Je, ni sahihi mpenzi wako kufahamu kipato chako unachokipata?

Mfumo dume at work...! Kuficha kipato chako kwa mkeo sio jambo la busara kwa sababu a)itamfanya mkeo ashindwe kupanga bajeti ya nyumba-maana hajui kiasi gani kinaingia-
 
Hizi ndoa hizi. Yani watu wanawachukulia wake zao kama ma housegirl. Kwa nini wife asijue kipato chako? Tatizo nyie mmeshajiwekea mwanaume ana ela kuliko mwanamke ndio maana mnaleta dharau.

Kama sijuhi kipato chako nitawezaje kupanga matumizi ndani?

Kwa mtaji huu mkaoe tu mashambani!
Hiyo ulitakiwa uwe umeisoma zamani sana.
 
Unatakiwa ufahamu yote unayoongea, lakini usiongee yote unayoyafahamu. Kwa ajili ya kumaintain heshima na jina ni vema kutoweka wazi kila kitu. si lazima mtu ajue una nini sasa ingawa unatakiwa uwe responsible father kwa familia na mkeo. Kama mama anapata reasonably mahitaji yake wala hatakuwa na haja ya kujua mshahara wako.
Kwa mimi sioni ulazima, ila nitawajibika kama baba kwa familia.
 
Ngumu kutoa ushauri.. maana inategemea na akili ya mkeo anapenda maendeleo au ndio walewale
 
Mfumo dume at work...! Kuficha kipato chako kwa mkeo sio jambo la busara kwa sababu a)itamfanya mkeo ashindwe kupanga bajeti ya nyumba-maana hajui kiasi gani kinaingia-
Kimsingi hii pointi haina mashiko sana kama ambavyo walioitoa wangependa tuamini. Kwanza kuna suala la bajeti inayozungumziwa hapa, sina hakika wasemaje wanakusudia bajeti gani kwa sababu kuna bajeti za aina nyingi. Je ni bajeti ya misosi na mavazi, bajeti ya ujenzi au ni bajeti kwa ujumla wake kwa maana ya kila kitu. Vyovyote iwavyo bado hakuna uhusiano wowote wa kupanga bajeti na kujua mshahara kwa sababu ili mtu upange bajeti unachotakiwa kujua ni kiasi gani umepewa. Kwa hiyo basi utaona kuwa mke haitaji kujua mshahara ili apange bajeti bali anachotakiwa kukijua ni kiasi gani atapata kutoka kwa mume kwa mwezi period. Kwa hiyo wakuu tutoe hoja nyingine sio ishu ya kupanga bajeti, kwa sababu hata hao wasiojua mshahara wanaachiwa fedha kiasi na bajeti wanapanga.

My Take:
Mimi mke wangu kujua mshahara sio tatizo, japo hii haina maana kwamba aupangie matumizi :)
 
mim sio goalkeeper na kamwe sitakakuwa,usijeshangaa ukijua mm ni mpiganaji kuliko ww.
Na kwani ni ajabu mwanaume kufukuzwa?au kwa vile umezoea hao ambao ukiwaachia kodi ya meza tu umemaliza hawahitaji kujua mengine?hao ambao idara wanayoimudu ni jikoni tu?YES ,ninao uwezo wakumfukuza mwanamume akiwa ni kikwazo cha maendeleo na malengo yangu.
kipato changu nitamueleza na mim nitahitaji kujua chake ili tujue ni jinsi gani kipato chetu wote kitatupatia vipi maendeleo.
kutojua kipato cha mwenzangu ni kikwazo cha maendeleo ya familia yetu,lengo la kujua ni ili kama kwa mf. hatuna nyumba mm kama mama nijue tutajibana vipi hadi tujenge n.k.

hahaa eti ukiniachia tu HELA YA MATUMIZI mengine nisitake kujua,bahati mbaya mm siishi kwa kula kuvaa na kulala tu nataka mambo makubwa ya maendeleo hivyo usiponishirikisha ktk kipato chako utakua umenizuia kutafuta maendeleo ya familia yetu na ndio nitakutimua sbb mtu mwenye mawazo kama haya ni wale wanakazi nzuri lkn miaka yote kapangisha huko magomen na hata kivitara hana,mm nataka mwanaume mwenye kiu na akili ya maendeleo kama MIMI, pamoja na kuwa umesema situmii oblangata lkn u r very wrong my dear na kwa mawazo haya uliyonayo si a jabu una kipato kizuri lkn huna maendeleo.

