Biological make up. Utashauriwa sana ilabkama uliumbwa hivyo huto ni wewe hakuna mfano wako. Unawezabjitahidi sana kubarika ukawezabkwa kipindi flani ila baadae utarudi kwenye default settings zako. Huyo ndio wewe mkuu, kwenye hayo yote hakuna hata moja unalovunja sheria ya nchi. Hivyo kama una kereka na ulivyo fanya namna ubarike, ukishindwa baki ulivyo. Huyo ndio wewe.
Kwenye hizo sifa mimi nina zaidi ya tano. Ila huyu ndio mimi. Mimi sio mtu wa kujali kabisa pengune hata zaidi yako. Mimi watu wanaweza sikitika juu ya jambo baya, ila mimi kama nitasikitika basi ni usoni tu ila moyo hauhisi chochote. Unaweza nipigia simu nikaiona ila kama nakujua huna cha maana naweza nikakutafuta hata kesho na apologies nyingi. Na ni muda wote mimi niko na simu. Nafanya biashara hivyo simu yangu muda wote ninayo, na kipigwa namba ngeni najua ninteja nipokea chap, ila kama nakujua na huna issue ya maana hapo nitaitazama tu.
Mwaka juzi mwishoni mama aliumwa sana tukawa tunamuuguza. Wenzangu walikua na majonzi na mishtuko mimi wala nilikua nafanya vile inavyopaswa kuwa kiume zaidi bilabkuonesha masikitiko. Mwaka jama mwanzoni mama alifariki. Nilisimama vizuri kama mtoto wa kiume tukafanya mazishi tukamaliza. Baadavya msiba shemeji yangu aliniambia, "shem wewe ni jiwe sana, wakati wenzio wana taharuki wewe unachukulia vitu kawaida tu, kuna muda wenzio hawakuwa na utulivu kabisa na hawakujua wafanye nini, ila wewe neno lako moja tu lilikua linatoa mwanga na watu wanapona mioyo" siku huo ndio nilijua kuwa kumbe hali yangu sio hasara ni faida kwenye baadhi ya mambo.
Mkuu usihofu, huyo ni wewe huna haja ya kubadirika.