Je, Rais Magufuli hakuyaona haya alipokuwa mbunge/waziri?

Hii ndiyo point mengine hayana maana!! Sasa je kama hakuyapenda kwanini hakusema aua hata walau kushauri???

Tumuaminije sasa??
Timing. Hakuwa wakati. Mfumo uliokuwepo ungemtupa nje na kupoteza na pengine leo tungekuwa katika hali mbaya. Ukombozi unataka mipango mkakati na ni mipango mkakati ya muda mrefu sio papara.
 
Kujibu swali LA mleta hoja ni kuwa angethubutu kupingana na wakubwa wake asingekuwa Rais leo . Kilichomo ndani ya CCM humo ni kuwa fala kwa matakwa ya boss au chama. Mfano ni bunge live na Nape na wabunge wote wa CCM hawawezi kumkosoa Maghufuli ni mfumo wao.

Tukiacha kuogopa defender na washawasha viongozi wetu watasaini mikataba yenye tija, si sasa hawana wasiwasi wowote
Kwahiyo Mkuu, CCM waliochini wanaunga mkono mambo ya kuangamiza taifa ikiwa tu Mkubwa wao amekusudia hilo jambo?

Una maana leo hii Magufuli angekuwa mbunge na sio rahisi bado angepitisha madudu ya CCM?

Jamani sio magufuli huyu aliyeleta MV Dar es Salaam? Alivyoleta ujeuri akaipeleka JWTZ na kuwaambia wananchi wanaokisema kivuko hiko wajue ni mali ya Jeshi, je kile kivuko kilitengenezwa kwa madhumuni ya Jeshi? Ni sawa na leo hii hao viongozi wa jeshi waje wajifanye wazalendo, wakati nao wanaona kabisa ujinga ambao watanzania tumefanyiwa.
 
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM (AKIWEMO YEYE) WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!

Acheni kumulaumu Rais Magufuli. Kumbukeni Hosea alikuwa Mkuu wa Tukuru, lakini alipokuwa akichunguza mafisadi according to weakleaks alimweleza balozi wa Marekani kuwa Rais Kikwete kamwambia asichunguze ufisadi aende pole pole. Watanzania tuna ugonjwa mmoja, hatuwezi kuwapinga wakubwa zetu, malezi haya tunaanza bado wadogo, kila kitu tunakubali kwa unafiki. Wapinzani musiseme kitu, haswa Chadema, yeyote akifukuzwa CCM munamusafisha na munamukaribisha kwa mikono miwili. Upinzani ungechukuwa serikali, musingefanya anayoyafanya Magufuli, muliyemuchaguwa kupigania Urais kwa niaba ya chama Chenu ni Lowassa badala ya kunyimwa fulsa CCM, na alikuwa na lawama ya Richmond, mpaka akajihuzuru. Hajapelekwa mahakamani, nyinyi wenyewe wapinzani mukimuita fisadi mala kujiunga na nyinyi akawa msafi.

So far Watanzania hawana alternative zaidi ya Rais Magufuli. Wengi kwenye upinzani mulikuwa CCM, na wengi mkifanyiwa test ya integrity mutashindwa mmoja mmoja. Rais Magufuli alikuwa mbunge na alikuwa Waziri, katiba yetu Waziri hampingi Rais, Rais ana power kubwa, na angempiga Rais Magufuli leo asingekuwa Rais.

Nape katetea ukweli leo hana kazi, hizi ndizo siasa za kiafrika, hatujakomaa kidemokrasia. Hata kama Chadema wengechukuwa serikali ingekuwa worse. Inaonekana wazi, kwa vitendo kuwa Rais Magufuli anavyofanya, serikali iliyopita ilikuwa ikimuudhi sana, lakini la kufanya kama Watanzania wengine alikuwa hana. Alijaribu kukamata wezi wa samaki zetu, akageuziwa kesi akawa yeye ndiye mshitakiwa, si ajabu na hii kesi ya mchanga atageuziwa yeye, sio na Wazungu bali na baadhi ya Watanzania ambao wana chuki na ubinafsi wa nchi hii watakuwa UPANDE wa Wazungu wanaotuibia kwa sababu hali mbaya iliyokuwepo, wachache walikuwa wakifaidika.
 
Aliyaona na kuyapitisha akiwa waziri na mbunge.
Tena na yeye alishiriki kutuibia sana. Meli mbovu aliyonunua,akauza na kugawa nyumba za serikali.
Na leo anasimama mbele za camera kujinadi kuwa ana uzalendo na Tanzania, sijui uzalendo unakuja baada ya mtu kupewa madarakaaa!!!!??????

Poor CCM, hata baada ya 2020 atakuja mwingine na ngonjera hizihizi.
 
