Je, ni sawa anachotaka kufanya?

Je, ni sawa anachotaka kufanya?

mtoto mpole

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2010
Posts
678
Reaction score
148
Fatuma ana mume wake wa ndoa kwa mda wa miaka minne sasa, ana kazi nzuri, wamejaaliwa mtoto mmoja ana 3years, wanavumiliana kwa mengi. Wanafanya mambo yao pamoja wanasaidiana ila Fatuma amekua akiona charts za mumewe na wanawake tofauti kwenye simu anavumilia anajipa moyo kwamba watakua wanataniana. Saa ingine anafanya uchunguzi wake anamuuliza mumewe yaani si mdada wa kukurupuka na haamini kama mumewe anaweza kumsaliti.

Fatuma ana rafiki yake anaitwa Hidaya ni rafiki sio sanaaa japo ni marafiki sasa amegundua ya kwamba Hidaya amezaa na mumewe tangu january kajua na ana ushahidi wote kuhusu huyu baby boy wa Hidaya na mumewe japokua hajamuuliza mumewe hajamwambia chochote sasa anajipanga aombe uhamisho akafanyie kazi Morogoro ni mfanyakazi wa local government anaipenda ndoa yake.

Hataki kuiacha ila kamchukia mumewe sana anataka kukaa nae mbali na hataki kumwambia chochote mumewe

Je yupo sahihi?
 
Kitendo cha huyo dada kuhamia Moro ndiyo kuivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe anatakiwa akae aingee na mumewe ila hizo chuki jamaa si avuta huyo alizaa nae wakati huyo mkewe akiwa Moro


Sema huyo Mke nae anataka akiwa Moro akalipe kisasi kwa huru na hapo ndiyo twasema kuwa "Kosa halirekebishi Kosa"


Hapo muhimu ni kukaa chini sio huo upuuzi wa kuhamia Moro eti ana mchukia,Mumewe kadondoka dhambini Mke nae anakwenda jidondosha tena dhambini

Mwambie akae na mumewe na watu wa heshma wayazungumzee vzr
 
wayazungumze kwa pamoja,ila asihame nyumbani maana atampa nafasi mmewe kuendelea na huo uchafu wake na yeye pia(mwanamke) atajiwekea vishawishi au atataka kulipiza kisasi
 
Kukimbia tatizo sio kulitatua. Amweleze mumewe ili ausikie ukweli kutoka kwake, akishafanya hvyo aje tena tumpe ushauri wa hatua inayo fuata kulingana na kitakachokua kimejiri
 
Atahama ila mawazo yatakua home.hapo atakua amebadilisha basi ila safari ileile.
 
atoe "unyonge" inauma ukiumizwa, lakini haifai kufa kikondoo awe muwazi.
 
Acha nipite tu aisee

Nyie wanaume matendo mnayotenda mnasababisha mioyo ya wake zenu igande juu yenu halafu mnataka mke akae ajenge ndoa? Ajenge nini na juhudi za mume zimeibomoa?

Au mnadhani wake zenu wana mioyo ya mawe?

Ingekua fatuma anatembea na wanaume na kutiwa mimba na rafiki wa mumewe, reaction ya mumewe ingekuwaje?

Fatuma afanye anayojisikia kuponya moyo wake, ila amwambie mumewe ili ajue kuwa anajua kazaa na hidaya

Then afuate kile moyo wake unataka
 
Sidhani kama atakuwa sahihi kuondoka kuacha ndoa yake! Ndo kwanza atampa nafasi azae na idaya ama mtu mwingine mtoto mwingine !! Akae chini amweleze mumewe ndipo maamuzi yafuate!!
 
Kwahiyo bado anaipenda sana ndoa yake ila anamchukia mume wake?

Akubali tu matokeo, wasaidiane kulea otherwise atapoteza ndoa.
 
Kwanza kitu cha kwanza anapaswa kujua huyo mumewe bado ana mapenzi nae?? Then kitu cha pili mmewe yupo tayari kuomba msamaha na kuendelea kuwa na mkewe coz inawezekana aliteleza tu,as long as mwanamke yupo tayari kuilinda ndo yake naamini anaweza kusamehe from there wazungumze wasameheane na mwanaume aaahidi kutoa rudia tena then wapange jinsi gani wataweza kuendelea kuishi wote.
 
Nawaza kama fatuma angetembea na rafiki wa mumewe na kupewa mimba mume angekaa na kumsamehe? Jamani tusipende kucheza na hisia za mtu huyo mwanamke ana moyo kama walivyo wengine na mwanaume bora angezaa na mwingine na si rafiki yake
 
1. Fatuma..Hidaya...so am assuming mume naye ni Juma. Bwana Juma awaoe wote tu na kwakuwa ni mashosti natumai wataishi vizuri tu.

AU

2. Bi Fatuma atekeleze maazimio ya moyo wake ila ajue tu kwa kufanya hivyo ni sawa na kujiandikia talaka.

3. Bwana Juma amefanya kitendo cha kinyama sana ambacho kama angefanyiwa yeye walah talaka tatu zingemfuata bi Fatuma.

4. Ni ngumu sana kwa bi Fatuma kuendelea kuishi na mumewe huyo (naona ni kama mzazi mwenzie tu) huku akiwa na maumivu moyoni...kuna siku ataamka. kisu cha moyo usiku. Ni vyema tu akauvunja ukimya.

5. Reaction ya mumewe ndiyo itakayo dictate line of action sahihi kwake kuichukua. Otherwise huenda ikawa hata huyo mtoto wa Hidaya hana uhusiano wowoteee na bwana Juma.

#semaNaye #usioneSoo

PM Moderator,
Mentor.
 
Last edited by a moderator:
Asifanye hivyo maadamu ushahidi anao aongee na mumewe ikishindikana aite wazazi wasaidie
ndoa ni ngumu sana jamani inahitaji uvumili wa hali ya juu vinginevyo inakua ngumu
 
Asimwogope mumewe, atafute siku ambayo anamuona mumewe yuko ktk mood nzuri azungumze naye kwa upole na kumueleza jinsi alivyoumia na kumkumbusha ahadi yake ya kuwa mwaminifu siku ile walipofunga ndoa.
 
Back
Top Bottom