Je, ni vyuo gani vinaongoza kwa kutoa wasomi walioiva vizuri Tanzania?

Nimepata kuwa kwenye Gymnasium sköla tulikuwa tunaangalia ubora wa vyuo hasa vya Afrika, ni aibu

Kwa Tanzania UDSM baada ya maprofesa kuingiza siasa na kushindana kuandika mathesisi,
Kimeshuka sana, japo Kwa TZ hakina Mpinzani ,
Pili chuo wali ki dismantle kwa kukigawa gawa mara UCLAS MUHAS vikaondoka,

Ukija upande mwingine, IFM, DIT, SUA na Mzumbe wako vema sana, baada ya UDSM

Udom siasa na UCCM mwingi sana., hata miundombinu si ya kutosha kwa baadhi ya Faculties


Britannica Encyclopedia
 
Kwa sasa Chuo kikuu kinachotoa wahitimu Bora ni Open University of Tanzania. Chuo hiki kinaenda na mabadiliko ya Technology,kina platform moja ya kujifunzia online inaitwa "Moodle" ambayo nadhani hakuna Chuo chochote hapa Nchini kinayo! Pili Wanafunzi wa OUT wanasoma kwa mfumo " Kuku wa Kienyeji", wanajitafutia materials na hawasomi handouts " madesa" kama Vyuo vikuu vingine!
Na hivyo kwa Wanafunzi wa OUT ambao wako serious wako deep sana!
Tatu,nafasi ya degree za " chu.pi " hakuna kwani Instructors na Wanafunzi kukutana ni mara chache sana !

toa uchafu wako hapa
 
Mtoa mada unazingua kabisa...Kwa jinsi ulivyowasilisha mada yako ni dhahiri kabisa pasi na Shaka jibu tayari unalo au unataka jibu la aina gani kuhusu chuo Bora ni kipi... Nikushauri tu Kama still upo chuo mpaka Sasa tumia muda kusoma kwa juhudi uwe vizuri hasa katika practicing uwe bora wewe Kama wewe na sio kuteletea mada mufilisi Kama hizi...
 
Uwezo Wa mwanafunzi na uwezo Wa chuo wakati mwingine ni vitu tofauti unaweza soma chuo chenye sifa kubwa lakini uwezo wako ukawa Mdogo kuliko aliyesomea chuo cha kawaida tumeshuhudia katika mazingira ya kawaida tu msomi anaishindwa kazi anakuja kuifanya mtu ambae elimu yake ni ya kawaida sana
Thats point!!! uzuri wa elimu ni kutumikiakile ulichojifunza na siokwamba unamiliki cheti cha chuo gani, kunakijana ana CPA lakini ni mweupehata Bank Reconciliation kutayarisha hawezi ila anaonekana bonge lamuhasibu kwa vile tu ana CPA. Kubwa ni uwezo wa mwwanachuo baada yakuipata gamba nakuingia mtaani ni elimu gani aliyokuja nayo
 
Hiki ni chuo cha masela na ma sister du wanaosoma degree kuongeza bei yao sokoni
Siyo kweli! Ni chuo Kikuu pekee Tanzania na east Africa kinachofundisha na kujihusisha na maswala ya Ushirika. Karibu ujionee maarifa mapya na namna ya kufungua ubongo wako uweze kufanikisha maendeleo yako binafsi na ya nchi.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
Unazungumzia katika profession ipi mkuu?
Km katika kozi za afya ni Aghakan ile ni international university.Kuna Hindumandal pia. Kairuki kikifuata.
 
Mkuu Elimu ya chuo kidogo imekaa kimtindo ambao mwanafunzi anapaswa kujiongeza kwa Africa huku kwa kweli kwa swala la kwenda na curriculum bado sana utashnagaa modules zilipo kwenye vyuo vyetu ziko outdated, Usmart wa graduate unakuja pale tu akiwa mtu wa kujiongeza haswa kusoma vitabu ili kupanua uwezo out of modules zake hakuna chuo nchini apa kina shape graduate kweli aka meet ata soko la Africa tu kila sehemu nikujiongeza
 
Dar es salaam maritime institute, Africa viwili tu kingne magharibi njoo kwa mabaharia pale watu wachache wanajua nn wanafanya Unique africa achana na mbwembwe za udsm na aridhi
 
Unazungumzia katika profession ipi mkuu?
Km katika kozi za afya ni Aghakan ile ni international university.Kuna Hindumandal pia. Kairuki kikifuata.
Hapa Bongo Kuna chuo kinaitwa Hindumandal au vipi mkuu
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.

1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?

2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?

NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
Hakuna aliejibu hii hata Mimi mwenyewe. Hii ndio post bora kabisa. Maprofesa wengi ukiwatoa chuoni hawajui chochote kuendesha maisha. Wakistaafu ni kupata stroke na kufa baaaasi.
 
Back
Top Bottom