Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,159
Tumemsikia Waziri wa kilimo, Mheshimiwa Japhet Hasunga, akiongea na waandishi wa habari, akielezea mpango "mpya" utakaotumika katika ununuzi wa zao la korosho, katika msimu ujao
Katika Maelezo yake amesema serikali itasimamia tu zoezi hilo, lakini haitajihusisha na ununuzi huo wa zao hilo la korosho kwa nchi nzima. Akaendelea kueleza kuwa wanunuzi watakuwa wafanyibiashara wa korosho na mtindo utakaotumika utakuwa ni wa wazi na wa kutumia zabuni.
Maelezo ya Waziri Hasunga ni tofauti kabisa na msimamo aliokuwa nao Rais Magufuli mwaka Jana.
Msimamo wa Rais wa mwaka jana ulikuwa kwa serikali kununua korosho yote iliyozalishwa na wakulima na ndicho kitu kilichosababisha kilio kikubwa sana kwa wakulima wa korosho wa mikoa ya Kusini, ambao hawakulipwa na serikali hiyo pamoja na kutamba kufanya hivyo kwa mbwembwe nyingi.
Hata wabunge wa CCM wa kutoka mikoa hiyo ya Kusini walitishiwa kuvuliwa ubunge wao, iwapo wangeendelea kuwasemea wakulima wao wa korosho, kuwa serikali yetu imewadhulumu korosho Zao na hata Waziri Mkuu wetu, Kassim Majakiwa, akatishiwa kupigiwa shangazi zake, iwapo hizo "ngebe" zisingekoma!
Hivi nani hakuona "mbwembwe" za wanajeshi wetu kumiminika na malori yao huko Kusini mwa nchi yetu, walikoamriwa kwenda kwa ajili ya kwenda kusomba korosho hiyo na hata tukaambiwa kuwa hao wanajeshi wetu wana uwezo wa kuzibangua korosho zote zilizovunwa??
Wanasiasa wengi na wananchi kwa ujumla wao walitahadharisha mno kuwa njia hiyo wanayoitumia viongozi wetu wa serikali ya awamu ya tano siyo sahihi
Tujikumbushe tena namna Waziri mkuu, Kassim Majakiwa "alivyoumbuliwa" na Rais Magufuli, pale aliposema kuwa ametafuta kampuni moja ya kichina, ambayo imekubali kununua korosho yetu yote na kuisafirisha
Jibu alilopewa Waziri mkuu, bado tunalikumbuka sisi sote, kwa kuambiwa kuwa aachane na kampuni hiyo ya kichina na Rais wetu akaongea kwa mbwembe na kujiamini kuwa serikali yake itakuwa tayari kununua korosho yote iliyozalishwa nchini kwa shilingi 3,300 kwa kila kilo moja
Vile vile katika sakata hilo la korosho, halikuacha kula vichwa vya watu, akiwemo aliyekuwa Waziri wa kilimo, Charles Kizeba na Waziri wa Biashara Charles Mwijage
Sasa Taifa limepiga U turn kwa kurejea utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa kuwaachia wafanyibiashara wa korosho wanunue korosho za wakulima
Tumejifunza nini katika sakata hilo la korosho??
Kama Taifa tumejifunza kuwa ubabe na maamuzi ya kukurupuka hayalisaidii Taifa hili na badala yake yanaliingizia Taifa hili hasara kubwa!