Je, Rais Magufuli atahudhuria kikao cha UN General Assembly cha mwaka huu?

Vikao vya UN ni vikao vya kupoteza muda na kula bata tu hasa kwa marais wa Africa. Unakuta Rais toka Africa anapoteza pesa kwenda kuongea nusu saa tu kama sio upuuuzi ni nini! Unachoongea chenyewe hamna anaezingatia. Kazi hiyo anaweza fanya muwakilishi tu sio Rais na msafara wake.

Ian Khama Rais aliyepita wa Botswana alikua haudhuruu kabisa huu upuuzi na nchi yake ilipiga hatua zaidi chini ya utawala wake.

Kule UN kuna mambo ya pembeni yanayoendelea kwenye corridor za diplomasia kuliko kuongea hiyo nusu saa

Kuna kukutana on the sideline na viongozi wenzako wa mataifa mbalimbali mkazungumza ushirikiano

Kuna kukutana na delegations za wafanyabiashara na wawekezaji etc

Ina maana hata Nyerere alipokuwa akienda huko alikuwa anapoteza pesa?
 
Wakuu naombeni msaada kuna thread ilitoka juzi story yake Inamhusu tajiri ROMAN IBRAMOVIC na hustling zake , nilijisahau ku- subscribe, mtu anayejua ile thread ilipo pls nisaidie, pia kuna watu walio tag-wa you can direct me pls

Thanks
Kumradhi kwa kuvamia hii thread
 
Hapa JF angalia kulia kwenye webapage ya JF pembeni mwa jina lako lilipoandikwa, utakuta kialama cha "Search" kikclick hicho halafu type kuhusu Roman Ibramovic, zitakuja thread kibao kumhusu na wewe utachagua unayoitaka
 
Kikao cha UN General assembly kinafanyika tena mwezi wa tisa mwaka huu kama ilivyo ada

Ni mwaka wa nne huu wa utawala wa Rais Magufuli hajawahi kusafiri kutoka nje ya Afrika, tofauti na watangulizi wake, Mheshimiwa Magufuli hajahudhuria kikao hata kimoja cha UN General assembly.
Kikawaida vikao vya General assmebly ni vikao vyenye hadhi ya wakuu wa nchi ambapo mambo mengi huzungumzwa pale lakini ukiacha mbali na hapo huwa ni nafasi nzuri kwa mkuu wa nchi mmoja kupata nafasi ya kuongea na kukubaliana mambo mengi ya maendeleo na wakuu wenzie wa nchi mbalimbali.

Kwa sasa mathalani zao letu la korosho limeyumba, huu ulikuwa ni muda muafaka wa raisi Magufuli kuongea na wakuu wenzie wenye viwanda na masoko ya korosho kuona Tanzania inaweza kunufaika na fursa zilizoko kwao.

Lakini pia nchi yetu inahitaji uwekezaji mbalimbali wa mitaji, hii ni nafasi ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa ambao hufunga safari kipindi hiki ili waweze kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kuzungumza masuala ya uwekezaji.

Pia kwa kuwa nchi yetu ina utalii basi hiyo pia ni fursa nzuri ya kuongea na wadau wa utalii na kuona namna gani tunaweza kuleta watalii wengi zaidi.

Swali langu ni kwamba Miaka minne Mheshimiwa Raisi hajaenda kukutana na Kiongozi yeyote wa Taifa kubwa na wala hajahudhuria kikao chochote cha UN General assembly.

Je safari hii itaenda?

Akienda nitahamia Hargeisa.
 
Wakuu naombeni msaada kuna thread ilitoka juzi story yake Inamhusu tajiri ROMAN IBRAMOVIC na hustling zake , nilijisahau ku- subscribe, mtu anayejua ile thread ilipo pls nisaidie, pia kuna watu walio tag-wa you can direct me pls

Thanks
Kumradhi kwa kuvamia hii thread
daah hadi connection mkuu ndio uipate
 
Kuanzia kwa mtoa mada na wewe mchangiaji, hakuna yoyote mwenye hoja yenye mashiko. Unatamkaje kwa mamlaka wakati tamko unalotoa halina utekelezaji wenye tija? kwenda au kutokwenda hakuna jipya. Bora afanye ziara France au Netherlands au hata Nchi za Scandinavian kuliko UN.