Sawa Mamaa, Wanawake Mnaweza, ni vizuri ukifahamu kipato cha familia ili uweze kupanga matumizi yake. Usipofahamu unaweza kumshauri 'me wako kufanya jambo kubwa kuliko kipato chenu, akaona kama unadhalilisha vile. Lakini kama unafahamu, utashauri kulingana na kile kilichopo. Mimi sioni kama kuna shida, hata mimi yule mdogo wako huwa namwambia na kila mshahara ukiongezeka anakuwa "updated".
 
Rafiki yangu Cheusimangla unaonekana umekasirika au unakuwaga na hasira sana. Pole sana, namefurahia mawazo yako lakini kuna haja ya kupunguza ukali, nafikiri wawili mnaopendana mtajuani vizuri kwa sababu mtakuwa mmeshasomana kwa hiyo mnaweza kujua jinsi ya kushare mapato yenu. Kwa kawaida maisha hayana formula, coz we all differ in thinking and priorities. Ila kunahaja ya kushirikishana katika kutafuta maendelea>>. Nitakutafuta siku tuongee zaidi....poa!
 
sio dhambi kuwajulisha wake zenu mishahara yenu bt ni dhambi mkiwaficha wake zenu mishahara yenu! Ukimjulisha mkeo, atapanga budget vizuri sana!
 
hivi mnajua wanawake ni watu hatari sana kwenye maisha ya waume zao mwanamke akijua kipato chako na kujua mambo yako mengi akimpata mwanaume mwingine akawa anatoka naye ni rahisi sana kumweleza kila kitu anacho kijua kuhusu mume wake ni bora akujue nusu nusu na hata muda mwingine asikujue kabisa akiwa anakaa na mashoga zake story ni kwamba mume wangu kwa kweli siwezi kumsimlia kwa jambo lolote lile kwa sababu aeleweki kuliko kuwa muwazi kwa mkeo kwa kila kitu ni wachache sana ambao wako makini lakini kwa asilimia kubwa ni wepesi kuropoka hasa wanapokuwa wanakula uroda na wanaume wengine,
 
kumwambia mshahara ni lazima. Usiishie hapo, panga nae bajeti ya matumizi na mgawane majukumu ya kuisimamia bajeti. Hela za madili si lazima ajue maana hazina uhakika sana. Mimi kwenye bajeti yetu kibuku hamna fungu lake lakini kila jioni napata ya afya. Hakuna malalamiko, payslip yangu anaipata kila mwezi. Na ikitokea imejensi hela natoa nje ya bajeti. Heshima inazidi.
 
punguza hasira cheusi mangala, kubali kuwa chin ya mumeo mana we ni mkewe! Kwa suala la kumfukuza bwanaako hapo utakuwa uko wrong, umetumia lugha ya ubabe, afu ukipelekea sana akili yako kwenye pesa na kujua kipato cha mumeo hutampenda na hutampa mapenzi ya dhati, utawaza pesa tu. Mambo mengine unapotezea tu. Right?

not right and not okay.
sina jazba,huwa siandiki nikiwa na jazba.
hehehe wakati wa kulala naweza kukubali kuwa chini lkn ktk maswala ya maendeleo ya familia sitaki kuwa juu zaidi yake lkn naona ni muhimu usawa ukiwepo.
tatizo nikiongea kama wanaume wanavyoongea naitwa mbabe,hapo pananipa huzuni,mara ngapi wanaume wanasema yule mwanamke asipojirekebisha namfukuza lkn mm nikisema nitamfukuza naitwa mbabe?:biggrin1::biggrin1:
haya sitamfukuza lkn nikimbembeleza aniambie mshahara wake akiendelea kunificha nitamuomba aondoke akatafute wanayeendana.
tatizo tuna mawazo tofauti,narudia kwamba nataka kujua jumla ya kipato chetu wote kwa lengo la kujua jinsi ya kupanga mipango ya maendeleo ya family yetu,akinambia ndo nitampenda zaidi lkn
mume niliyeapishwa naye kanisani akinificha kipato chake si nitajua kuna mengi sana anayonificha hivyo hata penzi langu kwake linaweza kupungua.Right?
 
