Mohamedex121
JF-Expert Member
- Jan 27, 2022
- 1,688
- 3,142
Habarini wakuu! Toka majuzi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi hili suala la wajasiriamali kuwa wengi nyakati hizi tofauti na miaka ya zamani let say 90's.
Kipindi cha miaka ya 90's wajasiriamali na wafanyabishara walikuwa wachache sana, yaani kukuta duka la Mangi moja mtaa mzima au kijiji kizima ilikuwa ni kawaida sana. Mzee wangu anakumbuka nyakati hizo,, wateja walikuwa wanapanga foleni kwa wenye maduka, biashara zilikuwa chache, sijui hili inamaanisha nini au kipindi hicho watu walikuwa Bize na kulima? Ama walikuwa Bize na kusoma ili kuja kuajiriwa?
Katika miaka hiyo nahisi watu suala la biashara kipindi hicho haikuwa kipaumbele chao, watu walikuwa Bize na masuala ya elimu kusoma ili kuajiriwa serikalini ama sekta binafsi au pia inawezekana watu wengine walikuwa vijijini wako Bize na kilimo na pengine walishindwa kuja mjini na hivo kuliacha kundi la watu wachache kufanya biashara ama wengine huwa wajasiriamali hasa maeneo mbalimbali ya miji.
Miaka ya 90's hakukuwa na soko la kariakoo ilo mnaliona miaka hii karibuni, bali soko kubwa la jiji la Dar lilikuwepo posta na mnazi mmoja.
Sasa sijui nini kulipeleka kukuwa kwa masoko mengi ya wafanyabishara nyakati hizi ukianzia soko la kariakoo, tegeta, Manzese, Buguruni, Mbagala, ubungo (ilikuwa zamani), na hata hapa Mbezi mwisho nilipo, wajasiriamali tumejaa kila kona. Ukipita mitaa ya Mbagala kila nyumba inafremu la duka la Mangi na sio Mbagala tu hata huku mitaani maduka ni mengi. Mama ntilie ndio usiseme wemejaa kila kona, kuna wanauza chai na uji wakitembeza kwenye vijiwe na majumbani achilia mbali wale wamama wanaouza mihogo akitembea mtaa kwa mtaa, mama zangu wa mbogamboga wamejaa kila mahali.
Yaani siku hizi kila mtu ni mjasiriamali haijalishi huyu kuajiriwa ama hajaajiriwa , haijalishi huyu ni mtoto wa au ni mtu mzima yaanj naona madogo siku hizi nao wamo kwenye gemu ya ujasiriamali, achilia mbali wanasiasa, wazee , wamama nao siku wamechangamka tofauti na wamama wa miaka ya 90's waliokuwa wakishinda nyumbani, ila siku hizo wote tupo nao masokoni kila mtu ni mjasiriamali aliyesoma na asiyesoma wote tupo kwenye gemu la ujasiriamali yaani daah shiiiiidaaaa hili ni bomu soon nahisi litalipuka tu kama zilivyo kwenye ajira za wasomi.
Huwa najiuliza baada ya haya yote ya kila mtu kuwa mjasiriamali je nini kitatokea miaka ya baadaye je kutakuwa na mfumo mpya na option mpya za watu kufanya shughuli nyingine tofauti na ujasiri na kama zitakuwepo ni zipi hizo?? Watu watakuwa na mishe gani mbali na ujasiriamali?
#Natanguliza_shukurani_wakuu