Ujue umekaa kipombe pombe,
Na wanakumulika, halafu hata mke huna, upo tu kama mhuni
Dada sio hivyo ,nilioa miaka ya nyuma kidogo na alhamdulilah mwanamke walipata kumuona pamoja na wanangu wawili.
Dada sababu za kihisia kwa wifi yako nilipatwa na kesi nikawekwa ndani nimekaa hapo Keko magereza kwa muda wa mwaka na miezi kadhaa .
Nilipotoka rasmi nikapewa talaka na mke wangu mzuri ,nilikuwa na vimali vya urithi hapa Dar es salaam kutoka kwa baba pamoja na baadhi ya vitu katika mkoa huu ,ikabidi vigawanwe .
Dada kidogo nikapewa Mimi ,kikubwa akapewa yeye kwakuwa yupo na watoto ,bad enough siku si nyingi baada ya hayo akadai hata watoto si wangu .
Nikajipigiliza kwa watoto kila Mara nionanane nao walau wajue Mimi ni baba yao ,dada watoto wakaanza nao kunikataa kwa kusema wao mbona wanajua Mimi si baba yao wanaye baba mwingine .
Dada ,wifi yako kaolewa Sasa na aliyemuoa ndiye anasema ni baba wa wanaye .
Uhuni wangu uko wapi hapo ? Natamani kuoa Ila nitamuoa Nani ilihali bado nampenda mke wangu sijaamini kuwa ameniacha naamini labda atarudi panapo majaaliwa .
Dada siishi kihuni ,ninazo heshima zangu na ninayo mipaka yangu na wanakijiji Ila ni vile dunia inaamua kunihukumu kwa mfumo huu .