Sawa Mamaa, Wanawake Mnaweza, ni vizuri ukifahamu kipato cha familia ili uweze kupanga matumizi yake. Usipofahamu unaweza kumshauri 'me wako kufanya jambo kubwa kuliko kipato chenu, akaona kama unadhalilisha vile. Lakini kama unafahamu, utashauri kulingana na kile kilichopo. Mimi sioni kama kuna shida, hata mimi yule mdogo wako huwa namwambia na kila mshahara ukiongezeka anakuwa "updated".
mdogo wangu ana bahati kweli.
lazima nyie mtakua na maendeleo sana.
ngojea na mim nimuombe mungu anipatie mume atakayeamin uwezo wa akili yangu ktk kutafuta maendeleo.
endelea hivyo hivyo mtafika mbali sana.
 
haaaaaaa! We cheusi mangala naomba niwe mumeo mama yangu!! Unakili wewe!!!! Hei! Sijawahi ona! Hakyanani!! Nikoradhi kwa lolote lile utakalo sema ila ndo sina kipato kizuri shule yenyewe ndoogo hali mbaya ndo nawaza kuja kuponea kwako au ndo utantimua ntajitahidi kujituma na kazi.cheusi mangala
 
Ndg ndoa ni uhusiano kati watu wa2 na hao wa2 si wa2 tena bali wamekuwa mmoja hutaki kuwa msiri tambua ya kuwa ww na yy nikitu kimoja hamtakiwi kufichana
 
hivi mnajua wanawake ni watu hatari sana kwenye maisha ya waume zao mwanamke akijua kipato chako na kujua mambo yako mengi akimpata mwanaume mwingine akawa anatoka naye ni rahisi sana kumweleza kila kitu anacho kijua kuhusu mume wake ni bora akujue nusu nusu na hata muda mwingine asikujue kabisa akiwa anakaa na mashoga zake story ni kwamba mume wangu kwa kweli siwezi kumsimlia kwa jambo lolote lile kwa sababu aeleweki kuliko kuwa muwazi kwa mkeo kwa kila kitu ni wachache sana ambao wako makini lakini kwa asilimia kubwa ni wepesi kuropoka hasa wanapokuwa wanakula uroda na wanaume wengine,
Kudadadadeki
 
not right and not okay.
sina jazba,huwa siandiki nikiwa na jazba.
hehehe wakati wa kulala naweza kukubali kuwa chini lkn ktk maswala ya maendeleo ya familia sitaki kuwa juu zaidi yake lkn naona ni muhimu usawa ukiwepo.
tatizo nikiongea kama wanaume wanavyoongea naitwa mbabe,hapo pananipa huzuni,mara ngapi wanaume wanasema yule mwanamke asipojirekebisha namfukuza lkn mm nikisema nitamfukuza naitwa mbabe?:biggrin1::biggrin1:
haya sitamfukuza lkn nikimbembeleza aniambie mshahara wake akiendelea kunificha nitamuomba aondoke akatafute wanayeendana.
tatizo tuna mawazo tofauti,narudia kwamba nataka kujua jumla ya kipato chetu wote kwa lengo la kujua jinsi ya kupanga mipango ya maendeleo ya family yetu,akinambia ndo nitampenda zaidi lkn
mume niliyeapishwa naye kanisani akinificha kipato chake si nitajua kuna mengi sana anayonificha hivyo hata penzi langu kwake linaweza kupungua.Right?
Cheusi cheki PM
 
haaaaaaa! We cheusi mangala naomba niwe mumeo mama yangu!! Unakili wewe!!!! Hei! Sijawahi ona! Hakyanani!! Nikoradhi kwa lolote lile utakalo sema ila ndo sina kipato kizuri shule yenyewe ndoogo hali mbaya ndo nawaza kuja kuponea kwako au ndo utantimua ntajitahidi kujituma na kazi.cheusi mangala
Mkuu umejiunga ili upige mdogo mdogo kwa bibie :) . Angalia sana hizi avatar zisikuchanganye

Kumbuka: No trespassing, violators will be shot and survivors will be shot again.
 
Back
Top Bottom