Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 5,557
- 8,190
Ni rafiki wa kushibana kwetu kama kwao na kwao kama kwetu, urafiki wetu ni zaidi ya undugu maana tunasaidiana kuliko hata hao ndugu zetu wanavyo tusaidia
Urafiki wetu ulianza na kukua kwa kasi tukiwa school na kwa bahati nzuri kila tukivuka level moja kwenda nyingine tunajikuta tumepangiwa shule moja yani hadi raha hatujawahi kugombana hata siku moja katika urafiki wetu japo hadi sasa wote ni majobless kwa maana hatujaajiriwa pamoja na kumaliza chuo miaka kama 7 iliyopita
Sasa kasheshe ilianza nilipotaka kuoa (mimi nilioa punde tu baada ya kumaliza chuo) nilikuja gundua kuwa mtu niliotarajia kufunga nae ndoa kumbe rafiki yangu nae alikuwa anamtaka maana alikuwa classmate wetu na alivyojua nataka kufunga nae ndoa ni kama alipunguza urafiki japo hakuonesha hisia zake wazi wazi. Hii inshu niliijua kupitia kwa dada yake na aliyekuwa mchumba wangu na sasa mke wangu alinipa story nzima kwani alikuwa akiambiwa na mdogo wake mambo ya mahusiano yake
Mwanzo nilisita na nikataka kugairi kumuoa huyu mwanamke kwa kuhofia kuwa huenda anaweza kutuchanganya wote wawili au nikamuoa kwa shinikizo la ndoa ila kumbe hanipendi anampenda rafiki yangu ila baadae yeye alinifuata na kuniambia yote na kukiri kuwa moyo wake uko kwangu, sikutilia maanan nikawa busy na mdada mmoja mwingine hivi mpaka pale dada yake alipoamua nae kunifuata na kuniambia kuwa nimuelewe mdogo wake kwani alichokuwa anasema ni kweli
Basi nilifanya maamuzi ya kumuoa na mpaka sasa hivi tunaishi vizuri tu japo changamoto za ndoa hazikosekani, ila toka hivyo rafiki yangu hakuoa na hata kwenye Ile harusi yangu hakuja ila mchango alitoa na muda wote huo mawasiliano yalikuwa kawaida japo sio kama mwanzo maana hata kule kutembeleana sasa hakupo
Sasa kanitaarifu kuwa mwezi wa kwanza anafunga ndoa na amenipa muariko na hata ndugu zake wananitafuta ili niwe kampani katika hiyo harusi ( kwa sisi waislam kuna yule anaemsindikiza bwana harusi kama partner wake). Binafsi napenda niende ila kila nikiwaza ya huko nyuma napata ukakasi na ukizingatia hata ya kwangu hakuja vipi hii namimi nisipoenda kuna lawama?
Kwenu wanajamii