Je, nini maana ya 'Impeachment'?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,101
40,764
Je, mtu anapokuwa 'impeached', huwa ina maana gani? Na nini humtokea mtu huyo, lets say Rais kwa mfano.
 
Siyo rais tuu anaweza kuwa impeached.. Impeachment inaweza kutokea pia kwenye nchi ambazo ndani ya mfumo wa uongozi Kuna waziri mkuu..waziri mkuu anaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Mfano mzuri ni Tanzania..nchi zinazofuata mfumo wa presidential democracy kitu Kama hiki ni jambo la kawaida Kupitia mfumo wa "check and balance "
 
Siyo rais tuu anaweza kuwa impeached.. Impeachment inaweza kutokea pia kwenye nchi ambazo ndani ya mfumo wa uongozi Kuna waziri mkuu..waziri mkuu anaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Mfano mzuri ni Tanzania..nchi zinazofuata mfumo wa presidential democracy kitu Kama hiki ni jambo la kawaida Kupitia mfumo wa "check and balance "
Mtu akishapigiwa kura ya kutokuwa na imani nae, nini humtokea? Au nini kinafuata sasa..?
 
impeach
/ɪmˈpiːtʃ/
verb
  1. call into question the integrity or validity of (a practice).
    "there is no desire to impeach the privileges of the House of Commons"
 
Je, mtu anapokuwa 'impeached', huwa ina maana gani? Na nini humtokea mtu huyo, lets say Rais kwa mfano.
Francis da Don,
Impeachment
in the United States is the process by which the lower house of a legislature brings charges against a civil officer of government for crimes alleged to have been committed.This is analogous to the bringing of an indictment(mashtaka) by a grand jury.The impeached official for example President Donald Trump,remains in office until a trial is held.

Soma taarifa ifuatayo ili uweze kupata kiundani juu ya mchakato unaoendelezwa na Baraza la Wawakilishi la Marekani ili kuweza kufanikisha lengo lao la kumuondoa Rais Donald Trump madarakani.


Uchunguzi dhidi ya Trump: Bunge la Marekani limeanza mchakato wa kupiga kura ya kihistoria
  • 18 Desemba 2019
Sambaza habari hii kwa Email,Facebook,Twitter na Whatsapp.

SpViongozi wa Marekani


Rais Donald Trump wa Marekani anakabiliwa na tishio la kuwa rais wa 3 wa Marekani kushitakiwa,pale ambapo baraza la wawakilishi la Marekani litapiga kura ya kihistoria ambayo itafungua milango ya mashitaka dhidi yake.
Wabunge wa Democratic wanatarajiwa kuidhinisha mashitaka mawili dhidi ya rais wa Republican siku ya Jumatano.
Bwana Trump anajandaa kufika mbele ya Seneti mwezi ujao, lakini bunge hilo linadhibitiwa na wanachama wengi wa chama chake na huenda lisipige kura ya kumuondoa madarakani.
Rais ametaja mchakato huo kuwa "jaribio la mapinduzi" na "hujuma".
Katika barua ya kurasa sita aliyoandika mkesha wa kura hiyo, Bwana Trumpa anadai kuwa alinyimwa haki "kuanzia mwanzo wa sakata la kutaka kumuondoa madarakani".
Aliwazuia washirika wake kufika mbele ya kamati ya bunge kutoa ushahidi na pia kupuuzia mbali ombi la kumtaka afike yeye mwenyewe mbele ya kamati hiyo siku ya Jumanne.Spika wa hilo Bunge Nancy Pelosi,alitangaza kwamba,baraza la wawakilishi litapiga kura leo kuamua kuhusu mashitaka yote mawili.


Nancy Pelosi



Baraza la Wawakilishi litatumia moja ya mamlaka muhimu sana, ambayo limepewa kikatiba wakati wabunge watakapopiga kura dhidi ya rais wa Marekani.
Bi Pelosi aliwasilisha ujumbe kwa wenzake wa chama cha Democratic, akisema kuwa Baraza la wawakilishi litatumia moja ya mamlaka muhimu sana, ambayo limepewa kikatiba wakati wabunge watakapopiga kura kuidhinisha vifungu viwili vya mashtaka dhidi ya rais wa Marekani.
Spika huyo pia aliongeza kuwa katika kipindi hicho muhumi katika historia ya taifa hilo, lazima wabunge wailinde katiba ya nchi,dhidi ya maadui wote wa nchi na ndani ya Marekani.
Wabunge watakutana asubuhi 09:00 majira ya huko (14:00 GMT) siku ya Jumatano. Kura hiyo inatarajiwa kupigwa kati ya 18:30 na 19:30.
Bunge linapojiandaa kwa kura hiyo muhimu, Rais Trump atazuru eneo la Michigan kwa hafla ya "Krismasi" pamoja na makamu wake Mike Pence.


