Okay, tumefukuza madaktari, then? Ningekuwa rais hotuba yangu ingekuwa hivi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Okay, tumefukuza madaktari, then? Ningekuwa rais hotuba yangu ingekuwa hivi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Akira, Jul 26, 2012.

 1. A

  Akira Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni takribani mwezi mmoja tangu mgogoro wa awamu ya tatu ulipoanza baina ya Madaktari na Serikali, tumeendelea kujionea kila kukicha mambo mengi yanayohusiana na mgomo huo wa madaktari. Ni mwezi January mwaka huu ambapo madaktari waliitaka serikali irekebishe maslahi yao pamoja na kuwapatia mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa tiba, na madawa. Madaktari iliwabidi wagome ili kuishinikiza serikali baada ya kuona hawakutimiziwa waliyokuwa wakihitaji.

  Serikali ikiwa imekuja na kauli yake ya kusema kuwa iliwatimizia madaktari matakwa yao ikiwemo kuwafuta kazi viongozi wa kuu katika wizara ya afya, kwa maoni yangu, lile halikuwa dai la msingi la madaktari, isipokuwa baada ya kuona ni viongozi ambao dhamira na matendo yao hayana maslahi kwa afya ya watanzania ndio wakadai waondolewe kwa kuwa hawakuweza kutatua suala ambalo wangeliweza chini ya mamlaka yao.

  Hata tukihoji, serikali ikisema iliwafuta kazi kama madaktari walivyodai, hivi ni kweli, au walifanya hivyo kisiasa, kwasababu, mosi hawakuwatoa muda ule madaktari walipotaka watolewe, na pili ni kisiasa kwa kuwa watumishi wale walionesha kushindwa kumudu kazi waliyopewa kitu ambacho kilionwa na watanzania wengi wenye kutafakari kwa makini na hivyo rais hakuwa na budi ila kuwaondoa.

  Raisi akaendelea kusema, baada ya kutimiza yote, na madaktari kuona kwamba suala la mshahara halijabadilishwa, walikubaliana kukataa makubaliano hayo na hivyo kujikusanya na kuanza mgomo upya, hichi ni kitendo kilichomuudhi Mheshimiwa Raisi na Serikali yake, na kuamua kutoa tamko katika hutuba yake ya mwisho wa mwezi ambayo, haikuwa inaongelea madai ya msingi ya madaktari isipokuwa mshahara, kwamba asiyetaka mshahara huu ambao tutaweza kuuongeza basi na aache.

  Alitumia fursa hiyo kuwaasa ma-intern kwamba warudi kazini kwani wakifukuzwa watakuwa wameharibu future yao, akiwa anasema haya kumbe serikali yake ilikuwa inampango kabambe wa kuwafutia ma-intern leseni zao za kufanya kazi nchini. Nikifikiri kwa makini Napata maana ya ule usemi ulotolewa bungeni wa liwalo na liwe na wa mheshimiwa Raisi kuwaasa ma-intern kumbe nyuma ya pazia mipango yote ilikuwa ishasukwa.

  Ningekuwa mimi ni Raisi, ambaye nasimamia ustawi wa jamii hii ninayoingoza, basi hotuba yangu ingekuwa fupi sana na ingesomeka kama ifuatavyo; Ndugu wananchi, Madaktari wamekuwa watu wabaya nchini, kwa kuwa tunawalipa mshahara mkubwa kuliko watumishi waote wa serikali, nikiwa namaanisha kipato chao cha mwezi ni kikubwa kuliko cha wafanayakazi wote wa serikali, tumewawekea mazingira mazuri ya kazi na lengo letu ni kufikisha huduma nzuri ya afya kwa watanzania wote bila upendeleo wowote wa kijinsia, kimatabaka na hata kifedha.

  Ni serikali hii ambayo imeweza kupandisha hadhi hospitali zote za mikoa na kuwa kama za rufaa, na hili tunalifanyia kazi na ndio maana hospitali ya mkoa ya Tanga Bombo haina X-ray Machine, Mawenzi Hospitali ya Kilimanjaro haina chumba cha Upasuaji na hata pia Hospitali zote za serikali na zile ambazo serikali zina mkono wake kama za mashirika ya dini, ikiwapo KCMC, BUGANDO, na hata ile ya taifa MUHIMBIL, hakuna CT scan ambayo ni muhimu kama vile kipimo cha malaria katika hospitali za rufaa.

  CT Scan inahitajika, kwa mfano, katika wadi za upasuaji si chini ya wagonjwa watatu mpaka watano watahitaji kipimo hicho kwa siku, na kukosekana kwake kumegharimu maisha ya watu wengi sana, kwani vilema na vifo vimeongezeka kwa sababu tu madaktari wetu tumewaweka katika wakati mgumu, kwani wakati mwingine hawajui wamtibu mtu vipi kwa kukosa kipimo hiki. Bei ya CT Scan ni takriban pesa za kitanzania million 250 ambayo serikali haina uwezo nayo. Hatahivyo, kipimo hiki kwa bahati nzuri kipo katika hospitali ya binafsi, yani serikali tumeshindwa na mtu binafsi katika kupata ufumbuzi wa afya ya wananchi waliotupigia kura.

  Hata hivyo hali ya afya inakuwa mbaya kwa watanzania wanaolazwa hospitali kwakuwa mara nyingi utakuta wagonjwa wenye magonjwa tofauti na yanayoweza kuambukizwa wanalazwa pamoja, si mara moja, na wakati mwingine unakuta zaidi ya mgonjwa wawili wanalazwa katika kitanda kimoja, kwa mfano mwananyamala hospitali, na pia si ajabu kukuta mgonjwa katandikiwa godoro chini katika hospitali yetu ya taifa. Wanaouguwa saratani, tunatoa matibabu bure, lakini pia dawa zake hazipatikani katika hospitali zao mfano ORCI na dawa zao haziko katika bima ya afya na ni bei ghali sana.

  Lakini pia kwa kuona madaktari wanaingia katika siasa, kwa kuonesha jamii ni jinsi gani ambavyo hatufanyi kazi, tumeamua kuwafukuza ma-intern ili kuwapa fundisho jamii yeyote ya wafanyakazi ambao walitaka kutumia staili hii ya kuwasilisha, nimesikia walimu nao walitaka kufanya kama hivi, sasa akili za kupewa?

  Tumefukuza madaktari takribani 350, hii inaonesha ni jinsi gani tunaweza kuchukua maamuzi magumu, haya nayafananisha na yale maamuzi ya kuwaambia waizi wa pesa za EPA warudishe pesa ndani ya mwezi mmoja, na kusimamia chenji za rada kutengenezea madawati bila kujali kuwawajibisha waliosababisha uchafu huu.

  Tumefukuza madaktari tukijua kabisa kwamba, daktari mmoja Tanzania anahudumia watanzania 50,000 na sasa tunaupungufu mkubwa sana, kwa mfano Mawenzi Hospitali ya mkoa Kilimanjaro ina upungufu wa madaktari 150, na mpaka sasa, ndugu wananchi, clinic zote hazijafunguliwa, mfano katika hospitali ya KCMC.

  Tumeamua kuwafutia ma-intern leseni ya kufanya kazi hapa, lakini angalizo, bado ni madaktari, na wanaweza kufaanya kazi nchi yeyote ile na kupata ujira mkubwa tu kuliko hapa, na pia kuwa katika mazingira mazuri ya kazi kuliko hapa, ndugu wananchi tumewaambia wakatafute ambao wataweza kutambua thamani yao. Asanteni kwa kunisikiliza.

  Swali la muhimu kujiluza, kuna ubaya gani kwa madaktari kutaka milioni 3.5? kwani wenyewe hawana haki ya kuthaminisha huduma wanayoitoa? Je serikali haikuweza kujadiliana kwa kuwaambia madaktari kiwango ambacho wanaweza kuwalipa katika meza ya majadiliano badala ya kuja kuwahadaa wananchi kwa kuwaambia madaktari walikataa mapendekezo yetu wakati suala hilo halikutamkwa katika majadiliano? Kweli daktari anayefanya kazi usiku mzima alikuwa anastahili kulipwa 10,000 mpaka January, au 25,000 wakati huu ambapo wamesema wamefanya marekebisho?