Mkuu;
Ningependa kusema hivi;
Magufuli aliyaona haya yoote ila hakuyapenda. Ndio maana tangu siku ya kwanza alipopewa fimbo ya kukimbiza Tz nzima, hakutoka kama mgombea wa ccm bali alitoka kama Magufuli mwenyewe. Tukaambiwa, chagua Magufuli.
Nadhani, moyoni alitamani apite aje atengue hivi vitendawili. Usiwaone mawaziri na wabunge wa ccm useme ni wote wanafurahia uovu huu.Wapo wachache wanaumia kindani ndani lakini hawajui wafanyeje. Ni mawazo yangu tu ila kama tukipita huu mtego, tiyari tutakuwa tumeikomboa nchi
Ulishawahi kukisikia kivuko cha MV Dar es Salaam? Unajua kuwa nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya kutupwa? Unajua kipindi hiko Waziri alikuwa ni nani?

HAKUNA MSAFI WA KUMUONESHEA KIDOLE MWENZIE NDANI YA CCM.
 
Acheni kumulaumu Rais Magufuli. Kumbukeni Hosea alikuwa Mkuu wa Tukuru, lakini alipokuwa akichunguza mafisadi according to weakleaks alimweleza balozi wa Marekani kuwa Rais Kikwete kamwambia asichunguze ufisadi aende pole pole. Watanzania tuna ugonjwa mmoja, hatuwezi kuwapinga wakubwa zetu, malezi haya tunaanza bado wadogo, kila kitu tunakubali kwa unafiki. Wapinzani musiseme kitu, haswa Chadema, yeyote akifukuzwa CCM munamusafisha na munamukaribisha kwa mikono miwili. Upinzani ungechukuwa serikali, musingefanya anayoyafanya Magufuli, muliyemuchaguwa kupigania Urais kwa niaba ya chama Chenu ni Lowassa badala ya kunyimwa fulsa CCM, na alikuwa na lawama ya Richmond, mpaka akajihuzuru. Hajapelekwa mahakamani, nyinyi wenyewe wapinzani mukimuita fisadi mala kujiunga na nyinyi akawa msafi.

So far Watanzania hawana alternative zaidi ya Rais Magufuli. Wengi kwenye upinzani mulikuwa CCM, na wengi mkifanyiwa test ya integrity mutashindwa mmoja mmoja. Rais Magufuli alikuwa mbunge na alikuwa Waziri, katiba yetu Waziri hampingi Rais, Rais ana power kubwa, na angempiga Rais Magufuli leo asingekuwa Rais.

Nape katetea ukweli leo hana kazi, hizi ndizo siasa za kiafrika, hatujakomaa kidemokrasia. Hata kama Chadema wengechukuwa serikali ingekuwa worse. Inaonekana wazi, kwa vitendo kuwa Rais Magufuli anavyofanya, serikali iliyopita ilikuwa ikimuudhi sana, lakini la kufanya kama Watanzania wengine alikuwa hana. Alijaribu kukamata wezi wa samaki zetu, akageuziwa kesi akawa yeye ndiye mshitakiwa, si ajabu na hii kesi ya mchanga atageuziwa yeye, sio na Wazungu bali na baadhi ya Watanzania ambao wana chuki na ubinafsi wa nchi hii watakuwa UPANDE wa Wazungu wanaotuibia kwa sababu hali mbaya iliyokuwepo, wachache walikuwa wakifaidika.
Ivi unaposema rais hapingwi, unakumbuka baada ya ndalichako kuona haendani na jk alifanya nini???

BTW sio kwamba tunamlaumu...ni kwamba ajue huu upuuzi ulianzia kwao na sio vingine! Na pia iwe funzo kwa wabunge wa ccm waache ujinga wa kupiga makofi hata kama hamna la maana!!
 
Sio Wabunge wa CCM tu wabunge wote. Kitu kikubwa ni katiba, katiba tuliyonayo haiendi na siasa ya sasa. Hakuna haja ya kulaumu chama, watu wakiwa kwenye chama mawazo yao hayafanani, wanakuwa na mawazo mbali mbali. Tunaweza wote tukawa Chadema na vitendo vyangu tofauti na wewe, pengine wewe vitakuudhi. Hakuna haja ya kulaumu wana chama wote wa CCM, ama wana chama wote wa Chadema, sisi wote ni Watanzania, kwenye jambo ambalo linatuhusu uhai wetu, tuweke siasa mbali na tuwe kitu kimoja.
 
Ulishawahi kukisikia kivuko cha MV Dar es Salaam? Unajua kuwa nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya kutupwa? Unajua kipindi hiko Waziri alikuwa ni nani?

HAKUNA MSAFI WA KUMUONESHEA KIDOLE MWENZIE NDANI YA CCM.

Waziri hana uwezo wa kuuza nyumba za serikali bila ya Rais na bunge. Yeye ni kuambiwa tu fanya hivi na anafanya. Mawaziri kwa katiba tuliyonayo Sasa hawana power ya kuamua wana power ya kutimiza wajibu wao wakiamuliwa kufanya. Magufuli hakuuza nyumba za serikali kwa amri yake, aliamuliwa auze yumba za serikali yeye akiwa Waziri. Waulizeni Kikwete na Mkapa hawa ndiyo machampioni wa kuuza Mali za Watanzania.
 
Umeanza kuutetea upuuzi!
 