Volodymyr Zelensky and Donald Trump meet on the sidelines of the UN General Assembly in New York, September 2019


Trump anashutumiwa kuacha kutoa usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine ili kuilazimisha nchi hiyo imchunguze hasimu wake kisiasa

Mashitaka ni yapi ?
Baada mjadala wa saa kadhaa wiki iliopita, kamati ya masuala ya haki inayoongozwa na Democrats iliidhinisha mashitaka mawili dhidi ya Rais Trump.
Trump anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kuiagiza Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ambaye yuko katika kinyang'anyiro cha kuwania urais kwa tikiti ya chama cha Democratic.
Hatua hiyo ikitajwa kuwa kama njama ya kumpinga asiweze kuwania urais katika uchaguzi wa 2020 wa Marekani.
Trump pia anakabiliwa na shitaka la kufanya njama za kuvuruga uchunguzi wa bunge dhidi yake katika tuhuma hiyo kwa kuwazuia maafisa kutoa ushahidi wao pamoja na kuficha baadhi ya nyaraka.
Vifungu viwili vya mashitaka vinatarajiwa kupitishwa na baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic.
Kama mchakato utakwenda kama inavyotarajiwa kesi yake itafunguliwa Januari mwakani.


Je inawezekana kumvua madaraka rais wa Marekani?
Vi

Je inawezekana kumvua madaraka Rais wa Marekani?
Ikiwa kura ya bunge kama inavyotarajiwa Jumatano sambamba na mirengo ya kisiasa,Bwana Trump atakua Rais wa tatu katika historia ya Marekani kuchunguzwa.
Baadae atashtakiwa katika Seneti, ambako maseneta kutoka vyama vyote wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kutoa hukumu kwa uhuru.Bunge la Seneti linadhibitiwa na chama cha rais cha Republican. Kiongozi wa Seneti Mrepublican Mitch McConnell aliwaudhi Democrats wiki iliyopita aliposema Maseneta wa Republican watashughulikia uchunguzi wa Trump kwa "utaratibu kamili" na na kupiga kura kupinga mchakato.
Chuck Schumer, kiongozi wa walio wachache katika bunge la Seneti alisema :"Kama vipengele vya uchunguzi vitatumwa katika Senati, kila Seneta atakula kiapo cha kutoa 'haki bila upendeleo '.
Kuhakikisha Seneti inaendesha kesi ya haki na ya kweli inayoruhusu ukweli wote unajitokeza ni jambo muhimu."
Mapema Jumanne, wakili binafsi wa Bwana Trump Rudy Giuliani alionekana kuthibitisha kwamba alifanya juhudi za kumuondoa balozi wa Marekani nchini Ukraine, Marie Yovanovitch, ili kutoa fursa kwa ajili ya uchunguzi.Hilo linaweza kuwa jambo la maana kisiasa kwa Bwana Trump.
Bwana Giuliani aliliambia gazeti la New York Times kuwa alimfikishia Bwana Trump "mara kadhaa" taarifa juu ya namna Bi Yovanovitch anaweza kuwa alihusika kwa njia fulani katika uchunguzi.
"Nilihitaji Yovanovitch atoke," Bwana Giuliani aliliambia gazeti hilo la New York.


Shutuma za Trump


White spacer

Marais wawili wa Marekani wamepigiwa kura ya kutokuwa na imani ni Andrew Johnson mwaka 1868 na Bill Clinton mwaka 1998 lakini katika matukio yote mawili bunge la Seneti halikupiga kuwalazimisha kung'atuka madarakani.
Richard Nixon alijiuzulu Agosti mwaka 1974 wakati ilipojitokeza wazi kwamba anapigiwa kura yakutokwa na imani naye na kung'atuliwa madarakani na Congress baada ya kutokea kwa kashfa ya Watergate.
Makundi ya waandamanji wanaotaka Trump apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye, wameandamana katika miji mikuu kote nchini Marekani leo Jumanne.


Raia was Marekani wamegawanyika kuhusu mchakato mzima wa uchunguzi wa kutaka kumuondoa madarakani Rais Trump


Raia wa Marekani wamegawanyika kuhusu mchakato mzima wa uchunguzi wa kutaka kumuondoa madarakani Rais Trump.
Wengi wao walikuwa wameshika mabango yanayosema "Muondoeni Trump" na kuandika hashtagi #ImpeachTrumpNow.
Wachambuzi wanasema kwamba Marekani imegawanyika.
Tovuti ya kisiasa ya Marekani inaonesha kuwa kura za maoni 538 za kitaifa, zinaonesha kwamba asilimia 47 ya watu wanaunga mkono mchakato wa Trump kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, huku asilimia 46.4 wakipinga mchakato huo.
 
Je, mtu anapokuwa 'impeached', huwa ina maana gani? Na nini humtokea mtu huyo, lets say Rais kwa mfano.
impeachement is the way of removing irresponsible leader who get power under democratic system(election) ambapo bunge hupiga kura kumpinga rais

inauhusiano na vote of no confidence kwa waziri mkuu ambapo hii humwondoa waziri mkuu madarakani

it is applicable only to democratic states, kwa nchi zisizo na democracy (autocratic) hutumia njia ya mabavu kumwondoa kiongozi asiye wajibika kwa wananchi wake
 
Bwana Trump anajandaa kufika mbele ya Seneti mwezi ujao, lakini bunge hilo linadhibitiwa na wanachama wengi wa chama chake na huenda asipige kura ya kumuondoa madarakani.
Rais ametaja mchakato hu


What if haya yangekuwa yanatokea hapa kwetu, waanzilishi wa sakata wangekuwa salama?
 
Back
Top Bottom