je ni lazima kuhesabiwa? SENSA

swamy

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
252
143
Kumekuwa na mvutano wa maneno kutoka kwa viongozi wa serikali na viongozi wa kidini.... dini ya kiislamu, katika kijiji cha DONGOBESH mkoani manyara wilaya ya mbulu, watu wamekuwa wakitishiwa na polisi tangu saa 6 usiku wa tarehe 26, wanagongewa wakikataa kufungua mlango na wakisema hawataki sensa, polisi wakishirikiana na makarani wa sensa, wanawaambia musipofungua tunawatuhumu kama nyinyi ni majambazi, na tutawapeleka polisi kuwashtaki, Haya yamefanyika leo GUEST ya NILE DONGOBESHI......, JE NIKIULIZA WANASHERIA ANAEKATAA KUHESABIWA ANASTAHILI KUSHTAKIWA!!!!!!!!!!! NA HUKMU YAKE NINI?.
 
Kuhseabiwa ni lazima vinginevyo serikali haitaweza kuwa na vigezo vya kupanga mipango ya maendeleo. Hata hivyo, kwa serikali fisadi na do nothing kama yetu wakati mwingine sensa ni zoezi la kulia pesa ya wafadhili. Maana ukiona mipango ya maendeleo hakuna zaidi ya maendeleo hewa. Idadi ya watu inaongezeka kama mvua na hakuna anayehoji. Hili limekuwa tatizo la Afrika kwa ujumla. Ninapoandika nchi kama Kenya yenye ukubwa chini ya nusu ya Tanzania ina watu sawa na Tanzania. Uganda kadhalika. Rwanda na Burundi ndiyo usiseme. Laiti serikali za nchi hizi zingekuwa serikali kwa maana ya neno zingejifunza tokana na sensa.
 
Kumekuwa na mvutano wa maneno kutoka kwa viongozi wa serikali na viongozi wa kidini.... dini ya kiislamu, katika kijiji cha DONGOBESH mkoani manyara wilaya ya mbulu, watu wamekuwa wakitishiwa na polisi tangu saa 6 usiku wa tarehe 26, wanagongewa wakikataa kufungua mlango na wakisema hawataki sensa, polisi wakishirikiana na makarani wa sensa, wanawaambia musipofungua tunawatuhumu kama nyinyi ni majambazi, na tutawapeleka polisi kuwashtaki, Haya yamefanyika leo GUEST ya NILE DONGOBESHI......, JE NIKIULIZA WANASHERIA ANAEKATAA KUHESABIWA ANASTAHILI KUSHTAKIWA!!!!!!!!!!! NA HUKMU YAKE NINI?.

Unajua serikali hii hapo ndipo ilipochemka ok utamlazimisha ngo'ombe kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji! Hivi wamefikiria kwamba hao wanaowalazimisha wanaweza wakatoa data za uongo katika hilo dodoso lao?!
Hii ni sawa na 1+1-2
 
Back
Top Bottom