Kwenye udaktari hakuna shortcut aisee, ni lazima ukomae miaka isiyopungua mitano kwa hapa Tanzania halafu baada ya hapo ni lazima kisheria upige mazoezi(internship) mwaka mmoja. Kwa baadhi ya nchi kama China, Medicine sio chini ya miaka 6.
Daktari specialist maana yake amesomea master's of Medicine na uwe umefanya mazoezi mwaka mmoja(internship), na kusomea Master's of Medicine ni lazima uwe na Bachelor of Medicine kwanza.
Na kama unataka kuwa Specialist utapaswa kufanya kazi kwa at least miaka miwili kwanza(Japokuwa wapo wanaokwepa hili kwa sasa) ndio uende kuusomea. Kwahapa Tanzania Master's of Medicine huwa ni miaka mitatu kwa vyuo vingi na vichache miaka minne. Kwa nchi kama UK, USA, Canada nk. ni miaka minne na kuendelea.
Sio kweli kuwa kuusomea uspecialist ni lazima uende nje ya nchi. Karibu vyuo vyote hapa Tanzania vinavyotoa kozi ya Medicine basi pia vina kozi mbalimbali za specialist. Na kwa sasa zaidi ya 90% ya madaktari wanaosomea uspecialist wanasoma katika vyuo vya Tanzania.
Na huwezi amini kabisa, katika vyuo vya Tanzania, kuna wageni wengi sana kutoka nchi za nje hususani Afrika wapo wanasimea uspecialist.
Kwa utafiti wangu mdogo katika kuwadadisi madaktari wao wenyewe huwa wanadai kuwa, pamoja na kozi ya medicine na uspecialist kuwa ngumu na za muda mrefu lakini ni TAMU MNOO, INA HESHIMA YAKE YA KIPEKEE SANA KIJAMII, NA MARA ZOTE WANATAMANI SANA HADI WATOTO WAO WAJE KUISOMEA(niligundua pia madaktari wengi wazazi wao walikuwa madaktari au wataalamu wa Afya)