Je, Rais Magufuli hakuyaona haya alipokuwa mbunge/waziri?

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,532
34,909
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM (AKIWEMO YEYE) WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Labda aliogopa mamlaka za juu....kama alivyoogopa Lowasa na kuingia mkataba wa Richmond na kuliletea taifa hasara....

Hili jibu nililitarajia sana!! Kwahiyo unamaanisha magufuli ni muoga??? Hata kama aliogopa kwanini hakusema ukweli ili aokoe nchi kama kweli alikua na nia hiyo??

Okey kama aliogopa ina maana ni muoga...so akija trump akamwambia nataka nchi then atampa kwasababu anaogopa wakubwa??
 
Sahv magufuli anajichukulia misifa tu kwa mambo aliyo kuwa akiyapitisha yy na akijua madhara yake...
Kwakuwa wa Tz ni watu wa matukio leo walio wengi wanamuona shujaa kwa kutoa kafara kina Muhongo kwa mambo ambayo yalikuwepo tangu enzi.
Kama kweli magufuli ana uchungu na rasilimali za nchi hii serikali yake na ipitie upya mikataba yote tata aache maigizo ya kuumia na kusononokea rasimali zetu mbele ya kamera na vipaza sauti.
 
Kujibu swali LA mleta hoja ni kuwa angethubutu kupingana na wakubwa wake asingekuwa Rais leo . Kilichomo ndani ya CCM humo ni kuwa fala kwa matakwa ya boss au chama. Mfano ni bunge live na Nape na wabunge wote wa CCM hawawezi kumkosoa Maghufuli ni mfumo wao.

Tukiacha kuogopa defender na washawasha viongozi wetu watasaini mikataba yenye tija, si sasa hawana wasiwasi wowote
 
Hili jibu bado ni mfu kabisa!! Inamaana huyu magufuli anaogopa wakubwa???

Kwa hiyo trump akija akamwambia anataka nchi atampa kwasababu ni mkubwa??
 
Sahv magufuli anajichukulia misifa tu kwa mambo aliyo kuwa akiyapitisha yy na akijua madhara yake...
Kwakuwa wa Tz ni watu wa matukio leo walio wengi wanamuona shujaa kwa kutoa kafara kina Muhongo kwa mambo ambayo yalikuwepo tangu enzi.
Kama kweli magufuli ana uchungu na rasilimali za nchi hii serikali yake na ipitie upya mikataba yote tata aache maigizo ya kuumia na kusononokea rasimali zetu mbele ya kamera na vipaza sauti.
Kuna mambo yanafanyika hapa nchini nashindwa kuelewa kabisa!!
 
Hili jibu nililitarajia sana!! Kwahiyo unamaanisha magufuli ni muoga??? Hata kama aliogopa kwanini hakusema ukweli ili aokoe nchi kama kweli alikua na nia hiyo??

Okey kama aliogopa ina maana ni muoga...so akija trump akamwambia nataka nchi then atampa kwasababu anaogopa wakubwa??
Hata Lowasa pia aliogopa kusema ukweli kwanini alisani mkataba mbovu wa Richmond.....

Na leo ni mwanachama wetu na anatarajiwa kugombea uraisi...2020....
 
Hujajibu swali! Kama aliogopa Ina maana yeye ni muoga??

Kama kweli alikua na nia kwanini asingesema au hata kushauri kwamba hii mikataba si rafiki!!

Kama alikaa kimya na mikataba ikasainiwa tumueleweje???
 
Hili jibu bado ni mfu kabisa!! Inamaana huyu magufuli anaogopa wakubwa???

Kwa hiyo trump akija akamwambia anataka nchi atampa kwasababu ni mkubwa??
Wewe kama unaona hivyo comment hivyo unavyotaka. Sisi tunakupa hali iliyoko ndani ya chama na bunge lao.

Mfano Maghufuli alishiriki siku ile kupitisha mswaada wa Gas na mafuta usiku wa manane, je hakuelewa alichokuwa anakifanya pamoja na wapinzani kusimama kidete kuipinga ?! Ni mfumo unaotakiwa kubomolewa hasa ndani ya chama na kuwaacha wajumbe huru vichwani
 
Napenda kukujibu kwa mifano hai....

Hata Lowasa alipokuwa CCM aliiponda katiba ya Warioba na kupinga ukawa kwa maslahi ya chama chake cha zamani.....

Hata Lowasa alipokuwa waziri mkuu aliogopa mamlaka ya juu na kuupitisha mkataba tata wa Richmond....

Sasa kama kiongozi kama waziri mkuu anaheshimu na kugopa mamlaka za hadi kuingia inayolitia hasara taifa....waziri au mbunge anawezaje kupingana na matakwa ya walio wengi kwenye chama chake.....

Wewe unadhani hata hayo yanayoanyika huko CCM wanaCCM wote wanapendezwa nayo.....!!??
 
Hujajibu swali! Kama aliogopa Ina maana yeye ni muoga??

Kama kweli alikua na nia kwanini asingesema au hata kushauri kwamba hii mikataba si rafiki!!

Kama alikaa kimya na mikataba ikasainiwa tumueleweje???
Yupi muoga zaidi waziri mkuu aliyesaini mkataba mbovu na kulitia hasara taifa....na mbunge au waziri aliyeogopa kuongelea kuhusu mkataba mbovu....!!?
 
Wewe kama unaona hivyo comment hivyo unavyotaka. Sisi tunakupa hali iliyoko ndani ya chama na bunge lao.

Mfano Maghufuli alishiriki siku ile kupitisha mswaada wa Gas na mafuta usiku wa manane, je hakuelewa alichokuwa anakifanya pamoja na wapinzani kusimama kidete kuipinga ?! Ni mfumo unaotakiwa kubomolewa hasa ndani ya chama na kuwaacha wajumbe huru vichwani
Nahisi mtoa mada yupo kwenye mhemko wa hali ya juu sana.....kwa sababu kama waziri mkuu aliogopa mamlaka za juu na kusaini mkataba mbovu....mbunge au waziri kutoak chama chao anawezaje kuzuia hilo lisitokee.....!!??
 
Mkuu;
Ningependa kusema hivi;
Magufuli aliyaona haya yoote ila hakuyapenda. Ndio maana tangu siku ya kwanza alipopewa fimbo ya kukimbiza Tz nzima, hakutoka kama mgombea wa ccm bali alitoka kama Magufuli mwenyewe. Tukaambiwa, chagua Magufuli.
Nadhani, moyoni alitamani apite aje atengue hivi vitendawili. Usiwaone mawaziri na wabunge wa ccm useme ni wote wanafurahia uovu huu.Wapo wachache wanaumia kindani ndani lakini hawajui wafanyeje. Ni mawazo yangu tu ila kama tukipita huu mtego, tiyari tutakuwa tumeikomboa nchi
 
Wewe kama unaona hivyo comment hivyo unavyotaka. Sisi tunakupa hali iliyoko ndani ya chama na bunge lao.

Mfano Maghufuli alishiriki siku ile kupitisha mswaada wa Gas na mafuta usiku wa manane, je hakuelewa alichokuwa anakifanya pamoja na wapinzani kusimama kidete kuipinga ?! Ni mfumo unaotakiwa kubomolewa hasa ndani ya chama na kuwaacha wajumbe huru vichwani
Kama alishiriki kupitisha mikataba hovyo tumwaminije sasa ivi??

Je haya madhara ya kuivunja kama ikibidi unadhani atalipa yeye au mimi na wewe?
 
Back
Top Bottom