  Tumefukuza madaktari, hii itaboresha huduma za afya? Nini kinafuata?
   
 2. l

  lunyamu Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nimeambiwa kuna nchi moja ya jirani imesema ingependa hata kuwachukua wote, watanzania ambao kazi yao ni kushangilia jinsi serikali yao inavyovurunda wamekaa kimya...wanadhani wanawakomesha madaktari, uhalisia kwa mikoa ya dar es salaam na pwani uwiano wa daktari na wagonjwa ndiyo 1:30,000 lakini mikoa ya pembezoni mfano kigoma, rukwa, mtwara, Mara na Lindi ni 1:100,000. kwa hao 380 ni sawa na wananchi 11,400,000 na zaidi kukosa huduma halali. Nakiona kisiwa cha amani Tanzania tunakiteketeza wenyewe watanzania
   
 3. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Soma signature yangu hapo chini.
   
 4. M

  MLO Senior Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kilo moja ya dhahabu kwa bei ya leo ya hapa TZ ni (80,000,000)*4=320,000,000.????????????????????
  Upeo wa kufikiria unawasumbua watawala!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. B

  Bwanamdogo Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni katika nchi km Tanzania tu ambako unaweza kusikia kauli za ajabu ambazo zimejaa jeuri na kisasi ambako watawala wanaweza kufanya maamuzi yoyote hata km maamuzi hayo yataleta madhara zaidi.
  Km ana jeuri anatakiwa atuambie wtanzania kwa kuamuru Medical council of Tanganyika kuwafutia leseni interns ametusaidiaje watanzania wa kawaida kwenye upatikanaji wa huduma za afya. Na pia atuambie anampango gani na sekta ya afya siku za usoni km amewaambia madaktari wakatafute ambako wanaweza kupata malipo mazuri ambako ninauhakika ni nje ya nchi, huo uhaba wa wafanyakazi sekta ya afya ambao ni wimbo wa kila siku utaisha lini na kwa namna gani km tunawakatisha tamaa namna hiyo waliopo na kuwaambia waondoke?
   
 6. B

  Bwanamdogo Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni katika nchi km Tanzania tu ambako unaweza kusikia kauli za ajabu ambazo zimejaa jeuri na kisasi ambako watawala wanaweza kufanya maamuzi yoyote hata km maamuzi hayo yataleta madhara zaidi.
  Km ana jeuri anatakiwa atuambie wtanzania kwa kuamuru Medical council of Tanganyika kuwafutia leseni interns ametusaidiaje watanzania wa kawaida kwenye upatikanaji wa huduma za afya. Na pia atuambie anampango gani na sekta ya afya siku za usoni km amewaambia madaktari wakatafute ambako wanaweza kupata malipo mazuri ambako ninauhakika ni nje ya nchi, huo uhaba wa wafanyakazi sekta ya afya ambao ni wimbo wa kila siku utaisha lini na kwa namna gani km tunawakatisha tamaa namna hiyo waliopo na kuwaambia waondoke?
   
 7. M

  MLO Senior Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtu anweza akakubali awe mjinga kipindi cha intern baada ya hapo achukua leseni na kutimukia kwenye masilahi
   
 8. Xidian

  Xidian JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Inasikitisha sana na kuhuzunisha kila ninapowaona wagonjwa wodini , wodi inayohitaji madaktari 8 leo kuna daktari mmoja na wod zingine hakuna hata daktari, je kutakuwa na ufanisi kweli? Siku hizi hakuna service za wodini kama ilivyokuwa zamani ,
  Hivi J.Kikwete wakati unafukuza intern ulikuwa na njia gani mbadala? I cant afford seeing patients dying on my hands. Let me stop here maana kila ninavyoandika nazidi kuumia zaidi.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Nimekua nachangia ktk sredi kama hii kwa kusema kwamba mgogoro huu kati ya serikali na madaktari madhara yake yatajionyesha wazi miaka michache kuanzia sasa! Taifa litapoteza madaktari wengi vijana,watakimbilia nje ya nchi. Vijana wengi waliopo ktk shule za Sekondari ambao wangependa kuwa madaktari wataikimbia fani ya Tiba! Kwasababu watawala tulionao wanawaza leo kuhusu maslahi ya familia zao na chama chao mpaka wanafukuzwa madarakani madhara ya matendo yao utakuwa ni mzigo usiobebeka kwa taifa muda mrefu ujao.
   
 10. B

  Bob G JF Bronze Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unapoamua kumpigia gitaa mbuzi ukitegemea atacheza na kufurahia mziki wako ni sawa tu na kumwambia mwendawazimu amwonee huruma mtu mwingine na wakati yeye kasema liwalo na liwe, ikibidi watanzania wote mfe sawa sitakubaliana na madai ya ma dr na nimefunga majadiliano, acha wafe mi na ndugu zangu mafua India acha wamalizane wenyewe hawa wajinga
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kama India ingekua hapa jirani mfano Nairobi, Kampala, Kigali na miji ya nchi jirani wala nisingestuka na ujinga wako umeandika hapo juu. Ama mwenzetu unatumia ungo?! Ukipanda tu umefika India?!
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mimi nina wasiwasi kuwa jamaa wote hao wanaweza kuchukuliwa na serikali ya Rwanda tu halafu wakalipwa vizuri sana. Nilikuwa nafuatilia ziara ya Clinton wiki iliyopita huko Rwanda kama ilivyokuwa covered na CNN, inaonyesha kuwa yule Dikteta wa Rwanda hana mchezo wala mabo ya kijinga; anataka results tu. Ninajua watu kadhaa kutoka Tanzania ambao wana madaraka makubwa sana huko na kwa malipo mazuri tu kwa sababu ya results zao!!
   
 13. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  single ya madaktari mbona imeshachuja, tunangoja ya walimu!
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Siku utakapolazwa serious kitandani ama ndugu yako wa karibu ndipo utafahamu kama hiyo single imechuja ama la!
   
 15. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  tuna punguza idadi ya wananchi! maana wamekuwa weng mno!
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Tafadhali nakuomba Hotuba yako ianze na maneno hayo hapo chini...


  washabiki na wapenzi wa Simba Sports Club
  wamesusia kufturu Chapati zinazotengenezwa na
  kiwanda cha Azam.
  Hii inatokana na kipigo cha Gombania Daku
  walichokipata hivi karibuni
   
 17. i

  inocent Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa taarifa zilizopo ni kuwa vyuo vya udakitari wameambiwa undergraduate wote wafaulu.Hakuna mwanafunzi kufeli hata kama ni kilaza.Pia senate za shule husika zimekaa mapema kuliko ilivyo kawaida ili kutoa madakitari wa intern kufidia pengo la waliofukuzwa.

  kwangu nadhani sio solution kwa wakati huu wa mgogoro maana wengi hawatafanya application mapema na pia wengi watakuwa wamepitishwa tu.Tuombe Mungu atunusuru maana haya maamuzi mengine outcome yake ni mbaya.Kwa tunaotibiwa hapa tanzania tuko hatarini
   
 18. A

  Akira Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha msingi cha kukiangalia hapa ni; madai ya madaktari yalikuwa ya msingi au siyo, kama ndivyo, kuleta madaktari wengine si issue kama hapatakuwa na CT Scan, hapatakuwa na X-Ray...tutakuwa tunachochea maafa zaidi kuliko kujenga.

  Lakini kwanini pia wananchi hawahoji wanapokosa vifaa tiba hospitali? kwa nini hawahoji wanapokosa dawa? na pia hata wakilazwa mgonjwa zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja pia hawahoji!
   
Loading...