Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,497
- 26,986
Salamu wakuu!
Imekuwa kawaida kusikia watu wakisema kuhusu kujilipa mshahara, binafsi kwa mara ya kwanza nilisoma hii nadharia kwenye moja ya vitabu hamasishi vya uhuru wa kifedha.
Kitabu hiki ni maarufu kwa jina lake, ”The Richest Man in Babylon”. Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu, yeye anasisitiza hakikisha 30% ya kila unachokipata inakuwa ya kujilipa wewe.
Mfano kipato chako ni LAKI MOJA kwa mwezi, basi tenga 30,000/- kwa ajili yako. Kisha kiasi kinachobaki ndo kitumike kwenye shughuli zingine mfano gharama za familia kwa kadri ya majukumu yako, ikiwemo 10% ya Mungu [hili sikumbuki kama alilitaja, lakini ni muhimu].
Binafsi nikiri kuwa sijawahi kujilipa. Huenda kwa kutokujua namna gani nijilipe, au ni visingizio tu vya kipato kutokukidhi.
Kwa maana kila shilingi ikipatikana tayari inasubiliwa kumaliza au kusogeza jukumu fulani. Hata ikitokea isitumike muda huo basi itakuwa kuna lengo mahsusi lenye kuhitaji pesa ndefu, hivyo itakaa kwa muda ili tu kusubiri hesabu itimie.
Kwa ajili yangu na familia, nikimudu mahitaji ya muhimu kwangu naona kama nipo sawa tu.
Sasa naomba tupeane mawazo na uzoefu, kwa wale wenye nia au waliofanikiwa kujilipa. Unachora wapi mstari kwamba hiki kibubu ni kwa ajili yangu tu na kile ni cha familia?
Je, kujilipa ni kujiwekea akiba ya baadae au ni kujihudumia vema kwa muda huo? Mfano kujistarehesha kwa vitu roho inapenda, na hapo iwe nje ya kile ambacho unatumia na familia yako mwenyewe?
Natamani watu wanielewe ila sidhani kama ninaweza kuandika zaidi ya hivi, pengine kupitia mawazo ya wadau wengi tutaweza kuelewa vizuri.
Ni kwa jinsi gani huwa unajilipa?