Je, ni Kweli madaktari wanapojua mgonjwa atakufa humficha na kuwaambia ndugu zake tu?

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
2,138
2,000
Je ni Kweli madaktari wanapojua mgonjwa atakufa humficha na kuwaambia ndugu zake tu?

Pana tetesi huzisikia kwamba madaktari wanapotambua mgonjwa atafariki, au ana tatizo kubwa sana kuliko mgonjwa mwenyewe anavyoelewa, basi huwaita ndugu wa karibu wa mgonjwa huyo na kuwaambia "prognosis" mbaya ya ndugu yao, ikiwa ni kifo au tatizo kubwa la kiafya, huku wakimficha mgonjwa mwenyewe. Je, ni kweli?

Ni kwa nini? Kama ni kweli, haikiuki haki za mgonjwa kudhibiti taarifa zake binafsi? Nini kitatokea madaktari wakimwambia mgonjwa, "hutoboi", kama watatumia Kiswahili cha siku hizi, ili mgonjwa aweze kuweka mambo yake sawa akijua fika 'hatoboi', badala ya kubakia na matumaini hewa?

Wengine hudai kwamba mgonjwa akiambiwa ukweli, ndio atakufa kwa kihoro; hata uwezekano mdogo wa kupona utapotea, na kadhalika. Ndivyo ilivyo? Mbona nchi za mbali mgonjwa huambiwa ukweli bila kificho "hautoboi" miezi sita ijayo, na mgonjwa ndio huamua nani amuambie, nani amuache?

Ingekuwa wewe unaumwa kiasi kwamba madaktari wanajua "hutoboi". Ungependa wakuambie au wakufiche?

Ingekuwa ndugu yako anaumwa kiasi kwamba madaktari wanajua "hatoboi". Ungependa wakuambie wewe huku wakimficha mgonjwa au wakufiche wewe na kumwambia mgonjwa?
 

Rockefeller

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
511
500
Labda kwa mgonjwa aliepoteza fahamu kabisa lakini ethically Dakatri anatakiwa kumjuza mgonjwa wake juu ya hali yake na hatima yake, daktari hatakiwi kutoa taarifa kwa watu wengine tofauti na mgonjwa bila idhini ya mgonjwa mwenyewe isipokuwa kwa watoto, n.k

Mimi bora usiniambie tu hata nikifa hakuna cha kujutia kwanini nilikufa bila kujua.
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
2,138
2,000
Labda kwa mgonjwa aliepoteza fahamu kabisa lakini ethically Dakatri anatakiwa kumjuza mgonjwa wake juu ya hali yake na hatima yake, daktari hatakiwi kutoa taarifa kwa watu wengine tofauti na mgonjwa bila idhini ya mgonjwa mwenyewe isipokuwa kwa watoto, n.k

Kwa nchi zilizoendelea, hata hapo kwenye boldi huwa hakuna haki ya kuambiwa isipokuwa kwa mgonjwa tu, au mwangalizi wake anayetambulika kisheria. Hii haswa huendana na wasia-hai (Living Will) wa mhusika.

Mimi bora usiniambie tu hata nikifa hakuna cha kujutia kwanini nilikufa bila kujua.

Yaani madaktari na ndugu wanakuchora tu unavyopanga mipango mirefu, kumbe salio dogo! Naona kama inabidi taarifa hizo zitokane na uchaguzi wa mtu. Unapotibiwa unaulizwa tukwambie kila kitu au vingine tukufiche :D
 

Greg50

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
1,506
2,000
Wanaambia ndugu ili wakusafirishe mapema utakapozikwa, kusafirisha maiti ni bei gali kuliko mtu hai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom