Je ni sawa kumsaidia mwenzi wako?

Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,036
309
Habari zenu wana JF popote pale mlipo,ni matumaini yangu Mungu wetu mwema anawapigania daily,
Wapendwa naomba msaada wa mawazo yenu kwa wale mliokuwa tayaru mmeoa/olewa na wale walio bado pia wanaweza kutoa michango yao hata kujifunza pia,swali ni;

-Je ni sawa kumsaidia mwenzi wako katika maandalizi ya harusi yenu?mfano
  • Mahali not less zan laki 5..............
  • Gharama ya nguo cheapest ni laki nane gauni la bibi harusi,bado viatu,hereni,na vitu vidodovidogo,Bado saloon (bibi harusi,matron,wasimamizi) =1M...........
  • Pete(uchumba,ndoa 2) =laki 600............
  • ukumbi(pesa zinatoka ktk kamati but ili upate kumbi mapema ni vyema ukatoa hela yako kwanza zen vikao vikianza unarudishiwa)
Je kama mwanamke/mwanamme kuna haja ya kumsaidia mwenzako ktk gharama hizi?mfano salooni nijilipie mwenyewe,viatu hereni,mkufu etc?au mwanamme anatakiwa kufanya kila kitu mwenyewe?au unalipia gharama zen unamdai?
Naomba michango yenu ya mawazo.
 
Unaweza kumsaidia nitumie neno zuri kumshauri kulingana na bajeti ya mfuko wake lakini si kwa kila kitu.
 
MAHALI NI JUKUMUA LA MWANAMME. lakini mengine yote mnaweza kukaa na kusaidiana! kwa kufanya hivi, mtajenga msingi mzuri wa kusaidiana mambo mengi kwenye nyumba yenu.
 
kuna jamaa mmoja alinitumia meseji akasema....
''ukiwa kama ndugu wa karibu, nakuomba unisaidie kama laki2 hv nimalizie kulipa mahari''....we mtu, kuoa uoe ww, mahari nikulipie mm, si ujinga huo?

mahari hata hivyo sion sababu ya kuifanya iwe kuuubwa, ingekuwa vema bi harus aulizwe af ashauriane na mwenzake ambayo ataweza kuilipa...hata ukiifanya kubwa kias gan, bado haiwez kulinganisha na thamani ya mke au gharama za ulezi toka utotoni n.k....
nadhani mahar ifanywe kama shukrani kwa wazazi.
 
Mahari alipe mwanaume
mambo mengine mwaweza kusaidiana kama unaweza
ni vizuri mwanaume akiona kwamba budget inazidi mfuko bora kuandaa sherehe kuendana na michango/kipato chake
isionekana mwananmke amechangia zaidi kwenye ndoa pale mtafaruku ikiianza ndani ya nyumba masimango yanajitokeza ooohhh nimekuoa mie ndio niligharamia sherehe nzima
 
Kwa kuwa mataka kujenga familia moja, mnaweza kusaidiana. Ila kuna vitu ambavyo mwanamke hapaswi kufanya, mfano suala la mahari, tena mimi naona inategemea na makabila, ila kwa mtazamo wangu mahari mwanaume atafute mwenyewe hata ndg zake wasimsaidie, ila vitu vingine nyoooooote wamsaidie, mahari ndiyo inatoa muelekeo hasa kwa ndg kwamba kijana wao kweli amejiandaa kuoa, siyo kuwakaza wazazi eti wakulipie wengine wanakaa vikao vya ndg kabisa eti upitishwe mchango wa mahari, sasa mahari uchangiwe, arusi uchangiwe, nguo za bibi arusi uchangiwe, wewe utakuwa umejiandaa kwa lipi, wanaume kuweni serious mnapofikiria kuoa, jiandaeni kwanza kifedha kabla ya kupeleka wazo hilo kwa ndg au wazazi ili kuwapunguzia vikao na michango!!!!
 
ndo maana nazifagilia ndoa za dini flani. Very cheep! Mahari anataja binti. Mnafanya sherehe ya kibingwa ili kuutangazia umma kuwa umeoa/kuolewa na huyu ndo mme/ke wangu. Then mnapigwa tafu ya mkwanja wa kuanzia lyf. Sio magharama yoote hayo afu baada ya sherehe mnaanza kuangaliana.
 
Pearl My dearest!

Kutokana na kupanda kwa gharama za maisha mnaweza kusaidiana kwa kufanya sherehe/shughuli zote siku moja!

(engagement party + Kitchen party + sendoff party + harusi party + mahari party + kalaile katai party +e.t.c) = Ndoa Party!
 
MImi nadhani, vitu kama mahari na gauni alipe mwanaume still, but wewe as mwanamke you can help by selecting/opting for cheaper alternatives maybe.
 
Mahari alipe mwanaume
mambo mengine mwaweza kusaidiana kama unaweza
ni vizuri mwanaume akiona kwamba budget inazidi mfuko bora kuandaa sherehe kuendana na michango/kipato chake
isionekana mwananmke amechangia zaidi kwenye ndoa pale mtafaruku ikiianza ndani ya nyumba masimango yanajitokeza ooohhh nimekuoa mie ndio niligharamia sherehe nzima

Black Woman
Nakufuatilia sana
Una mawazo mazuri sana
Ila naomba u-AMPLIFY mwandiko wako ili tukupate bila shida
Sisi wengine mimacho yetu imesha-dead uwezo
 
Mwaya kama mapenzi ndio haya na uwezo najua hana namsaidia kwa moyo wote..y not jamani sie kwetu kule india wanawake wanatoa mahari wakishindwa wanatolewa na kakake bwana harusi lipi jipya hapa...swala muwe na furaha siku ya mwisho pearl wala usjali mwaya mapenzi ya sasa wenye hela nao shida tupu bora tusaidiane tuishi kwa amani milele
 
Natamini iwe kitradition zaidi mwanaume anigharamikie kwa uwezo wake, yaani anipe pete, nguo na mahari alipe. hata kama nina uwezo huo ningependa bwana harusi wangu anigharamikie. mie nitajiandaa kwa ajili ya KP na send off
 
Back
Top Bottom