Je ni sahihi kuita CRDB Bank....ACB Bank...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni sahihi kuita CRDB Bank....ACB Bank...?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LAT, Feb 5, 2011.

 1. L

  LAT JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kwa mtazamo wangu ninaona hapa kuna repitition ya maneno...kama vile inavyotokea mtu kusema barabara ya mandela road

  tumeona mabenki mengi yakiandika kwenye official docs na mabango yao kama vile

  CRDB Bank...Cooperative and Rural Development Bank Bank
  ACB Bank...........Akiba Commercial Bank Bank
  BOA Bank ........ Bank of Africa Bank

  haya mabank yaliyo sahihi ni kama Standard Charted Bank..... Barclays Bank... Exim Bank..... Mkombozi Commercial Bank

  nadhani udhaifu huu upo kwenye kutumia vifupisho vya maneno...mimi nahisi sio sahihi
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa CRDB imesajiliwa na kutambulika hivyo CRDB Bank Plc.

  Hizo zingine ni makosa kuongeza neno Bank ......iwe KCB na sio KCB Bank
   
 3. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Umenena kweli mkuu.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu...hapa nazungumzia maana ya jina na si uhalali wa kiusajili...kwani wao BRELA hawaangalii maana ya jina ipo sahihi au ...lakini ukweli unabaki kwamba CRDB Bank inaendelea kurudia rudia maneno
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umeona enh................?
   
 6. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 280
  Swanglish Kaka!!!
  Barabara ya Mandera Road..............
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Hiyo inaitwa sheng'
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndg yangu kwa taarifa tu,CRDB haikuitwa CRDB bank kimakosa kama ambavyo baadhi ya wachangiaji wanavyofikiri bali jina hilo lilikuja baada ya CRDB ile ya wakulima kubinafsishwa.
  Ilipo binafsishwa ilibadili mwwelekeo kutoka Cooperative Rural Development Bank {kwa maana yake halisi ya Benk ya maandeleo Vijijini} na kuwa benki ya wafanyabiashara tena wakubwa ambao kimsingi huwezi kuwakuta vijijini.
  Hivyo kuendelea kutumia 'CRDB' haingekuwa na maana na vilevile kutumia neno lingine lingekuwa na athari kubwa kibiashara kwa walio inunua. Ndio maana wakaamua kuita 'CRDB bank' na kwa sasa CRDB inayotumika sasa haina maana yoyote zaidi ya kutumika kama jina tu yaani huwezi kutoa kirefu cha CRDB Bank ya sasa kwa maana ile iliyokuwa inatumika zamani na huenda hakuna kirefu chochote cha neno hilo bali ni jina tu kama 'Athuman au John'
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu...hatusemi ni imeandikwa kimakosa.... tunachosisitiza ni repitition ya maneno... na kwa taarifa yako...haya ni makosa ya mwanzo yaliyofanyika wakati wa kuanzisha bank bila kuangalia jina lililo fupi na kuleta maana ile ile..... hii ni kutoshirikisha sector ya wataalamu wa branding au brand name developers....majina kama ali au john yote yapo kwenye kamusi na yana maana yake...hata majina ya kiasilia yana maana yake.... jee maana ya CRDB kama jina ni nini.....? na hawa ACB Bank ..... na hao KCB Bank.....

  ndugu yangu lazima tukubali udhaifu huu.... kwani walio tunga majina kama standard bank au Trust bank....au Eco Bank waliangalia mbali kwani jina la bank linatakiwa liwe fupi kulitamka
   
 10. regam

  regam JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usiwe mbishi wa kuelewa. Umeelezwa kwamba crdb si ile uliyokuwa unaifahamu kama cooperative and rural development bank. Hii ya sasa haina kirefu chochote. Kama walichangia wenzangu, crdb bank lilisajiliwa kama jina na biashara kama majina mengine. Sasa ukisema eti brela wanatakiwa kuuliza maana ya kila jina la kampuni utakuwa unakosea. Wao wanaposajiri cha kwanza ni kuangalia kama hakuna biashara yoyote yenye jina kama hilo. Walifanya hivyo kwani iliyokuwepo ilikuwa inaitwa crdb na sio crdb bank.kama kuna wengine wanaokosea sawa lakini kwa crdb bank ni sahihi. Kwani jina kama john lina kirefu chake? Aaaah bana usituchote akili!
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  naendelea kujifunza mambo asa hili la barabara ya mandela road ujue tunatamka kla cku bila kuangalia upande wa2
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mkuu nashawishika kuamini kuwa uelewa wako ni mdogo
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kuwa makini kusoma post kabla ya ku reply...nilchosema ndicho hicho hicho unachosisitiza.....hivyo basi CRDB haina kirefu kwa sasa hivi...... udhaifu wa kupata corporate brand ni ule ule na ndiyo maana CRDB ikakurupuka baada ya kuona udhaifu huu na wakati jina limeshajulikana... hivyo basi ikaelekea kufoji tu...ukweli utabaki vile vile there is repitition kwa kuangalia maana ya jina.... huwezi kwepa mantiki ya kirefu cha CRDB
   
 14. N

  Nalonga JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mkuu LAT,Technically unachokichangia kina ukweli mkubwa,Jamaa wamekurupuka ili waendelee kutumia Brand name CRDB ambayo imeshauza sokoni,kwani kimantiki hakuna jina la la kampuni ambalo halina maana yoyote,hivyo kwa minajiri ya biashara ilikuwa vigumu kuingia na new brand name kwani ingewacost sana katika kuanza kuitangaza,hivyo ili wasionekane kama kuna kurudia rudia maneno ikawabidi wauwe maana iliyobebeka katika neno CRDB.Hivyo inabidi tukubali tu kwamba kuna bank inaitwa CRDB.....na hiyo(CRDB word is meaningless)
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu nashukuru kwa kuboresha mantiki.... nadhani nilikua ninaweweseka kutoa maelezo yanayogonga haswaaa ukweli na inasikitisha sasa kusikia maneno yanayoeleza kwamba short form ya letters CRDB inafananishwa na jina JOHN
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  LAT tokea mwanzo ulipaswa ukubali kwamba hizo ACB, KCB n.k ni makosa kutamka ACB bank au KCB Bank.
  Na wao ukiangalia nyaraka zao hawaandiki ACB Bank bali wataandika kifupi cake au jina kwa kirefu.

  Kwa upande wa CRDB Bank wala usilazimishe kwamba walikosea, hiyo Coop Rural Dev Bank ni tafasiri yako ukiamini inaendelea kuwepo kwa vile imewahi kuwepo. Kama unataka maana ya kila herufi kawaulize wenye Bank maana kuna biashara nyingi zimesajiliwa kwa kufupisha majina sasa tukitaka kupeana majibu hapa ndani itakuwa kazi ndefu.

  Tunachokubaliana na wewe ni namna ambayo wengi tunakosea kutamka baadhi ya mambo kama Drphone kagusia "barabara ya mandela road" au wengine husema "still bado" kama ilivyo kwa "repeat again".

  Kwa muktadha huo hoja yako ina mantiki isipokuwa CRDB Bank
   
Loading...