Je ni maneno ya kweli au ni propaganda?

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Kuna baadhi ya wauzaji au madalali wa Magari wanasema Gari ambayo ni 4Wd sio nzuri kwasababu zifuatazo.

1. Zinakunywa sana Mafuta
2.Utengenezaji wake unakuwa mgumu.

Hapo nazungumzia kwa upande wa Zanzibar,tena kwa baadhi ya Yadi ambazo ni maarufu.

Kwa mfano Dalali anaweza kukuambia kwamba Gari aina fulani ni nzuri lakini shida yake ina 4Wd labda uitoe.

Mimi sio mtaalamu wa Magari wala sio mpenzi wa kuendesha Magari sana,lakini inapobidi na hapa sio kwamba naihitaji hapana! nataka tu nipate elimu.

Kwanza sielewi maana ya 4Wd kwamba kazi yake ni nini? kuna faida gani kuwa na Gari ya namna hiyo,lakini tofauti kati ya Gari ambayo sio 4Wd ni ipi?

nimejiuliza pia kwamba,je ikiwa mafundi wanaweza kutoa huo mfumo wa 4Wd si wataiharibu Gari?😳

Shukran
 
Kuna baadhi ya wauzaji au madalali wa Magari wanasema Gari ambayo ni 4Wd sio nzuri kwasababu zifuatazo

INATEGEMEA NA GARI YENYEWE

1. Zinakunywa sana Mafuta
TOA NENO SANA.

2.Utengenezaji wake unakuwa mgumu.
INATEGEMEA NA KILICHA HARIBIKA KIPO WAPI.

Hapo nazungumzia kwa upande wa Zanzibar,tena kwa baadhi ya Yadi ambazo ni maarufu.
ZNZ %95 YA GARI ZA 4WD ZINATUMIKA MJINI NA SIO VIJIJINI/MASHAMBA, LAZIMA WATASEMA INAKULA MAFUTA 7BU GARI YA SPEED 180km/h, ATATEMBEA SPEED ISIOZIDI 50km/h NDANI YA WIKI NZIMA. NB, GARI YEYOTE ILE INATUMIA MAFUTA MENGI MIJINI KULIKO NJE YA MJI.

Kwa mfano Dalali anaweza kukuambia kwamba Gari aina fulani ni nzuri lakini shida yake ina 4Wd labda uitoe.
KAMA HUIHITAJI HUITUMII KULINGANA NA GARI HUSIKA, SIO LAZIMA KUITOA, NA KUITOA NI GHARAMA PIA.

Mimi sio mtaalamu wa Magari wala sio mpenzi wa kuendesha Magari sana,lakini inapobidi na hapa sio kwamba naihitaji hapana! nataka tu nipate elimu.
ELIMU: KUTEGEMEA NA GARI, INAWEZA IKAWA NI AINA MOJA, ILA 01 IKAWA NA MFUMO WA 4WD NA NYENGINE ISIWE NA HUO MFUMO, WEWE UNAPOINUNUA YADI, UTACHAGUA NICHUKUE YENYE MFUMO AU LA, KULINGANA NA MATUMIZI YAKO, PIA BAADHI YA GARI HUO MFUMO UNACHAGUZI, KUUTUMIA UNAPOHITAJIKA AU KUTOUTMIA KWAKUA HAUHITAJIKI KWA WAKATI HUO.

Kwanza sielewi maana ya 4Wd
KIREFU: FOUR (4) WHILL DRIVE.
MAANA: NI MFUMO KTK GARI UNAOLIENDESHA/KUVUTA/KUSUKUMA GARI KWA KUTUMIA MATAIRI/MARINGI YOTE MA NNE (4).

kwamba kazi yake ni nini?
KUENDEDHA GARI KWA KUTUMIA MIGUU/MATAIRI YOTE MANNE.

kuna faida gani kuwa na Gari ya namna hiyo,
FAIDA YAKE INAKUA NA NGUVU SANA NA KIWEZESHA GARI ISIKWAME KTK SEHEMU KOROFI KAMA VILE KTK MATOPE, MAWE, MAPOROMOKO, MABARAFU AU HATA KTK MCHANGA MWINGI, NA KAMA ITAKWAMA/ITANASA UKIWA UNATUMIA 2WD, Eg, ZA MBELE, BASI UTARUHUSU MFUMO WA 4WD, NA ZA NYUMA ZITAFANYA KAZI NA GARI TOTOKA KWENYE MKWAMO BILA KUTAFUTA WATU WAJE KUSUKUMA GARI LAKO.

lakini tofauti kati ya Gari ambayo sio 4Wd ni ipi?
2WD + 4WD
4WD NI GARI ITUMIAYO MATAIRI MANNE YA NYUMA NA MBELE KUENDESHA GAR, WAKATI
2WD NI GARI ITUMIAYO NATAIRI MAWILI YA MBELE AU NYUMA KUENDESHA GARI.

nimejiuliza pia kwamba,je ikiwa mafundi wanaweza kutoa huo mfumo wa 4Wd si wataiharibu Gari?😳
NDIYO, WANAHARIBU GARI ILA WATAKUFANYIA KILE WEWE TAJIRI MWENYE GARI UNACHO KITAKA WAKURIDHIDHE NA UTALITUMIA GARI LAKO KAMA KAWAIDA.

Shukran
AHSANTE.
 
Inategemeana kuna 4wheel ya moja kwa moja ambayo hauwezi kuibadili (yani inakuwa ni 4wheel automatic mda wote ipo automatic).

Na kuna 4wheel ambayo ni Manual Hii Ipo Sana Kwenye Suzuki Escudo Zile Old Model Kabisa Zina Gia Kabisa Ya 4wheel na Hasa Ukiikuta Ile Yenye Engine ya 4 cylinder Yenye Cc 1780 Mafuta Haitumii Mengi Tofauti na Ile V6.

Na Kuna 4wheel Ambayo Ni Automatic any Time hii Ipo Sana Kwenye Noah Sr50 yenye Engine Ya 3s-fe yani mda wote Gari inakuwa ni automatic huna option ya kujichagulia iwe 4wheel au 2wheel Hii Wengi Hulalamika Hutumia Mafuta Mengi Japo Mimi Napingana Nao Maana Nimeitumia haili mafuta Mengi kiivo ni kawaida tu.

Ni Hayo Tu
 
Kuna baadhi ya wauzaji au madalali wa Magari wanasema Gari ambayo ni 4Wd sio nzuri kwasababu zifuatazo.

1. Zinakunywa sana Mafuta
2.Utengenezaji wake unakuwa mgumu.

Hapo nazungumzia kwa upande wa Zanzibar,tena kwa baadhi ya Yadi ambazo ni maarufu.

Kwa mfano Dalali anaweza kukuambia kwamba Gari aina fulani ni nzuri lakini shida yake ina 4Wd labda uitoe.

Mimi sio mtaalamu wa Magari wala sio mpenzi wa kuendesha Magari sana,lakini inapobidi na hapa sio kwamba naihitaji hapana! nataka tu nipate elimu.

Kwanza sielewi maana ya 4Wd kwamba kazi yake ni nini? kuna faida gani kuwa na Gari ya namna hiyo,lakini tofauti kati ya Gari ambayo sio 4Wd ni ipi?

nimejiuliza pia kwamba,je ikiwa mafundi wanaweza kutoa huo mfumo wa 4Wd si wataiharibu Gari?😳

Shukran
Hakuna gari inayokunywa supu.. hiyo gari ni 4WD au AWD

Gari ya aina gani ambayo unataka kununua?
 
Back
Top Bottom