Mpaka umesema tayari ni hatua ya kwanza kukubali una tatizo.
Acha nikupe some tips zinaweza kukusaidia.
TENGENEZA PICHA KUBWA YA MAISHA YAKO, YAPE MAISHA YAKO PURPOSE,usiiishi tu kwa kuwa unapumua
Jiulize wewe ni nani na unataka kuwa nani baada ya muda gani!
Unajiona wapi baada ya miaka 5, hakikisha unavunja vunja hiyo miaka mitano kuanzia minne kushuka chini mpka hapo ulipo leo.
kisha utaona unapaswa kufanya nini ili ufike pale.
NI KWELI JITIHADA HAISHINDI KUDRA, ila OGOPA SANA KUPATWA NA KUDRA BILA KUWA NA JITIHADA WALA MIPANGO.
Af u need People!
Wewe sio kisiwa , hata kisiwa kinakaa karibu na maji!
Watu wanatutoa, watu wanatupa deals, watu wnatusikiliza, watu wanatupenda, watu wanatufariji.
Sio Ujanja hata kidogo kuwa bila watu!
Your network is your networth.
Usingizi sana au kukosa usingizi kabisa ni dalili Ya kukata tamaa na maisha!
Sio swala la kuwa romantic, we hata mwenyewe hujipendi utawezaje kuonesha mapenzi?
Af acha kutizama mafanikio yako ukijilinganisha na mafaniko ya wengine
HII ITAKUCHELEWESHA SANA!
Wewe pambana na wewe mwenyewe!
Kabla ya kutizama mwingine kafaulu wapi,we jitizame ndani yako unafanya nini kizuri!
Kisha jiboreshe ZAIDI!
Si rahisi kufanya kila kitu vizuri, chagua maeneo ya kuwa best at!
Miaka 30 bado sana kukata tamaa na maisha!
So yes kuna eneo unatakiwa ulifanyie kazi pia practically!
UTARATIBU WAKO WA SIKU/WIKI/MWEZI
FUNGU LA KWANZA (UTARATIBU WAKO KWA SIKU)
1. Ikifika saa tatu , Zima simu ingia kitandani jilazimishe kulala
2. Kula chakula mapema, kabla ya kulala kunywa maji
3. Asubuhi amka mapema hata kama huendi kazini, kunywa maji ya vuguvugu, fanya mazoezi hata dk 10
4. Andika malengo ya siku hiyo, hakikisha unayapa time frame na unajikagua iwapo umetimiza
5. rudia namba tip namba 1-4 kila siku
FUNGU LA PILI (UTARATIBU WAKO WA WIKI)
Kila Jumatatu Weka malengo ya wiki nzima, yakague kila jumapili
Ona wapi umefaniukisha/umekwama, nani amekukwamisha, nani angeweza kukusaidia (Utaona gap yako)
Malengo ya wiki inayofuata ni kuunga pale uliona gap hasa ya watu kupitia mawasiliano.
FUNGU LA PILI (MWEZI )
Weka malengo tar 01 jikague tar 31.
Ninaposema malengo usiwaze sijui kujenga nyumba sijui kununua gari , Malengo makubwa sana ni mazuri lakini yanakatisha moyo na tujione hakuna tunachofanya
Kuna mengi ya kukusaidia, ILA HEM FANYA HAYA KWANZA !
af uje ulete feedback baada ya siku 90.
Ukifanikiwa tu hii umetoboa