What is the impact of the UN summit in the present world economy? In my views hakuna.
Mbona unaongea kwa woga? Funguka wewe acha kumbwelambwela! Tamka kimamlaka...nini hoja yako?
 
Nimuogope nani? Kuna lugha mtu akiongea unajua anasema kutokea nafasi gani. Uko shimoni. Hizi ni lugha za mkosaji. Toka lini kiingereza kimekuwa issue ya muhimu kwa political leaders?
Hata kama anajua kiingereza, akienda Russia na Ufaransa au China anafanyaje? Tunajua nguvi dola iliyonayo kwenye mambo ya diplomasia?

Bahati mbaya jiwe hawezi kuwa defined as a political leader kwa lugha yeyote ile. Hawezi kwenda kwenye international forum yeyote akaongea kitu kikaeleweka, sana sana ataji-embarass mwenyewe. Na anaujua vizuri ukweli huu; na ndio maana hajathubutu hadi leo kutia mguu nchi yeyote nje ya bara hili.
 
Write your reply...Ataongea na nani na hiyo Enterprentiua yake? hili ni janga la kitaifa.
kumbe ushamba ni ugonjwa sugu!
Wewe nawe unajiita mjanja daaaah dunia ina mengi Sana!!!kwa hiyo kule UN wanaenda wanaojua kubwabwaja kiingereza wengine ambao wewe unawarefer Kama washamba coz hawakijui hawastahili kwenda sio?yaaani hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipoishia?na bado unamlalamikia JPM kusababisha umasikini wako,kwa akili hiyo kweli unastahili kuwa ulivyo!!!!
 
Kuanzia kwa mtoa mada na wewe mchangiaji, hakuna yoyote mwenye hoja yenye mashiko. Unatamkaje kwa mamlaka wakati tamko unalotoa halina utekelezaji wenye tija? kwenda au kutokwenda hakuna jipya. Bora afanye ziara France au Netherlands au hata Nchi za Scandinavian kuliko UN.

What is the impact of the UN summit in the present world economy? In my views hakuna.

Ni kwamba Ngosha ana akili au ni mzalendo kuliko wakuu wa nchi wote waliowahi kwenda huko na wanaoendelea kwenda huko?
Je ni mzlaendo kwa nchi yake kuliko Nyerere, Mandela, Castro, Mkapa, Zenawi, Kruschev, Ahmednejad na wengineo?
Maana wote hao wamekwenda kuhutubia UN General Assembly
 
Wewe nawe unajiita mjanja daaaah dunia ina mengi Sana!!!kwa hiyo kule UN wanaenda wanaojua kubwabwaja kiingereza wengine ambao wewe unawarefer Kama washamba coz hawakijui hawastahili kwenda sio?yaaani hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipoishia?na bado unamlalamikia JPM kusababisha umasikini wako,kwa akili hiyo kweli unastahili kuwa ulivyo!!!!

Tatizo lake ni kubwa zaidi ya kutojua lugha. Intellectual inefficiency ndio shida kubwa kabisa. Anajua pia kuwa waandishi atakaokutana nao huko watamuuliza maswali ya kumuabisha (na kukataa kuongea nao itakuwa aibu kubwa zaidi).
 
Ataenda Pole pole kwa Niaba. Mwache mkuu wetu ana mambo mengi sana ya kufanya
 
Hajui lugha yoyote ya huko duniani huyu atasalimiana na nani? Atabakia bubu muda wote wa kikao. Kwanza hana hata gestures za wanadiplomasia, bora abaki hapa hapa na Bashite asije akatuabisha huko nje
Fikra sahihi uja kwa lugha sahihi.
Mbona viongozi wengine wa mataifa mengine wanatumia lugha zao?
Ili kukomesha ulimbukeni wa kutumia lugha za wenzetu,nashauri Mh.Rais pindi atakapokwenda popote nje ya nchi atumie kiswahili.
Walikamani wapo wengi tu na si hivyo tu siku hizi kuna vyombo maalum vya kutafsiri lugha mbalimbali.
 
Back
Top Bottom