Huu ni ukweli sio upuuzi. Ni wewe ndiye huekewi. JE unaijuwa katiba ya Tanzania ana unasema tu. Hii ndiyo shida ya kusema bila kuelewa. Watu wakikuelewisha unadunda. Sasa niulize kufanya ndiyo nini ha ha ha
Kwa hiyo yeye ni roboti kwamba akiambiwa abweke anabweka? Funny, huh!
 
Kiongozi wa kututoa hapa lazima atambue na kukiri makosa yamefanyika kutokana na mfumo mbovu wa serikali inayoongozwa na ccm kwa miaka zaidi ya 50 na awe tayari kuyasahihisha kwa kuweka mifumo thabiti ya kuhakikisha makosa na mapungufu kama haya hayatatokea tena. Lazima atambue uraisi ni taasisi na sio one man show. Akitaka kufanya kila kitu peke yake siku hayupo ina maana tutarudi kulekule.

Kama ana nia ya kweli ya kututoa hapa lazima, lazima lazima abadilishe ile dhana ya mkubwa kashasema hakuna wa kumpinga. Lazima aijenge na kuheshimu majukumu ya mihimili mingine.

Kama ana nia ya dhati lazima wale waliojihusisha kuliinguza taifa kwenye hasara wachukuliwe hatua stahiki. Kelele za majukwaani na kujiuzulu haitoshi.

Swali ni Je, raisi wetu mtukufu anafanya haya?

Nikuchallenge, kiongozi gani wa kututoa hapa???
 
Mawaziri wote wanachukuwa order kutoka kwa Rais. Mfano wa robot haundani na hii issue, tafuta mufano mwingine, ama sivyo soma katiba ya Tanzania kabla ya kuandika upuuzi unajiumbulisha.
Hapo ndipo unaukomelea upuuzi. Kwa hivyo alivyokuwa waziri alikubali kufanya yote ili atunze tu uwaziri badala ya kuangalia maslahi ya nchi. Eti kupokea maagizo ya Rais. My left foot! Hakuona madudu anayoyasafisha leo? Tendea haki jina lako usiitwe kopo.
 
Kiongozi wa kututoa hapa lazima atambue na kukiri makosa yamefanyika kutokana na mfumo mbovu wa serikali inayoongozwa na ccm kwa miaka zaidi ya 50 na awe tayari kuyasahihisha kwa kuweka mifumo thabiti ya kuhakikisha makosa na mapungufu kama haya hayatatokea tena. Lazima atambue uraisi ni taasisi na sio one man show. Akitaka kufanya kila kitu peke yake siku hayupo ina maana tutarudi kulekule.

Kama ana nia ya kweli ya kututoa hapa lazima, lazima lazima abadilishe ile dhana ya mkubwa kashasema hakuna wa kumpinga. Lazima aijenge na kuheshimu majukumu ya mihimili mingine.

Kama ana nia ya dhati lazima wale waliojihusisha kuliinguza taifa kwenye hasara wachukuliwe hatua stahiki. Kelele za majukwaani na kujiuzulu haitoshi.

Swali ni Je, raisi wetu mtukufu anafanya haya?

Lazima nikubali serikali ya Magufuli ina mapungufu yake, sina Wakati wa kuyapitia, lakini Pamoja na mapungufu yake kwa sasa hatuna alternative, anayoyafanya kwa sasa hata kama alikuwa ndani ya CCM inaonekana Mengi yalikuwa yakimuuzi. Sasa wewe Ssema ukweli, nani katika upinzani anaweza kuwa Rais na afanye mambo yote anayoyafanya Rais Magufuli Pamoja na mapungufu yake. Watu wengi walikuwa hawategemei, Viongozi wengi waliopita na ahadi tele, lakini wengi wao wanekumbatia wizi na dhuruma za walio wengi. Mimi binafsi ningependa MARAIS wa zamani wawekwe kizimbani ili wawaeleze Watanzania kwa madhambi yote waliyoyafanya ikiwa pamoja na mikataba mibovu. Je ni nani angeweza kuchukuwa hatuwa kama hizo? Na woga wa Wawatanzania? Si afadhari Rais Magufuli amejaribu. Hatujui vitisho vingapi anevipokea. Jamani Mnyonge munyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Hapo ndipo unaukomelea upuuzi. Kwa hivyo alivyokuwa waziri alikubali kufanya yote ili atunze tu uwaziri badala ya kuangalia maslahi ya nchi. Eti kupokea maagizo ya Rais. My left foot! Hakuona madudu anayoyasafisha leo? Tendea haki jina lako usiitwe kopo.

Ndiyo mawaziri wote wanaweza kuchunga kazi zao. Tanzania sio Uingereza wala Marekani kwenye demokrasia zilizokumaa na power ya Rais iko kwa watu. Bado tuna katiba ya kikoloni, tumeipiga vilaka hapa na pale tu. Rais bado Ana power kubwa. Umeona Nape kafukuzwa kwa kusema ukweli? Na Huu sio upuuzi, ni kwa vile huielewi katiba ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom