Je, ni Kweli Tumefika Mwisho wa Mapambano ya Ufisadi na Utawala Mbovu?

Je, ni Kweli Tumefika Mwisho wa Mapambano ya Ufisadi na Utawala Mbovu?

Mfilisti

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
3,727
Reaction score
19,465
Ni jambo la kusikitisha kuona jinsi wagombea wa nafasi za juu katika siasa za leo wanavyonyamazishwa au kwa Maksudi kabida kutoonyesha msimamo dhahiri kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi na utawala mbovu. Hoja hii muhimu inapuuzwa, hakuna Mgombea yoyote mwenye kuonyesha hatua atakazo fanya kupambana na majizi na mafisadi na wananchi tunabaki na wasiwasi kuhusu hatma ya mustakabali wa taifa letu.

Tukirudi nyuma Kampein za uchaguzi mkuu 2010 Chama cha CHADEMA kilionyesha dhamira kuu ya kupambana na Mafisadi mara watakapoingia madarakani. Japo walishindwa kuendeleza ajenda hii pale 2015.

2015 tuna kumbukumbu za kampeni za marehemu Rais John Magufuli, aliyeonyesha dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi / kuimarisha utawala bora na nidhamu ya kazi. Ilikuwa ni hatua ya kihistoria, ikionyesha kuwa serikali inaweza kuchukua hatua madhubuti dhidi ya tatizo hili. Hata hivyo, utekelezaji wa ahadi hizo umeonekana kusuasua na kushuka kasi mara alipoingia madarakani na hata baada ya kifo chake.

Kwa sasa, taifa letu linaonekana kupotea polepole kutokana na ukosefu wa viongozi wenye hofu ya kweli na hasira inayostahili dhidi ya ufisadi na utawala mbovu sio watawala CCM au vyama vya Upinzani. Wote wanaimba nyimbo zao wanazojua wenyewe, najiuliza Taifa linakwenda wapi?

Tunahitaji viongozi wapya wenye dhamira thabiti na ujasiri wa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi na utawala mbovu sio hawa wachumia matumbo yao na Makundi yao yanayowaweka madarakani. Viongozi wa mfano, wasioogopa kuwajibika, wanaoweza kuleta mabadiliko halisi yanayolenga kuinua taifa letu na kuimarisha imani ya wananchi.
 
Ufisadi umekuwa ndiyo nembo ya taifa la Tanzania. SI unaona jinsi Samia anavyohonga pikipiki na baiskeli nchi nzima?
Kwa nini hadi Upinzani wameweka kando hizi Ajenda?
 
Ndugu yangu hoja nzuri lakini nani anasikiliza? Hayupo hata mmoja. Wanachopanga wao ni kuuma sana sana na kupuliza kidogo! Baada ya miaka mitano ijayo mboga yote itakuwa imeisha au imerithishwa Moja kwa moja kwenye vizazi vyao, watakomba, kunywa mchuzi mpaka na kutafuna na mifupa pia.
 
1754799568453.jpeg
 
Kwa nini hadi Upinzani wameweka kando hizi Ajenda?
Kati ya haki na rushwa kipi ni adui mkubwa kuliko kingine?

Kwa kukusaidia tu, rushwa ni adui wa haki (kama kuna haki ), lkn bahati mbaya haki yenyewe hakuna. Ndiyo maana upinzani umejikita kuitafuta haki kwanza.... No reforms no election.
 
unalalamika nini kila mara uko upande wa hayo mqfisadi ya mtandao
Mimi ni mtu neutral, sifungamani na upande wowote. Kutokuwa upande wako haimaanishi kuwa niko upande ule mwingine. Panua wigo wako wa kutazama mambo.
 
Back
Top Bottom