Je, Rais Magufuli atahudhuria kikao cha UN General Assembly cha mwaka huu?

  • Thread starter Missile of the Nation
  • Start date
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
3,745
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
3,745 2,000
Kikao cha UN General assembly kinafanyika tena mwezi wa tisa mwaka huu kama ilivyo ada

Ni mwaka wa nne huu wa utawala wa Rais Magufuli hajawahi kusafiri kutoka nje ya Afrika, tofauti na watangulizi wake, Mheshimiwa Magufuli hajahudhuria kikao hata kimoja cha UN General assembly.
Kikawaida vikao vya General assmebly ni vikao vyenye hadhi ya wakuu wa nchi ambapo mambo mengi huzungumzwa pale lakini ukiacha mbali na hapo huwa ni nafasi nzuri kwa mkuu wa nchi mmoja kupata nafasi ya kuongea na kukubaliana mambo mengi ya maendeleo na wakuu wenzie wa nchi mbalimbali.

Kwa sasa mathalani zao letu la korosho limeyumba, huu ulikuwa ni muda muafaka wa raisi Magufuli kuongea na wakuu wenzie wenye viwanda na masoko ya korosho kuona Tanzania inaweza kunufaika vipi na fursa zilizoko kwao.

Lakini pia nchi yetu inahitaji uwekezaji mbalimbali wa mitaji, hii ni nafasi ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa ambao hufunga safari kipindi hiki ili waweze kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kuzungumza masuala ya uwekezaji.

Pia kwa kuwa nchi yetu ina utalii basi hiyo pia ni fursa nzuri ya kuongea na wadau wa utalii na kuona namna gani tunaweza kuleta watalii wengi zaidi.

Swali langu ni kwamba Miaka minne Mheshimiwa Raisi hajaenda kukutana na Kiongozi yeyote wa Taifa kubwa na wala hajahudhuria kikao chochote cha UN General assembly.

Je safari hii itaenda?
 
W

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Messages
211
Points
250
W

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined May 29, 2019
211 250
Naona watu wengi humu wanakitazama kama kikao tu, wanashau ni a place uanyoweza fanya meeting na wakuu wengi wa nchi tofauti personally na delegation zao.

Hizi huwa ni rahisi sana badala ya kusubiri zile visit za nchi kwa nchi.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
30,498
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
30,498 2,000
Kikao cha UN General assembly kinafanyika tena mwezi wa tisa mwaka huu kama ilivyo ada

Swali langu ni kwamba Miaka minne Mheshimiwa Raisi hajaenda kukutana na Kiongozi yeyote wa Taifa kubwa na wala hajahudhuria kikao chochote cha UN General assembly.

Je safari hii itaenda?
Something tells me, this time atahudhuria.
Mimi ndiye mwandishi wa kwanza private kuripoti from NY, the maiden speeches za maraisi wa Tanzania (Mkapa na Kikwete wakihutubia UN GA, I pray to do the same kwa Magufuli.
P
 
Jp Omuga

Jp Omuga

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
3,167
Points
2,000
Jp Omuga

Jp Omuga

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2012
3,167 2,000
Something tells me, this time atahudhuria.
Mimi ndiye mwandishi wa kwanza private kuripoti from NY, the maiden speeches za maraisi wa Tanzania (Mkapa na Kikwete wakihutubia UN GA, I pray to do the same kwa Magufuli.
P
Kumbe ndo maana..??
I now can easily connect the dots
 
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Messages
2,379
Points
2,000
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2016
2,379 2,000
Something tells me, this time atahudhuria.
Mimi ndiye mwandishi wa kwanza private kuripoti from NY, the maiden speeches za maraisi wa Tanzania (Mkapa na Kikwete wakihutubia UN GA, I pray to do the same kwa Magufuli.
P
Akiudhuria nitag mkuu.
 
Bufa

Bufa

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
5,210
Points
2,000
Bufa

Bufa

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
5,210 2,000
Kule UN kuna mambo ya pembeni yanayoendelea kwenye corridor za diplomasia kuliko kuongea hiyo nusu saa

Kuna kukutana on the sideline na viongozi wenzako wa mataifa mbalimbali mkazungumza ushirikiano

Kuna kukutana na delegations za wafanyabiashara na wawekezaji etc

Ina maana hata Nyerere alipokuwa akienda huko alikuwa anapoteza pesa?
UN ilikua zamani sio sasa. Sasa UN ni genge la ile security council tu wengine wote wanajichosha tu.

Rais kufunga safari ili kwenda kupiga soga kwenye corridors za UN ni ujinga, anaweza kuwafuata hao viongozi wengine rasmi au wao kuja.

Rais yeyote makini hana muda wa kwenda UN Assembly kila siku ili tu aonekane kahudhurina na kupiga story kwenye corridors unless kama ana agenda ya msingi sana, vinginevyo muwakilishi anatosha. Marais wengi tu siku hizi wanatokei huko
 
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
46,416
Points
2,000
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
46,416 2,000
Hivi hili 2015 wakubwa hawakuliona hadi kuanzisha kituo Masaki cha kuibia kura na kumpatia aliyeshindwa? Oneni dhambi yenu imelikosesha taifa fursa mbalimbali kwa miaka mitano na kuleta udumavu wa maisha kwa nchi nzima.
2020 makosa haya yasirudiwe tena
Mr Would yo re write your sentence in English?
 
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Messages
2,379
Points
2,000
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2016
2,379 2,000
No akihudhuria sio nitakutag, bali mimi mwenyewe, I will be the there to report in person, kuripotia JF his maiden spech at UN
P
Ikitokea miujiza akaudhuria ntafuatilia mahojiano yako na yake,asikutoe tu kwenye reli na kukuita njaa.
 
M

Msengapavi

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2008
Messages
7,788
Points
2,000
M

Msengapavi

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2008
7,788 2,000
Kabudi ataenda na kusoma hotuba iliyoandikwa na wataalamu ka akina Mahiga. Uwakilishi makini!
 
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Messages
2,687
Points
2,000
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2018
2,687 2,000
Sio lazima aende kwani ni gharama kubwa kwends huko newyork
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
45,523
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
45,523 2,000
Marais wengi wasiohudhuria vikao hivi ni wale wanaoogopa kutoka nje ya nchi zao na kupinduliwa.

Magufuli bila kutaka anatuweka katika kundi hili.
 
D

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Messages
1,390
Points
2,000
D

drilling

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2016
1,390 2,000
korea ya kusini lini walihudhuria UN na palestina lini walihudhuria UN kuna nchi nyingi hawajafika UN ila wanamaendeleo cuba nao pia hawajafika
 
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
11,270
Points
2,000
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
11,270 2,000
Bora mshamba kuliko mwizi. Nendeni kulima mpaka hatuondoi Rais kirahisi kama mnavyotaka. Tusije kuwapa majambazi bure
Hivi Tz hii nani si jambazi jamani ?! Kama yupo na anyoshe mkono
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
3,745
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
3,745 2,000
Akienda huko atakutana na maswali ya waandishi wa Kimataifa, Kwa nini serikali yako haichunguzi kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda inaelezwa alishikwa na vyombo vya usalama, yuko wapi?. Inasemekana kuna mamia ya Waliouawa Mkuranga je kwa nini serikali yako haichunguzi hili na kama ni uongo kwa nini haikumshitaki aliyetoa taarifa hizo?
Serikali yako inalalamikiwa kukandamiza haki za binadamu na demokrasia kwa nini serikali yako haiheshimu demokrasia kama ilivyokuwa kwa serikali zilizopita?
Hayo ndo maswali atakayokutana nayo huko
 
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
17,322
Points
2,000
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
17,322 2,000
Nani Mjinga?
Yaani Uende Huko Wakati Nyumba Yetu Bado Tunaisafisha Vema. Halafu Kule Kuna Nini
 
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
11,824
Points
2,000
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
11,824 2,000
Rais atakwenda. Ni mkemia na ni Dr!
 

Forum statistics

Threads 1,326,248
Members 509,448
Posts 32,215,758
Top