Je! Ni kweli wahehe wanakula mbwa?

Je! Ni kweli wahehe wanakula mbwa?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Wakuu hivi ni kweli kabila la wahehe wanakula mbwa? Navyojua mimi hizi ni story za watu vijiweni hakuna mhehe anaekula mbwa. Kipindi cha ukoloni wajerumani waliwauliza wahehe kwamba wanapenda chakula gani? Wakajibu wanapenda kula madogi wakimaanisha maharage. Ndipo wazungu wakachukulia moja kwa moja kuwa wahehe wanakula mbwa. Kama kuna mwenye data zaidi atujuze hapa.
 
kumbe majibu unayo. wanakula mbwa hawa hapa
article-2661107-1EB3C20F00000578-493_634x408.jpg

Z
 
kwa kweli siwezi jua ila kuna kipindi nilikuwa maeneo ya kule ilembula njombe, nilishangaa kuona nyumba 1 ya udongo ikikaribia kuanguka, na ilikuwa imezungukwa na mbwa kama 10 mpaka 15, nikauliza hawa mbwa wanafanya nini nikaambiwa ni wa mwenye nyumba hiyo, sasa nyumba yenyewe mvua zikianza sijui kama itapona hawa mbwa wa nini, nikajua kweli hawa mbwa ni kitoweo, wanavyowakamata na kuwachinja hapo sijui, huo ni ufahamu wangu tu
 
Ni kweli tunakula shida yako nini.
Ni kama wagogo wanavyokula panya wao wanaita 'fudi'
 
hapa dunian wanyama wote wanaliwa, inategemea wewe umekulia mazingira gani na nyama inayopatikana maeneo hayo. jamii ya wahadzabe wanakula wanyama wote isipokuwa fisi tu, tena nyama ya nyani ndio inaheshimika sana kuliko zote!
 
kwa kweli siwezi jua ila kuna kipindi nilikuwa maeneo ya kule ilembula njombe, nilishangaa kuona nyumba 1 ya udongo ikikaribia kuanguka, na ilikuwa imezungukwa na mbwa kama 10 mpaka 15, nikauliza hawa mbwa wanafanya nini nikaambiwa ni wa mwenye nyumba hiyo, sasa nyumba yenyewe mvua zikianza sijui kama itapona hawa mbwa wa nini, nikajua kweli hawa mbwa ni kitoweo, wanavyowakamata na kuwachinja hapo sijui, huo ni ufahamu wangu tu
mzee, huko ilembula njombe hawaishi wahehe, wanaishi wabena. wahehe waliokuwa wanakula mbwa ilikuwa zamani sana, inawezekana hata wewe ulikuwa haujazaliwa. na maeneo waliyokuwa wanakula mbwan i maeneo ya uhehe halisi (Wahehe wanatofautiana, wale wa mkwawa na wahehe wa dabaga). wale wa dabaga wanaitwa wa milimani hao hawana historia ya kula mbwa na hata lugha kidogo wanatofautiana na wahehe wa Tanangozi, isimani, kalenga hadi mafinga. ukiangalia utakuta Dabaga ina chakula kingi sana, matunda mengi sana na ukijani mbichi lakini huku tanangozi ilula hadi mafinga kuna ukame fulani uliowafanya hawa wahehe halisi kula hadi mbwa kwasababu hakukuwa na wanyama wengine na chakula ni scarce sana hadi leo. ukipita hata leo mimawe tu imejaa kwenye milima hakuna ardhi nzuri. ila ukienda dabaga kuna vyakula na wanyama wa pori wapo na wanafuga ng'ombe. Tanangozi walikuwa wanakula mbwa, ifunda, mafinga, kalenga ,isimani etc.

kaka yangu ameoa mtu wa asili ya dabaga na tulishaenda kutoa mahari huko na ninakufahamu sana. wahehe wa dabaga na wahehe wa kalenga (mkwawaz) ni tofauti na hao tu ndio waliopigana vita enzi zile, hao wa milimani wanaitwa wadzungwa na hawana historia yeyote ya kula mbwa au kupigana vita. hivyo kwa uzoefu nilionao naweza kusema wahehe halisi wale wa kwenye vitabu wa kalenga, ifunda, mafinga, ilula, isimani, isimila etc walikuwa wanakula mbwa kweli lakini ni zamani, kizazi cha sasa hakuna hata mbwa anayeweza kuliwa. vilevile ni utani tu wa makabila, mhehe hata kama amezaliwa mwanza na hajawahi kufika iringa ukimwuliza kuwa unakula mbwa atakwambia ndio kwa utani tu lakini uhalisia sio kweli kwasasa, zamani walikula sawa.
 
Siyo kweli,hawa ndugu hawali mbwa.By the way vipi yule Mbunge wenu Mh.Mgimwa bado yupo au imetosha???
 
nimekupata mkuu
 
Ndio Mbwa tunakula, hata wewe unaweza kula
Panya
Nyoka
Konokono

ILIMLADI USIONE KINYAA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom