataba ya kijuha sana!Kama ni hivyo, basi makampuni yenye migodi ndiyo yaliyoanza kuvunja mikataba,kwa hiyo Rais ana haki ya kufanya alilofanya.
 
Ameshapata urais...kwanini hataki mikataba ipelekwe bungeni ikaguliwe upya??
 
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM (AKIWEMO YEYE) WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!

NI MNAFKI MKUBWA.

Kashaona mambo kavurunda sasa ameamua kufanya economic suicide kwa nchi ili baadae asingizie kuwa sabotaged. na mazuzu wengi watamshangilia.,
Wanaita TV's tuone tulivyoibiwa wakati miaka 50 chama pekee kilichotawala ni CCM. Mikataba inayotumika kutuibia wamesaini wao, na huyu MNAFKI akiwa baraza la mawaziri. Hakuna hata siku aliyosema hadharani kuhusu hilo.

Hii wiki tutaikumbuka kama wiki tuliyogeuka BANANA republic.

Kama hatutaki wawekezaji tuwaambie wasije. Kama hatuutaki kuibiwa TUACHE kusaini mikataba gizani KISHA kuificha isionekane na yoyote yule. Bila kufanya hivyo hakuna mantiki ya upuuzi uliofanyika ikulu.

Ilikuwa ni show ya kishabiki, kutafuta umaarufu usio na sababu.

Mkataba wa kitapeli wasaini BARICK na CCM halafu CCM ije ikulu kutupigia kelele Barrick wanatuzulumu. Endeleeni kudananya wapuuzi.
 
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM (AKIWEMO YEYE) WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!

Mkubwa unajichosha tu, hawa watu ni wanafiki kwa kwenda mbele.....

Mchawi, jambazi na muuaji ndiye siku zote huwa wanajifanya wanalia kwa uchungu kweli kwenye msiba wa mtu yuleyule waliyemuua wao....!!

Hawa ndiye huyu Magufuli wa leo na wana CCM wenzake, wauaaji wakubwa hawa na leo ndiyo mapaji yao ya uso yameloa na machozi kwa kisingizio cha kumlilia marehemu Tanzania waliyemuua.....

Aisee, hii ni hatari kwelikweli !!!
 
Wewe kama unaona hivyo comment hivyo unavyotaka. Sisi tunakupa hali iliyoko ndani ya chama na bunge lao.

Mfano Maghufuli alishiriki siku ile kupitisha mswaada wa Gas na mafuta usiku wa manane, je hakuelewa alichokuwa anakifanya pamoja na wapinzani kusimama kidete kuipinga ?! Ni mfumo unaotakiwa kubomolewa hasa ndani ya chama na kuwaacha wajumbe huru vichwani
Nakubaliana na wewe Mkuu. Mzee Magu Aliona mbali na alifanya makadirio na hesabu za mbali. Kwa mfumo uliokuwepo ccm, angeonyesha dhamira yake ya kweli na uhalisia wake ni wazi angepotezwa kama alivyopotezwa Lyatonga, Kolimba, Maalim Seif n. K. Aliulewa mfumo uliokuwepo na kuwa na Mpango kazi wa muda mrefu. Wanaokupinga uwezo wao wa kuchambua mambo ni finyu. Kwa anayoyafanya sasa Mh. Rais ndio wakati sahihi akiwa ameshika hatamu zote za nchi na vyombo vyote vya dola.
 
Back
Top Bottom