JE NI KOSA KUMPA JIRANI MAJI YA IDARA YA MAJI?

WABALLA Inc

JF-Expert Member
Sep 2, 2014
2,706
2,000
Habari wana jamvi?
Kwa wale wenye uelewa na kanuni za Idara za Maji, ninatumia maji ya bomba kutoka Mamlaka ya Maji ya Mji mmoja. Ninavyojua kisheira hairuhusiwi kuuza maji bila idhini ya mamlaka husika. Nina jirani yangu amabye aliomba kutumia/ kuwa anachota maji. Kama mnavyojua jirani yako ndio ndugu yako sikumkatalia akawa anachota. Kwa sasa sipo eneo hilo ila wamekuja mafundi wa idara na kunikatia maji kwa kigezo kuwa ninauza maji. Nimejaribu kuongea nao kwa njia ya simu ila wamenikomalia kuwa lazima wakate kwa kusisitiza kuwa nauza maji. Mbaya zaidi wanasema kuna jirani yangu kapiga simu (yeye ana kiali cha kuuza maji) na analalamika kuwa namuharibia biashara hivyo itaonekana wamenipendelea wasipokata maji.

Swali langu ni , je hairuhusiwi kumpa jirani yako maji kisheira?
 

Nsamaka

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
5,703
2,000
Sijui huko kwenu ila huku nilipo mm naona majirani wengi wanachangia mabomba na bili ikija wanachangia wote.
Hii nayosemea mm ni kwa matumizi ya nyumbani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
15,373
2,000
Huyo anayeuza maji ndo kakuchongea, una muharibia biashara.

But infact hakuna kosa lolote hapo.
 

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,632
2,000
Jirani ndio ndugu yako endelea kumsaidia hila muamasishe naye ajiunge aunganishiwe maji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom