Je, Rais Magufuli hakuyaona haya alipokuwa mbunge/waziri?

Hili jibu nililitarajia sana!! Kwahiyo unamaanisha magufuli ni muoga??? Hata kama aliogopa kwanini hakusema ukweli ili aokoe nchi kama kweli alikua na nia hiyo??

Okey kama aliogopa ina maana ni muoga...so akija trump akamwambia nataka nchi then atampa kwasababu anaogopa wakubwa??
Unajuaje kama hakusema ukweli au kupinga wakati suala hili lilipitishwa kwenye baraza la mawaziri na mijadala ya huko huwa ni ya siri na jambo likishapitishwa huko kuja bungeni mtu hubanwa na kanuni ya corrective speech?
 
Unajuaje kama hakusema ukweli au kupinga wakati suala hili lilipitishwa kwenye baraza la mawaziri na mijadala ya huko huwa ni ya siri na jambo likishapitishwa huko kuja bungeni mtu hubanwa na kanuni ya corrective speech?
Kanuni za collective responsibility zilimtaka kama alipinga halafu jambo likapitishwa na yeye akaona hapendi, na jambo ni la msingi, ajiuzulu na aende kulipinga nje ya serikali.

Hakufanya hivyo.

Kanuni hizohizo zinasema jambo ukilipinga halafu likapitishwa, halafu usijiuzulu, na wewe umelipitisha.

Hivyo Magufuli alipitisha.

Na zaidi, mtu atakayesema Magufuli anakula njama na wawekezaji kuikamua fedha serikali katika kesi ya usluhishi London, siwezi kukataa.

Ni kama vile Magufuli kapitisha mkataba mbovu, wawekezaji wamechota madini mpaka wamemaliza, walivyomaliza wakamwambia Magufuli tuvunjie mkataba ili tukushitaki na kushinda kesi halafu serikali ipigwe faini tuliowe bila kuchimba madini kama IPTL.

Ndicho kitakachotokea.
 
Aliyaona na bado haiwezi kumzuia kuyaongea Leo, kikubwa ni pale mwanadamu unapoamua kujitambua na ukajisahihisha kwanzia hapo unakuwa umejiweka katika kundi la kuwa karibu na wanadamu na hata Muumba wako pia.
 
Kumlaumu rais kwamba alikuwepo wakati haya yaletayo tafrani leo unamwonea. Ukiwa ndani ya mfumo si kweli kuwa unakubaliana nao 100%, na ukionesha upinzani unatemwa, collective responsibility. Lawama kwake ni sasa ambapo anajua tatizo kuu la nchi hii ni katiba na sheria mbovu ambazo alishiriki kuzipitisha japo ni kwa shingo upande, lakini anazikumbatia, au kutaka kuzikwepa bila kuziondoa kwanza kwa taratibu zinazoeleweka.
Kwa hiyo hapa ile dhana ya kwamba ni mzalendo haipo ila ni tumbo linasumbua....mana tunaona huko duniani mtu asipokubaliana na hoja ya mkubwa wake anachukua maamuzi binafsi kuachia nafasi..lakini in tz hili aliwezekani mana kila mtu yupo kimaslahi binafsi zaidi...angekuwa na dhana ya uzalendo angeanza na mchakato wa katiba lakini...ndo hivyo
 
Kwanza nianze kwa kusema nnaumia sana kuona makaburu wakijinufaisha na rasilimali zetu huku mzawa akipata shida zisizo na ulazima.

Lakini nnajiuliza haya...

Hii mikataba ya madini wakati inasainiwa magufuli si alikua waziri? Si alikua mbunge? Kwanini alikaa kimya kipindi hicho?

Wakati mikataba hii inasaini Rais Magufuli si alikua mbunge? Kwanini asingetoa wazo mikataba hii ijadiliwe bungeni? Lakini cha kushangaza kwanini alikaa kimya kama mbunge?

Je ni mikataba mingapi ya hovyo alipitishwa bungeni yeye akiwa mbunge na alikua mstari wa mbele kusema NDIO huku akizani anawakomoa CHADEMA?

Kwanini kipindi hicho asingeikataa kama kweli alikua na nia ya kuipigania nchi?

Ni mara ngapi mkiwa bungeni akina zitto na mnyika waliwaonya juu ya hii mikataba mkawapuuzia?

Sasa tayari mikataba imesainiwa na kama hujui tu hamna mkataba unavunjwa bila kumlipa mzungu uliyewekeana nae makubaliano.

Nitoe tu angalizo... HAWA WABUNGE WA CCM (AKIWEMO YEYE) WANAOSEMA NDIOOOOO NA KUPIGA MEZA BILA KUJUA MADA NDIO WAMETUFIKISHA HAPA Na bado tutayaona mengi.

Angalizo tu..haya ya ACCACIA yasije kuwa kama Dowansi na akina Escrow!

Mungu ibariki Tanzania!
Aliyaona, lakini aliogopa neno "Sio Mwenzetu", hivyo, akawa anamwomba Mungu amwezeshe siku moja akabidhiwe kijiti, ndo maana unaona baada ya kukabidhiwa kijiti anachambua yale aliyokuwa anaona. Wewe ulitaka awe kama Mhe. James Lembeli ?
 
Aliyaona na bado haiwezi kumzuia kuyaongea Leo, kikubwa ni pale mwanadamu unapoamua kujitambua na ukajisahihisha kwanzia hapo unakuwa umejiweka katika kundi la kuwa karibu na wanadamu na hata Muumba wako pia.
Aliyekuwa na uchungu na nchi yake alishajipumzikia zake hawa wengine wote wapiga dili tuu...huyu anajitutumua tuu lakini hakuna kitakacho msaidia mtanzania hapo kutokana na hii inshu ya mchanga
 
WanaCCM wakikubaliana na kauli hii, nitamwelewa Rais kwa ukimya wake.
Hivi ndivyo naamini inafanyika.
Na siku zote tunasema maamuzi mengi yanafanyika kwa maslahi ya CCM
Tatizo CCM wao wenyewe wanasema wamefanya maamuzi hayo kwa maslahi ya Taifa.
Kifupi hawataki kukubali makosa.

Mkuu Utotole;
Hawa maccm hayana makosa kabisa. Wameondoka kwenye msingi wa imani yao sasa wamebakia tu kujilinda wasije toka madarakani. Hii inaleteleza kuulinda mfumo usipinduliwe.
Ingelikuwa ni upinzani umefanikiwa kuyaleta mabadiliko haya, sidhani kama mwaka ungeliisha kabla haya yoote hayajafumuliwa.
JPM akitaka mafanikio, aufumue mfumo tangu mkuu hadi mdogo. Akumbuke analindwa na katiba hivyo akifumua hataguswa wala kuwagusa walio mtangulia. Hatutavunja katiba bali tutaipamba katiba. CCM watake wasitake, njia pekee kupona ni kuufumua mfumo. Ipo siku, watajikuta sio wao wanaufumua, nayo itakuwa mbaya mno kwao. Aheri kukiosha kidonda wewe mwenyewe kuliko nurse.
 
Magufuli hajaanza leo kupiga kelele kuhusu mikataba ya madini, tangu akiwa waziri hili swala alikuwa analiongelea tena kwa hisia kali. Acheni kuwaaminisha watu uongo mlitegemea angefanya nini wakati hakuwa waziri wa nishati na madini ? Angelikuwa kashika hiyo wizara akashindwa kuchukua hatua hapo ndo ange ingia kwenye lawama
Alikuwa anakwmbia wewe na Mumeo sio ?
 
Ni ndugu moja? Je naye magufuli unataka sema ni fisadi??

Unaposema lowassa ni fisadi kwanini asichukuliwe hatua jibu swali!!
Mkuu, usiwe na hasira sana. Hii nchi inahitaji upole tu. Ukiruhusu hasira zikuongoze, unaweza kuua mtu bure au hata kujitia kitanzi ukaacha waswahili wakiendelea na mizaha yao kwa raha zao. Tena wakikushangaa nini kilichokupata? Soma bandiko taratibu upate kuuelewa ujumbe niliotaka kuufikisha.

Halafu vuta subira. Haya mambo nayo yatarejea palepale yalipotokea. Nani leo hii mwenye ubavu wa kumwajibisha Mkapa au Kikwete? Hii fokafoka inayoendelea ni kuwasaidia Watanzania kisaikolojia wapunguze jazba (letting out the steam) baada ya kuibiwa sana; wasije wakapasuka bure kama inavyotaka kukutokea wewe hivi sasa. Acha wenye msiba wao walie kwa sauti kubwa zaidi.
 
Nimekuelewa sana tu, uko katika kuwafunda walio katika nafasi za maamuzi. Lakini kuna ukweli ambao hutaki kukiri nao ni JPM asinge weza kufanya haya anayofanya sasa kama Rais wakati akiwa Mbunge na waziri. Sanasana angejiuzulu pengine akarudi kwao kulima ngombe na hata asingekuwa Rais leo hii. Na asinge fanya haya afanyao kama Rais maana si Rais.


Na washawasha!
Hii ndiyo ile kitu inayoitwa "tragedy" ya taifa hili. Hata leo hii pamoja na kuwa Rais, Magufuli bado hana jeuri ya kuwagonga wahusika wenyewe wa ufisadi huo. Ataishia kuzuunguka tu mbuyu. Very soon, we will return to square one.
 
Mafisadi wangapi imewasafisha na akina nani?Nafikiri Tanzania haijawahi kuwa na Fisadi aliye hai,angekuwepo Magufuli asingeruhusu asifik, hwe mbele ya mahakama ya kifisadi na kuhukumiwa kama impasavyo.
Kamanda swala la mafisadi wangapi na kina nani nadhani swali hilo ungenisaidia kuwauliza wale viongozi waliokuwa wakituaminisha wakati huo sisi ni wapinzani waukweli. Uliza tuu kina Mbowe ,Mnyika, Kubenea, Msigwa, Lema, lissu aliyetengeneza list of shame na wengineo unaowajua. nisaidie kuwauliza halaf uje hapa. Na wala usije na jibu la eti walikua wanatania. Itakuwa ni upumbaf na ujinga, kwa sababu kwwnye masuala nyeti ya nchi sitegemei mpinzani ambaye analilia kwenda ikulu atataka kwenda kimzahamzaha tuu. Mtu wa namna hiyo hatutamruhusu kwenda ikulu
 
Ingekuwepo tofauti kubwa ya ulichokisema hapa na nilichokisema mimi, ningejibu hoja hizo point kwa point. Ila tofauti kubwa siioni zaidi ya confusion na "big ego" uliyonayo.
Somehow, tutakutana mbele ya safari.

poa nashukia manzese niko mapipa sasa hivi
 
Kamanda swala la mafisadi wangapi na kina nani nadhani swali hilo ungenisaidia kuwauliza wale viongozi waliokuwa wakituaminisha wakati huo sisi ni wapinzani waukweli. Uliza tuu kina Mbowe ,Mnyika, Kubenea, Msigwa, Lema, lissu aliyetengeneza list of shame na wengineo unaowajua. nisaidie kuwauliza halaf uje hapa. Na wala usije na jibu la eti walikua wanatania. Itakuwa ni upumbaf na ujinga, kwa sababu kwwnye masuala nyeti ya nchi sitegemei mpinzani ambaye analilia kwenda ikulu atataka kwenda kimzahamzaha tuu. Mtu wa namna hiyo hatutamruhusu kwenda ikulu
Kubishia kiuno kwa jambo ambalo hao unao wataja walishasema kuwa walikosea kumtuhumu huyo mzee ni ujinga. Tafuta kitu kingine. Kama unabishia kiuno bado, mpeleke mahakama ya wezi. Ukuishindwa kufungua mashtaka unyamaze. Hopeless material kabisa!
 
Back
Top Bottom